Pages

Pages

Tuesday, December 31, 2013

SSRA yajadiliana na jukwaa la wahariri kuhusu mpango wa kupanua wigo wa hifadhi ya jamii


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Bi. Irene Isaka (aliesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na hali halisi ya sekta ya hifadhi ya jamii nchini,changamoto na mafanikio wakati wa semina ya siku moja iliyotolewa kwa Wahariri wa Nyombo mbali mbali vya habari nchini kupitia Jukwaa la Wahariri,iliyofanyika Mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Oceanic, Bagamoyo.
Mhariri Mkuu wa gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu akiuliza swali mara baada ya uwasilishwaji mada.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka akisisitiza jambo juu ya umuhimu wa vyombo vya habari katika kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi.kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini, Absalom Kibanda  na kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamashishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde – Msika.

Maajabu, jamaa apanda juu ya mnara akishinikiza kuonana na Rais Kikwete


 Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela
 Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan kwaajili ya kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar Es Salaam Leo
Hapa akishushwa na askari wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokoaji
Hapa Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akiwa amemuweka begani na Kushuka nae chini Mara baada ya kufanikiwa Kumshika vizuri kwaajili ya kumteremsha chini bila kupata madhara.
 Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Hassan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushushwa juu ya Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji muda mfupi uliopita Ubungo jijini Dar.
 Tukio likiendelea huku wakazi wa jiji la Dar Wakiendelea kushuhudia. CHANZO NI LUKAZA BLOG...........

Monday, December 30, 2013

Cindy aleta kicheko Mapacha Watatu

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UJIO wa mwanamuziki wa bendi ya Mapacha Watatu, Catherine Cindy umeleta kicheko kwa viongozi wake, baada ya kuwa nje ya nchi kwa miezi mitatu.
Meneja wa Mapacha Watatu, Hamis Dacota, katikati akiwa na wanamuziki wake, Jose Mara kulia na Khalid Chokoraa kushoto.
 
Cindy aliwasili nchini juzi akitokea nchini Japan, hivyo kusubiriwa kwa hamu na wadau wa bendi hiyo inayoongozwa na Khalid Chokoraa na mwenzake Jose Mara kama wakurugenzi.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mapacha Watatu, Khamis Dacota, alisema kuwa mwanadada huyo ameleta uhai zaidi kutokana na ubora wake jukwaani.
 
“Catherine si mtu wa kawaida na kila mdau wa muziki wa dansi anafahamu uwezo wake, hivyo sisi wote tumefarijika na kurejea kwake,” alisema.
 
Mwanadada huyo ni miongoni mwa vijana wadogo wenye ujuzi wa kucheza na sauti zao, huku makali yake yakitarajiwa kumuweka juu mno katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.
 

Msanii auelezea wimbo wa Safari ya Tanga

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Ahmad Salum ama (Mady Salu), amesema kwamba ili aweze kushiriki katika Tamasha la Handeni Kwetu ilimlazimu aingie Studio kurekodi wimbo uliokwenda kwa jina la ‘Safari ya Tanga’.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mady Salu alisema kwamba hatua hiyo ilisababishwa na uchu wake wa kupania kupanda katika jukwaa la tamasha lililofanyika kwa mara kwanza.
 
Alisema mara nyingi wasanii wachanga wamekuwa wakipata nafasi hiyo mara chache mno, hivyo nafasi yake ya kupangwa kuwapo katika tamasha hilo kulimfanya ajiandaye vizuri.
 
“Nisingepata nafasi ya kushiriki ningeumia kwakuwa niliambiwa namna gain ya kufanya ili niweze kufanya vyema katika tamasha.
 
“Tamasha lilihusu utamaduni, hivyo kitendo cha kurekodi wimbo wangu wa Safari ya Tanga hakika ulinitangaza vizuri na kuonyesha pia shauku ya kutangaza kipaji changu katika muziki wa kizazi kipya,” alisema.
 
Mady Salu aliwahi kuwapo katika kundi la Ngovita Clew lililotambulisha wimbo wa Maisha Miangaiko, ambalo baadaye liligawanyika.

