https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, March 03, 2013

Wacheza gofu waonyesha uwezo wao GYMKHANA

Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Mishack Ugulo, pichani.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANAMICHEZO mbalimbali wa mchezo wa gofu, jana walionyeshana uwezo katika mashindano yaliyodhaminiwa na benki ya BankABC, yakihudhuriwa pia na viongozi wa juu ya benki hiyo yenye matawi yake Dar es Salaam na Arusha.

Mashindano hayo yalivutia wachezaji wengi, wakiwamo wafanyabiashara na wateja wa BankABC, huku dhamira ikiwa ni kuendeleza juhudi za kuuweka mchezo wa gofu katika kiwango cha juu.

Akizungumza katika ufunguzi wa shindano hilo la siku moja katika Viwanja vya Gymkhana, yaliyoanza asuhubi hadi jioni, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya BankABC, Misheck Ugalo, alisema kuwa wameamua kudhamini shindano hilo ili kushiriki juhudi za kuuletea mafanikio mchezo huo.

Alisema benki yao ina haki ya kushiriki pamoja na wateja wao katika sekta ya michezo, ukiwamo gofu unaopendwa na watu wengi.

“Leo (jana) tumeamua kuwa na wateja wetu katika kudhamini gofu ambayo hakika ni mchezo mzuri unaohitaji umakini katika uchezaji wake.

“Shindano hili la siku moja nadhani litakuwa na tija hasa kama washiriki wote waliojiandikisha kushindana wataonyesha uwezo wao halisi,” alisema.

Benki ya BankABC sio mara yake ya kwanza kujiingiza kwenye michezo, hasa baada ya mwaka jana kudhamini michuano ya ‘BankABC SUP8R 2012.

.

Uchaguzi Mkuu Kenya 2013: Maandalizi yapamba moto


Na Dorine Otinga, Eldoret, Kenya
BILA shaka, zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa kihistoria nchini Kenya ambao utafanyika Machi, 4 mwaka huu ikishuhudiwa wagombea nane wakichuana kuwania nafasi ya urais. Maandalizi kati ya wakenya dhidi ya uchaguzi yanafanywa kwa udi na ambari. Wanasiasa wanajaribu kushindani kila siku kwa kumwaga sera za kuwezeshwa kupata kura.

Kama nilivyoelezea juma lililokwishapita juu ya kura za maoni ya wananchi wa Kenya wanaosadiki wagombea wao. Nikumbushe tu, wakenya 328 walioulizwa kwenye zoezi la kura za maoni juu ya uchaguzi walikuwa na mitazamo mbalimbali.

Watu 92% wamekubali kuwa mdahalo kwa njia ya runinga ulisaidia kujua mbinu na uwezo wa kujieleza wa wagombea wao. Wengine 24% walilazimika kubadili mawazo yao kwa ajili ya wagombea waliodhani watawachagua. 

Wapigakura hawa 34% ina maana wamebadili mawazo kutoka kwa mgombea mmoja kwenda kwa mwingine. Wakenya 27% wanadhani Uhuru Kenyatta atashinda uchaguzi.

Saturday, March 02, 2013

Tenga na TFF yake wapinga maagizo ya serikali


Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodgar Tenga, akizungumzia kupinga kwa maagizo ya serikali yaliyositisha matumizi ya Katiba ya mwaka 2012 na kutaka itumike ile ya mwaka 2006.

Benki ya BankABC yadhamini shindano la gofu GYMKHANA

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya BankABC, Misheck Ugalo, akizungumzia benki yao kudhamini shindano la mchezo wa gofu linaloendelea leo katika Viwanja vya GYMKHANA, jijini Dar es Salaam na kushirikisha wafanyabiashara mbalimbali.
Umeona kiwango?

Ngoja uone kazi leo....

