Pages

Pages

Wednesday, July 22, 2015

Mkutano wa kuimarisha ushirikiano wa Afrika wafanyika Visiwani Zanzibar

Vijana wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa ufunguzi wa mkutano huo kulia  Ali Hamad Suleiman na Rukaiya Rashid Kombo. uliofanyika katika ukumbi wac hoteli ya Zanzibar Beach Resorty Mazizini Zanzibar na kufunguliwa na Balozi Ali Ali Iddi kwa niaba ra Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
Viongozi wa meza kuu wakisimama wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliowashirikisha Marais Wastaaf, Viongozi wa Dini na Vijana kutona Nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resorty Mazizini Zanzibar.

Dkt John Magufuli achanja mbuga Shinyanga

Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsalimia kwa  furaha kubwa Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa kwa wananchi hao akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita mapema leo mchna alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Tuesday, July 21, 2015

Wanafunzi wawili walipiwa ada kwa malipo ya bima ya mama yao



Mratibu Mratibu wa Bima ya Elimu  kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, akizungumza na baadhi ya watumishi wa shule ya sekondari James Sangu (hawapo pichani ) juu ya namna ya kujiunga na fao hilo kabla ya kufanyika kwa zoezi la makabidhiano ya  hundi  kwa Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo  yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mama yake Anna Jelle kufariki Dunia. Picha zote Emanuel Madafa, Mbeya.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Financial Services, jana imewakabidhi wanafunzi wawili hundi ya Sh Milioni tatu, itakayowawezesha kila mwaka kupata Sh Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa ajili ya ada kwenye shule zao wanazosoma kutokana na malipo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao inayoendeshwa na taasisi hiyo.

Wanafunzi hao ni Jacqueline Ndyamkana wa shule ya sekondari ya James Sangu na Joceline Ndyamkana wa shule ya awali, huku malipo hayo yakitokana na bima ya mama yao aliyejulikana kwa jina la Anna Jelle, ambapo kwa kupewa kiasi hicho cha fedha kila mwaka, kutawafanya wasome bila usumbufu wowote katika kipindi hicho cha miaka mitatu mfululizo.
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura,akionyesha moja fomu maalumu zinazotumiwa na wateja wao katika hautua za awali wakati wa uombaji wa mkopo kupitia taasisi hiyo.
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, akitoa ufafanuzi kuhusiana changamoto mbalimbali zinazowakibili wateja wao na namna ambavyo walivyo weza kuhudumia wateja wao.

Alpha Akimu Meneja wa Kanda za Nyanda za juu Kusini akizungumza katika hafla hiyo.
Akizungumza jana wilayani Mbozi, mkoani Mbeya, Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Financial Sercices, Ruth Bura, alisema kwamba fedha hizo zinatoka kwa ajili ya kuwezesha watoto hao wawili.

Monday, July 20, 2015

Magufuli atikisa vilivyo jimboni kwake Chato

 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .
  Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.
  Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa  furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.
 Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo pichani.

Saturday, July 18, 2015

Washindi wanne wa Kopa Bayport wakabidhiwa fedha zao

 
Meneja wa Bayport Mkoani Lindi, Jovin Mapunda, kulia, akimkabidhi kiasi cha Shilingi Milioni moja mshindi wa Kopa Bayport, Said Mkinda, katika droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Fedha hizo alikabidhiwa juzi. Jovin Mapunda. Picha zote kwa hisani ya Bayport Financial Services.

Washindi wanne wa Kopa Bayport wakabidhiwa fedha zao
Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamWATEJA wanne wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, walioshinda Sh Milioni Moja kila mmoja katika bahati nasibu ya Kopa Bayport, wataisherehekea vizuri Sikukuu ya Eid el Fitr, baada ya kukabidhiwa fedha zao jana. Wateja hao ambao ni Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule (Kigoma), Phelis Nziku (Arusha) na Said Mkinda (Lindi), ambao washindi wote hawa walikabidhiwa fedha zao kwa kupitia Ofisi za Mkoa za Taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima.
 Mteja wa Bayport Phelis Nziku wa Arusha kushoto akikabidhiwa kiasi cha Sh Milioni moja baada ya kushinda bahati nasibu ya Kopa Bayport.

Akizungumzia hatua ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mauzo wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, alisema kwamba ni furaha yao kuona washindi wao wote wamepata haki zao kutokana na kushinda kwenye shindano la Kopa Bayport. 

Friday, July 17, 2015

Kambi Mbwana ajitosa Ubunge Handeni Vijijini

Mwandishi wa Habari za Michezo na mdau wa maendeleo ya wilaya ya Handeni, Kambi Mbwana, mwenye fulana ya CCM, akikabidhiwa fomu ya kuwania Ubunge, Jimbo la Handeni Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha Muya, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwa Mbwana ni Jerome Mhando, mmoja wa wadau waliomsindikiza katika tukio la uchukuaji fomu ya kuwania nafasi ya kuwatumikia wana Handeni. Picha na Mpiga Picha Wetu.