Sunday, December 29, 2013

Handeni wazitamani Simba na Yanga kukipiga kwenye Uwanja wa Azimio wilayani kwao


Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, mkoani Tanga, Thomas Mzinga, amesema kwamba Uwanja wao wa Azimio unastahili kukutanisha vigogo vya Simba na Yanga, katika michuano yoyote nchini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, pichani.
Akizungumza na Handen Kwetu Blog mapema wiki hii wilayani Handeni, Mzinga alisema kuwa hiyo ni kutokana na maandalizi na mwonekano wa uwanja wao wa michezo.


Alisema kuwa Uwanja wao ni mkubwa na unastahili kukutanisha timu kubwa na vigogo wa Tanzania Bara, vikiwapo Simba na Yanga.


“Tunajivunia kuwa na uwanja mzuri na muwajulishe huko kuwa wanapaswa waje wacheze huku katika mashindano yao mbalimbali.


“Tunaamini Uwanja huu pia ukikamilika kwa baadhi ya ukarabati wake, basi utachangia kwa kiasi kikubwa kuleta watu mbalimbali, hasa timu kubwa zitakapokuja,” alisema Mzinga.


Hata hivyo, kiu ya Mzinga na viongozi wa serikali wilayani humo inaweza kutimia kama wataipigania au kuwashawishi viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuhakikisha kuwa timu ya JKT Mgambo itaufanya Azimio kuwa uwanja wake wa nyumbani.

Twanga kuendeleza moto wake Leaders Club leo jijini Dar es Salaam


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BAADA ya kufanya shoo ya aina yake wilayani Kilosa mkoani Morogoro, Ijumaa na Jumamosi kuwachezesha Mango Garden, bendi ya The African Stars Twanga Pepeta, leo inawapa burudani wapenzi wake katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.



Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehan, alisema kuwa vijana wao wapo imara kwa kutoa burudani katika maeneo yao ya kujidai.


Alisema Leaders na Mango Garden ni maeneo ambayo lazima wawepo kika wiki, hivyo wanaamini mashabiki wao wataendelea kupata burudani kamili kutoka kwao.


“Ijumaa tulicheza Kisigino na mashabiki wetu wa Morogoro katika Ukumbi wa Babylone uliopo wilayani Kilosa na kuwaonyesha makali ya Twanga Pepeta,” alisema Rehani.


Baadhi ya wakali wa Twanga Pepeta wanaotamba katika bendi hiyo ni pamoja na Luiza Mbutu, Salehe Kupaza, Grayson Semsekwa, Dogo Rama, Kalala Junior na wengineo.

Malaika bandi kuwapa raha Tanga Hoteli leo jijini Tanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BENDI iliyokuja kwa kasi katika anga ya muziki wa dansi hapa nchini, Malaika, leo inawapa raha mashabiki wa jijini Tanga, katika Ukumbi uliopo ndani ya Tanga Hoteli.


Safari ya bendi hiyo katika mkoa wa unaotajwa katika sekta ya uhusiano wa kimapenzi ni mwendelezo wa kujitangaza na kujitanua zaidi kwa mashabiki wao wa muziki wa dansi.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Fadhili Mfate, alisema kuwa mashabiki wa jijini Tanga watapata vitu vya aina yake kutoka kwa wanamuziki wenye makali ya kutisha.


“Hii ni safari ya mwendelezo kwa mashabiki wa Tanga ambapo mara baada ya kuzindua bendi yetu tulikuja kujitambulisha kwao.


Tunaamini wote watakaohudhuria shoo wataelewa kwanini tunajitamba kuwa tumesheheni vijana wenye uwezo wa juu kisanaa,” alisema Mfate.


Malaika ipo chini ya Mkurugenzi wake Michael Loki, ambapo Rais wa wanamuziki ni Christian Bellah, anayeheshimika mno katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.

Kaseba achekelea kumdunda Alibaba


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amesema ushindi wake dhidi ya Ramadhan Alibaba, ulitokana na maandalizi yake pamoja na dhamira ya kuonyesha makali yake.


Pambano lao lilimalizika katika raundi ya nne, baada ya Alibaba kushindwa kuendelea, hivyo mwamuzi kumpa ushindi Kaseba.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema kuwa anaamini maandalizi yake yatazidi kumuweka katika nafasi nzuri ya kutangaza makali yake kwenye masumbwi.


