Nyosh El Sadaat
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa bendi ya FM Academia,
maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, Nyosh El Sadaat, amesema kwamba wamebuni aina
zaidi ya 300 ya uchezaji, ikiwa ni mikakati ya kuboresha zaidi burudani zao.
Nyosh aliyasema hayo mwishoni
mwa wiki, alipokuwa akizungumzia mikakati ya kuwaweka juu katika mwaka huu,
huku akisema aina zaidi ya 300 wameandaa kwa ajili hiyo.
Akizungumza kwa kujiamini,
Nyosh ambaye pia anajiita kama Rais wa Vijana, alisema kuwa aina hiyo ya
uchezaji itaendeleza mazuri yao ya kuwapatia mashabiki wao.
Alisema anaamini kuwa kila
anayebahatika kuona shoo yao, ataamini kuwa wao ni bora zaidi katika tasnia ya
muziki wa dansi, huku wakijikita zaidi kutoa burudani kwa wapenzi wao.
“Wazee wa Ngwasuma ni bendi
yenye mikakati kabambe kwa mwaka huu, hivyo naamini kwa aina hizi 300 za
uchezaji katika shoo moja, zitatuweka juu zaidi.
“Naomba mashabi wetu waendelee
kutuunga mkono maana tumepania na hatuwezi kurudi nyuma kamwe, hasa kwa kutunga
nyimbo nzuri na jinsi ya kufanya shoo zenye ubora zaidi,” alisema.
Wazee wa Ngwasuma, wamekuwa
wakijimaarisha zaidi kwa ufanyaji wao wa shoo, hasa kwa kitendo chao cha
kushuja chini ya jukwaa na kuanza kuwaonyesha mashabiki wao mitindo yao mipya,
kila baada ya wiki moja, hasa onyesho lao la kila Jumapili, linalofanyika New
Msasani Club.
No comments:
Post a Comment