Picha mbalimbali uzinduzi wa Victoria Sound, chini ya Mwinjuma Muumini jana

 
 
 
Hizi ni baadhi ya picha za matukio ya kuzindua bendi mpya ya muziki wa dansi ya Victoria Sound, chini ya Mwinjuma Muumini, uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni na kuhudhuriwa na watu kibao.

SEMINA KUHUSU TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO NA UTAWALA BORA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ISACA Tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu teknolojia ya mawasiliano na Utawala Bora vinavyoweza kuchangia maendeleo ya uchumi na kufanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na ISACA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Norway Registers Development. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya washiruiki wa Semina hiyo kutoka katika taasisi za Fedha
Rais wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ISACA tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akitoa mada katika semina hiyo.

MAMA SALMA KIKWETE AMSHUKURU DK. MIGIRO

Nakushukuru Dr Asha Rose Migiro kwa kuja kutembelea Shule yetu ya WAMANAKAYAMA na kututia moyo na kuunga mkono juhudi zetu za kuwahudumia waTanzania.
Vijana wa Kike kutoka kote Tanzania walioko ndani ya Shule yetu hii pia wamefarijika kufanya mazungumzo na wewe.
Karibu tena WAMANAKAYAMA.

"Nakushukuru Dr Asha Rose Migiro kwa kuja kutembelea Shule yetu ya WAMANAKAYAMA na kututia moyo na kuunga mkono juhudi zetu za kuwahudumia waTanzania.
Vijana wa Kike kutoka kote Tanzania walioko ndani ya Shule yetu hii pia wamefarijika kufanya mazungumzo na wewe.
Karibu tena WAMANAKAYAMA." - MAMA KIKWETE

Friday, March 01, 2013

TBL yakabidhi magodoro 210 na vyandarua 200 kwa Hospitali za Kiaseni na Huruma
Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa magodoro kwa mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako mara baada ya kukabidhiwa na kampuni ya Bia Tanzania TBL.katikati ni mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindi.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindi,(katikati)akimkabidhi kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahim Msengi  msaada wa magodoro kwa ajili ya hosptali ya Huruma ya wilayani Rombo pamoja na kituo cha Afya cha Uru Kiaseni ,kulia kwake ni mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako.  Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimetolewa na TBL kwa ajili ya kituo chaAfya cha Uru Kiaseni na hosptali ya Huruma .
Wakiwa katika picha ya pamoja na Waganga wa vituo hivyo.

Pambano la ngumi la kutisha kupigwa nchini Ghana, Machi 30


Wakali hawa, watachuana Machi 30, nchini Ghana, ambapo Albert Mensah atacheza na Ben Odamettey.

Mbwana Matumla asifia viwango cha Kaseba, Oswald

Mbwana Matumla akiwa ulingoni.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mbwana Matumla, amesema pambano la Japhet Kaseba na mpinzani wake Maneno Oswald, litakuwa zuri kutokana na umahiri wa wakali hao wa masumbwi hapa nchini.
Mabondia hao wanatarajia kuzipiga Machi mbili katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, jijini Dar es Salaam, huku mgeni rasmi akiwa ni Kamanda wa Polisi KanDA Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Matumla alisema Kaseba na Osward ni mabondia mahiri katika ngumi nchini, hivyo mpambano wao utakuwa wa aina yake.
Alisema kwamba anaamini mashabiki watapata kitu kizuri kutoka kwa mabondia hao, maana ni hodari wa kurusha masumbwi pamoja na uzoefu wa aina yake.
“Pambano la Kaseba na Oswald litakuwa la aina yake, maana ni mabondia mahiri na wenye uwezo mzuri, hivyo naamini upinzani utakuwapo kwa wawili hao ulingoni.
“Wamekuwa kwenye mvutano wa siku kadhaa tangu kutangazwa kwa pambano hilo, katika suala zima la masumbwi, lolote linaweza kutokea, hivyo tusubiri tupate majibu,” alisema.
Kuelekea kwenye pambano hilo la Osward na Kaseba, kumekuwa na tambo za aina yake kutoka kwa wawili hao, huku kila mmoja akijigamba kumtandika mwenzake.