Alisema kuwa makali yake katika mchezo wa ngumi yanampa imani kuwa ataendelea kuwa juu kiasi cha kutoa kichapo kwa kila bondia atakayekutana naye ndani ya ulingo.


“Sijabahatisha kucheza na kumpiga Alibaba, maana nimedhamiria kuonyesha umwamba wangu kwa kila atakayepanda na mimi ulingoni,” alisema Kaseba.


Hata hivyo, Alibaba mwenyewe alisikika akilaumu ushindi wa Kaseba akisema mara kwa mara alikuwa akimchezea rafu, hivyo ameshinda kwa hila na si uwezo kama anavyojigamba.

Msondo Ngoma walivyoendeleza ubabe wao TTC Sigara Chang'ombe

Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani kwa mashabiki walioudhulia onesho lao lililofanyika TTC Chang'ombe jumamosi kutoka kushoto ni Eddo Sanga,Othumani Kambi , Shabani Dede na Hasani Moshi.
Wapuliza ara wa bendi ya Msondo ngoma wakiwajibika wakati wa onesho lao kutoka kushoto ni Shabani Lendi,Hamisi Mnyupe na Romani Mng'ande.
Wapiga magita wa msondo ngoma wakifulumusha magita hayo wakati walipokuwa wakitoa burudani kutoka kushoto ni Abdul Ridhiwani na Mustafa Pishuu. Picha zote ni kwa hisani ya Msemaji wa Msondo Ngoma, Rajabu Mhamila, Super D.

Thabit Abdul atangaza kuunda kundi lake na kukimbia rasmi Mashauzi Classic

Mwanamuziki mkali wa kuandaa na kupangilia muziki mwenye uwezo wa kupiga ala zote za muziki, kama, Kinanda, Gitaa zote yaani Solo, Bass na Rhythim, na zaidi katika kukaanga 'Chips', kuzicharaza drams, Thabiti, Abdul, pichani, ameamua kuachana na kazi za kutumwa na badala yake ameamua kuunda kundi lake jipya la Taarab, linalokwenda kwa jina la Wakali wao.

Akizungumza kuhama kwake, Thabit alisema kuwa kundi lake hadi sasa lina jumla ya wasanii 13, na linaendelea na mazoezi yake maeneo ya Kinondoni katika ukumbi wa Way Bar ili kujiweka sawa kwa ajili ya kuandaa albam yao ya kwanza itakayokuwa na jumla ya nyimbo nne.

Aidha alisema kuwa katika bendi hiyo iliyo chini ya Meneja wake, Godfrey Ngowi, hadi sasa imekwishaanza kufanya shoo katika baadhi ya maeneo huku ikiwa na waimbaji wengi wapya yaani Ma Under Ground, na wapiga vyombo aliowataja kwa majina kuwa ni Jumanne Ulaya, anayepiga solo, Shomari Zizu, anayepiga Gitaa la Bass, Omary Alli na Ndage Ndage, wanaopiga Kinanda.

Bendi hiyo inatarajia kutambulishwa rasmi mwezi Februari na kuzinduliwa ramsi mwezi wa nne katika Sikuku ya Pasaka, ambapo itazinduliwa rasmi bendi hiyo ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa Video zake, Albam na Vyombo vipya, ambapo kila shabiki atakayeingia getini atapatiwa Cd moja ya Audio yenye nyimbo za bendi hiyo.

Thabiti, alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Kalieni Viti Sio Umbea, Lipo Linalo Kusumbua, Mtu Mzima Hovyo na Subira Haina Kikomo.   Kwa hisani ya Sufiani Mafoto.

Mwimbaji wa Injili Rose Muhando awakuna wakazi wa Tanga


Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho a.k.a Injili,na anaetamba na wimbo mpya wa Facebook,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati wa muendelezo wa tamasha la Krisimasi lililofanyika leo Mkoani Tanga.Tamasha hilo ndio kwa mara ya kwanza linafanyika mkoani humo,limezindundiliwa jijini Dar siku ya Krisimasi ndani ya uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watazamaji lukuki.Tamasha hilo baada ya kufanyika mkoani Tanga,kesho litafanyika jijini Arusha na baadae mkoani Dodoma likiwajumuisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

 Pichani kulia ni Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za kusifu na kuabudu kutoka nchini Zambia, Epfrahim Sekeleti akiimba pamoja na mwimbaji mwingine mahiri wa nyimbo injili hapa nchini,Bon Mwaitege pichani shoto.

