https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, March 12, 2013

Balozi Kagasheki: Wanawake jitumeni kuinua uchumi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kagasheki, akizindua rasmi kikundi cha Habari Group kinachojumuisha waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari, ufunguzi uliofanyika Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam juzi. Anayeshuhudia kushoto ni Mratibu wa kikundi hicho, Rabia Bakari na wageni wengine waalikwa. Picha na Kambi Mbwana.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kagasheki, amewataka wanawake kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wao, ikiwa ni pamoja na kuendelea kujiunga kwenye vikundi.


Kagasheki aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika ufunguzi wa kikundi cha waandishi wa habari wanawake kutoka vyombo mbalimbali vya habari, kinachojulikana kama Habari Group.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Kagasheki alisema ili uchumi wa Tanzania kukua, ni pamoja na kuona wanawake wanajiwezesha zaidi kwa kufanya biashara mbalimbali kwa kupitia vikundi vyenye uwezo mkubwa wa kusaidiwa pamoja na kukopeshwa.

Alisema mara baada ya kualikwa kwenye uzinduzi wa kikundi cha Habari Group kinachojumuisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari, alijisikia faraja akiwa akiwa na lengo la kuwawezesha ili maisha yao yawe mazuri kwa mjumuiko huo.

"Naunga mkono juhudi zenu za kila aina katika kuhakikisha kuwa mnajikomboa kuanzia mwanzo wa ufunguzi huu na kuendelea, maana nyie waaandishi habari mkijikwamua, naamini Uchumi unaotakiwa utafika mahali pazuri.

"Naomba muendelee kuwa pamoja na kubuni vitu vyenye tija katika maisha yenu, maana ili muendelee, ni wazi vikundi vya aina hii vinatakiwa kuendelea kuundwa kwa kila sekta," alisema Kagasheki.

Awali mratibu wa kikundi hicho cha Habari Group, Rabia Bakari, aliwashukuru wahudhuriaji wote katika hafla ya ufunguzi huo, Angela Kairuki, ambaye ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwamo PPF na wengineo.

mwisho

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...