Nyosh: Tuna aina nyingi za uchezaji

Nyosh El Sadaat
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa bendi ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, Nyosh El Sadaat, amesema kwamba wamebuni aina zaidi ya 300 ya uchezaji, ikiwa ni mikakati ya kuboresha zaidi burudani zao.
 
Nyosh aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, alipokuwa akizungumzia mikakati ya kuwaweka juu katika mwaka huu, huku akisema aina zaidi ya 300 wameandaa kwa ajili hiyo.
 
Akizungumza kwa kujiamini, Nyosh ambaye pia anajiita kama Rais wa Vijana, alisema kuwa aina hiyo ya uchezaji itaendeleza mazuri yao ya kuwapatia mashabiki wao.
 
Alisema anaamini kuwa kila anayebahatika kuona shoo yao, ataamini kuwa wao ni bora zaidi katika tasnia ya muziki wa dansi, huku wakijikita zaidi kutoa burudani kwa wapenzi wao.
 
“Wazee wa Ngwasuma ni bendi yenye mikakati kabambe kwa mwaka huu, hivyo naamini kwa aina hizi 300 za uchezaji katika shoo moja, zitatuweka juu zaidi.
 
“Naomba mashabi wetu waendelee kutuunga mkono maana tumepania na hatuwezi kurudi nyuma kamwe, hasa kwa kutunga nyimbo nzuri na jinsi ya kufanya shoo zenye ubora zaidi,” alisema.
 
Wazee wa Ngwasuma, wamekuwa wakijimaarisha zaidi kwa ufanyaji wao wa shoo, hasa kwa kitendo chao cha kushuja chini ya jukwaa na kuanza kuwaonyesha mashabiki wao mitindo yao mipya, kila baada ya wiki moja, hasa onyesho lao la kila Jumapili, linalofanyika New Msasani Club.

Wanawake 10 wapanda Mlima Kilimanjaro kuhamasisha usawa wa kijinsia

JUMLA ya wapanda mlima maarufu wanawake wapatao 10, kutoka nchi za Nepal, Afrika kusini na Tanzania wanatarajia kupanda mlima Kilimanjaro leo kupitia geti la Machame kwa lengo la kuhamasisha usawa wa jinsia.
 

Wakiwa wamewahi kufanikiwa kupanda mlima mrefu zaidi duniani, mlima wa Evarest, wanawake saba katika nchi ya Nepal wanaungana na wenzao watatu kutoka afrika akiwemo msanii maarufu wa Tamthilia ya Isidingo, Hlubi Mboya maarufu kwa jina la Nandipha.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wapandaji hao, Mkurugenzi wa shirika la chakula duniani nchini Tanzania (WFP), Richard Ragan amesema kuwa la la elimu, kutokana na mamba za mapema, kuolewa wakiwa wadogo pamoja na changamoto ya kukosa fedha za kumudu mahitaji yao na ndio maana wameamua kuwaunganisha katika kueneza elimu ya usawa na ukombozi wa mwanamke.

Waziri wa Kazi azindua Bodi Mpya ya NSSF

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii ya Jamii (NSSF),Ramadhani Dau akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya Shirika hilo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akizungumza wakati wakati wa uzinduzi wa bodi mpya Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Mwenyekiti UVCCM Taifa aanza ziara ya kichama mkoani Morogoro

Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema hivi karibubi, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Hamis Juma kuwasili kwenye ofisi hiyo, Februari 28, 2013 kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
Sadifa akipatiwa burudani ya shairi na mmoja wa waghani maarufu wa mashairi mkoani Morogoro.Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda
Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis Juma akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda wakati wa mkutano wa ndani kati ya Mwenyekiti huyo na wajumbe wa Baraza la Vijana mkoa wa Morogoro

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...