Saturday, December 28, 2013

Vijana waaswa kujituma uwanjani ili wafikie malengo yao

Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

VIJANA wenye vipaji na uhitaji wa kucheza soka wametakiwa wacheze soka kwa kujituma ili wafikie malengo, badala ya kutegea katika mazoezi hivyo kujiweka katika hatari ya kushindwa kufika mbali na kutimiza malengo yao.


Hayo yamesemwa na kocha wa timu ya soka ya Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Sufian Omary, katika mazoezi ya vijana wake wanaoendelea katika mashindano ya Mbuzi Cup inayokutanisha timu mbalimbali za Kata ya Kwamatuku.


Akizungumza mapema wiki hii wilayani humo, Omary alisema kwamba vijana wengi wanaopenda kuwika katika soka, wameshindwa kufika mbali kutokana na kutegea katika mazoezi yao uwanjani.


“Wachezaji wote wenye malengo yao lazima wafanye mazoezi makali na kuweka bidii uwanjani, hivyo lazima mcheze kwa bidii, ukizingatia kuwa hakuna mashindano madogo hata kama tungekuwa tunagombea kuku.


“Naamini tukifanya hivyo itakuwa ni njia ya kuiweka timu yetu katika nafasi nzuri zaidi, huku ikiwa njia ya wachezaji wenyewe kuwa katika wakati wa kuwaza maendeleo katika mashindano,” alisema.


Timu ya Komsala ni miongoni mwa maeneo yenye wachezaji wazuri kiasi cha kutia hamu kuwaangalia wanavyokuwa uwanjani, huku wakishiriki katika mashindano ya kugombania mbuzi katika Kata ya Kwamatuku, yanayofanyika katika Uwanja wa Kijiji cha Kweingoma.

Soma Waraka wa Absalom Kibanda kwa Rais Jakaya Kikwete na Watanzania kwa ujumla

Na Absalom Kibanda, pichani na haya ndio maoni yake.
MHESHIMIWA Rais wangu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Nakusalimu kwa salamu ya utii inayotambua na kuheshimu kwa dhati mamlaka makubwa na ya juu uliyonayo kama mkuu wa taifa letu ambalo mazingira yake ya leo yanapaswa yawe wenye mwelekeo wa kushangilia kama si kujivunia uhuru ambao tuliupata mwaka 1961 na 1964 kwa kutegemea upande tulipo katika muungano wetu.

Mheshimiwa Rais, najisikia faraja iliyojaa majonzi moyoni kupata fursa hii adhimu kukuandikia waraka ambao msukumo wake unasukwasukwa na dhamira njema kabisa ambayo aghalabu kiini chake si kingine bali mapenzi mema kwa nchi na viongozi wetu wote.

Ni faraja kwa kuwa nimepata fursa ghali na adimu ya kuteta na kiongozi wetu mkuu kwa upendo, uhuru na kwa kujiamini, huku nikiwa na uchungu pia kwa sababu ujumbe ambao unabebwa na waraka huu ni wa kuumiza sana nafsi, roho, akili na mwili.

Mheshimiwa Rais, wewe ni kiongozi wa Watanzania wote tukiwamo sisi ambao baadhi ya wateule wako wameamua kwa sababu wanazozijua wao na wakati mwingine wakidai kwa maelekezo ya wakuu wao kutujengea taswira zinazotufanya tuonekane tu watu wa ovyo na kada ya wanajamii waliokosa utu na eti tunaopaswa kufundishwa hekima na somo la uzalendo ambalo limekuwa sehemu ya makuzi yetu nyumbani, shuleni, jeshini na ndani ya jamii.

Watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 kujiunga na elimu ya sekondari 2014

Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule mbali mbali za Serikali hapa nchini

Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.

Akitangaza idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kutokana na tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa hadi ifikapo machi mwaka mwakani.

Aidha, Sagini anaeleza takwimu za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.

