BONDIA wa ngumi za kulipwa
nchini, Mbwana Matumla, amesema pambano la Japhet Kaseba na mpinzani wake
Maneno Oswald, litakuwa zuri kutokana na umahiri wa wakali hao
wa masumbwi hapa nchini.
Mabondia hao wanatarajia
kuzipiga Machi mbili katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, jijini Dar es
Salaam, huku mgeni rasmi akiwa ni Kamanda wa Polisi KanDA Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Matumla alisema Kaseba na Osward ni mabondia mahiri katika ngumi
nchini, hivyo mpambano wao utakuwa wa aina yake.
Alisema kwamba anaamini
mashabiki watapata kitu kizuri kutoka kwa mabondia hao, maana ni hodari wa
kurusha masumbwi pamoja na uzoefu wa aina yake.
“Pambano la Kaseba na Oswald
litakuwa la aina yake, maana ni mabondia mahiri na wenye uwezo mzuri, hivyo
naamini upinzani utakuwapo kwa wawili hao ulingoni.
“Wamekuwa kwenye mvutano wa
siku kadhaa tangu kutangazwa kwa pambano hilo, katika suala zima la masumbwi,
lolote linaweza kutokea, hivyo tusubiri tupate majibu,” alisema.
Kuelekea kwenye pambano hilo la
Osward na Kaseba, kumekuwa na tambo za aina yake kutoka kwa wawili hao, huku
kila mmoja akijigamba kumtandika mwenzake.
No comments:
Post a Comment