Amesema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 412.

Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.

Friday, December 27, 2013

Mpira Pesa wazidi kumchulia mwenyekiti wao wa Simba, Aden Rage


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Tawi la Mpira Pesam Ustadh Masoud, amesema moto wa kutokuwa na imani na mwenyekiti wao Ismail Aden Rage umesambaa nchi nzima, kutokana na kiburi anachoonyesha mwenyekiti wao.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Masoud alisema kwamba Rage ni mbishi asiyependa kusikiliza ushauri wa mtu yoyote, huku akijidanganya kwamba ni Mpira Pesa tu wasiyokuwa na imani naye.


Alisema mara kadhaa Rage anatushutumu sisi Mpira Pesa, ila wakati huu kila mtu anayeipenda Simba hafurahishwi na mwenendo wa mwenyekiti wetu, ndio maana hata ushauri aliyopewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ya kuitisha Mkutano ameshindwa kuutekeleza.

Malaika bendi wazidi kuchapa mwendo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa bendi ya Malaika, Michael Loki, amesema kwamba baada ya kuonyesha makali yao, sasa wanajipanga zaidi kulinda heshima yao kwa kuhakikisha kuwa mashabiki wao wanapata burudani kali.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Loki alisema kwamba vijana wao wapo imara wakiongozwa na Rais wa bendi hiyo, Christian Bellah, hivyo wanaamini wadau wao wataendelea kupata vitu vizuri kutoka kwao.


Alisema kuwa katika shoo zao nyingi walizokuwa wakifanya tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo, mashabiki wamekuwa wakiingia kwa kwa wingi na kuonyesha shauku ya kuburudika.


“Tulikuwa na kiu kubwa ya kuonyesha cheche zetu katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, hivyo hakuna kitakachotufanya tulale na kuacha wengine wakifanya vyema katika ramani ya muziki huo,” alisema.


Uzinduzi wa bendi hiyo ulifanyika mapema mwezi uliopita katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama, huku ukihudhuriwa na watu wengi waliokwenda kuangalia manjonjo ya vijana wa Malaika.

Ukakamuvu ndio nyumbani kwao vijana wa JKT

Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Mgambo, wilayani Handeni mkoani Tanga, wakionyesha umahiri wao wa kucheza sarakasi katika Tamasha la Utamaduni wilayani humo la Handeni Kwetu 2013 lililofanyika Desemba 14 mwaka huu katika Uwanja wa Azimio. Vijana hawa kwa pamoja walishirikiana na vikundi mbalimbali vya ndani na nje ya Handeni kulizindua Tamasha hilo la aina yake, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya hiyo, DC Muhingo Rweyemamu.Picha na Fadhili Athumani.

Bondia Kalama Nyilawila ajifua vikali kumchakaza Maokola Desemba 31 mwaka huu

Msimamizi wa Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza
makaburini, Bernald Lumbila (kushoto) akimwelekezai bondia Kalama Nyilawila jinsi ya kupiga ngumi katika mbavu Dar es saam Nyilawila anajiandaa na mpambano wake dhidi ya Ibrahimu Maokola utakaofanyika Desemba 31 katika Ukumbi wa Msasani Clabu.
Kalama Nyilawila akijifua
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Kalama Nyilawila yupo katika mazoezi makali ya mwisho mwisho kabla ajamkabili mpinzani wake Ibrahimu Maokola siku ya Desemba 31  mpambano wa kufunga mwaka utakaoshirikisha mabondia mbalimbali akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kalama ameseme yeye yupo fiti wakati wowote kwa ajili ya mpambano huo kwa ana usongo wa kuonesha ngumi zinachezwaje kwa mabondia chipkizi nchini

Mpambano huo utaanza kabla ya bondia Fransic Miyeyusho kupanda jukwaani kuvaana na David Chalanga kutoka Kenya mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi.

Wednesday, December 25, 2013

Wananchi Misima waondolewa hofu kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji Handeni



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

WANANCHI na wakazi wa Kata ya Misima, wilayani Handeni mkoani Tanga, wameombwa kutokuwa na wasiwasi na hatua ya kuingizwa kwenye Halmashauri ya mji kwakuwa mpango huo sio mbaya kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Thomas Mzinga, akiwa kwenye moja ya matukio ya kijamii wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, alipozungumza na Mtandao wa Handeni Kwetu, juu ya hatua mbalimbali za kuunganisha eneo hilo na Handeni Mjini.

Alisema mchakato wote wa kuunganisha mji huo na Kata ya Misima ulifuata sheria zote, huku akisema woga wa wananchi unatokana na hoja dhaifu kuwa viwanja vyao vitauzwa na serikali.

“Sio kweli kama kuingia kwenye Halmashauri ya Mji basi viwanja vyote na mashamba yaliyokuwapo yatauzwa ovyo na watendaji wa serikali, maana hiyo si sababu ya kupanua mji wetu.

“Wananchi wameaminishwa uongo ili suala hilo lisiwe na mafanikio, hivyo tunaamini tutaendelea kuhamasisha wananchi wetu na Watanzania kwa ujumla ili kwenye mambo ya kimaendeleo tufanye kama inavyopangwa na viongozi wa serikali kwa ujumla wake,” alisema Mzinga.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, hatua ya kuunganisha eneo la Misima katika Halmashauri ya Mji ni kuweka mikakati kabambe ya kuupanua mji wote wa Handeni na kusogeza pia maendeleo karibu na wananchi.

Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, wananchi wa Misima wamekuwa wakivutana na viongozi wa serikali ya wilaya ya Handeni wakigoma kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji kwa madai kuwa bado mapema na kijiji hicho kipo mbali kabisa, huku wakiona kuwa huenda ni mipango ya waheshimiwa hao kusogea karibu ili kuteka mashamba yao.



Tunawatakia sikukuu njema ya Christmas wasomaji wote wa Handeni Kwetu Blog

LEO ni Desemba 25 Wakristo wote nchini wanaadhimisha sikukuu ya Christmas. Sikukuu hii muhimu kwa wakristo wote duniani ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu kristo.
Sisi Handeni Kwetu Blog tunawatakia sikukuu njema. Tunaomba sikukuu hii iadhimishwe kwa amani,upendo na ushirikiano kwa jamii yote. Pia sikukuu hii isiadhishwe kwa kufanya mambo maovu kama vile ngono, uvutaji bangi na mambo mengine mabaya badala yake tufanye mambo yanayompendeza Mungu.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal, amjulia hali mzee Ali Machano Muasisi wa ASP

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal,picha juu na chini akizungumza na Mzee Ali Machano (122) mmoja kati ya Waasisi wa ASP wakati alipomtembelea kumjulia hali kijijini kwake Moga Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Disemba 24-2013. (Picha na OMR).

MOHAMED MATUMLA NASIBU RAMADHANI KUMARIZA UBISHA CHRXMAS

Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao leo katika

ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam leo katikati ni promota wa mpambano huo kaike siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Promota kaike Siraju akiwainua juu mikono Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani kwa ajili ya mpambano wao wa kugombea pikipiki siku ya sikukuu ya Xmasi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, December 24, 2013

Umeme sasa bei juu kuanzia Januari Mosi mwakani


Taarifa ya EWURA YA bei mpya za umeme zitakazoanza kutumika Januari, Mosi,2013
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.

Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa 
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. 

Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).

Msondo na Sikinde hapatoshi kesho TCC Club Chang'ombe

Na Mwandishi Wetu

Mabingwa wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra “Sikinde” kesho mchana zitachuana vikali katika viwanja vya TCC Club  Chang’ombe, Temeke.

Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi litakuwa la kufunga mwaka 2013 na pia litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa muziki wa dansi nchini mwaka huu.

Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano huo litanzaza saa nane alasiri hadi majogoo.

Vijana wa Msondo Ngoma pichani.
Kapinga alisema Sikinde wataingia TCC wakitokea Bagamoyo walipokuwa wakipiga kambi wakati kambi ya Msondo Ngoma imebaki kuwa siri kwa muda wote.

Mratibu huyo alisema kila bendi litapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa hujuma.

Kapinga alisema kila bendi itatapewa muda wa saa moja kupiga jukwaani kabla ya kumpisha nyingine.

Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera  alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaibuka kidedea.

Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni  'Nimuokoe Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali' na  'Suluhu'.