 Na Mwandishi Wetu, Handeni
MWANDISHI wa habari za michezo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga, amejitokeza rasmi katika mbio za kuwania ubunge jimbo la Handeni Vijijini kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Makabidhiano hayo ya fomu yalifanyika mbele ya Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha Muya, ikiwa ni siku chache baada ya milango ya uchukuaji fomu za kuwania nafasi za Ubunge na udiwani kufunguliwa rasmi. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mbwana alisema kwamba ameamua kujitokeza katika mbio hizo za ubunge ili afanyie kwa vitendo yale aliyokuwa anayapenda, hususan katika suala zima la maendeleo, huku wachache wao wakishindwa kuelewa faida ya harakati zake, zikiwapo zile za kuitangaza Handeni kwa njia mbalimbali.

Alisema wilaya yao imekuwa na changamoto kadhaa zinazohitaji nguvu za pamoja katika suala zima la shida ya kubwa ya maji, migogoro ya ardhi, ukosefu wa huduma bora za kijamii, hivyo kunahitajika jitihada na mipango ya pamoja kufanikishaji mambo hayo.
“Nilikuwa kimya kwa siku kadhaa nikiangalia akina nani wapo katika mchakato wa kuhitaji nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Handeni Vijijini na kusikitishwa na watu wasioishi huku na wasiokuwa na uchungu wala dhamira ya kuwakwamua wananchi wakijitokeza kwa wingi kuwania nafasi ya ubunge, inaonyesha wapo kwa maslahi yao zaidi.

“Hii haiwezi kukubalika, ukizingatia kwamba wananchi wameendelea kuishi maisha ya mashaka kwa kukosa maji safi, elimu, afya, michezo, utamaduni na mambo mengine yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa kushirikiana na watu wote, wakiwamo viongozi wa kisiasa, watendaji wa serikali na Watanzania kwa ujumla,” alisema Mbwana.


Licha ya kuonekana mpya katika ulingo wa kisiasa hususan kwa nafasi ya ubunge, Mbwana anakumbukwa na kushukuriwa na wengi kutokana na mradi wake wa Tamasha la Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka, kuasisi Taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, bila kusahau kuandika kitabu kinachojulikana kama Dira na Tumaini Jipya Handeni kilichopokewa kwa hisia tofauti, haswa kutokana na kilichoandikwa kwenye kitabu hicho.

Thursday, July 16, 2015

Kakore kugombea Ubunge Same Magharibi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
Mwandishi wa gazeti la DIMBA, Ahadi Kakore pichani, ametangaza kugombe Ubunge Jimbo la Same Magharibi, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Kakore alisema kuwa baada ya kujipima na kutafakari juu  ya matatizo yaliyopo kwenye Jimbo la Same Magharibi ameamua kuwania nafasi hiyo ili kupeleka mbele maendeleo yaliyokwama kwa miaka mingi.
“Nimetafakari kwa kina nikajipima nikaona kuwa wakati wa kuwatumikia Wanasame Magharibi umefika na kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji mtu makini na mwenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kulingana na matatizo waliyonayo.

“Naelewa Same tangu Uhuru tuna matatizo ya Barabara, Maji, Afya, Mazingira na Michezo mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa miaka mingi hivyo zinahitaji mtu makini na kijana ambaye anaweza kusaidia kuyatatua kwa haraka na wakati unaofaa,” alisema Kakore.


Alisema kuwa Jimbo la Same Magharibi ni miongoni mwa majimbo yenye matatizo mengi ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa wa Kilimanjaro jambo alilodai kuwa kwa wakati huu anahitaji mtu makini, anayefahamu matizo ya Wanasame lakini mwenye uwezo wa kuyashughulikia kwa uhakika.


Kakore ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo kazi ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka 15 ambapo alishafanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.
Jimbo la Same Magharibi kwa sasa linashikiliwa na David Mathayo David ambaye amekaa kwenye kiti hicho kwa miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa. Mionggoni mwa watu wa kwanza kuwa wabunge kwenye Jimbo hilo ni aliyewahi kuwa waziri katika katika serikali ya awali ya kwanza, Marehemu Chediel Mgonja. 

Mbio za Uchaguzi Mkuu, Mazala aingia Singida Mjini

fomu
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akionesha vijana fomu yake ya kuwania ubunge Jimbo la Singida Mjini jana kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoani Singida.

Na Hillary Shoo, Singida
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (MNEC) Manispaa ya Singida,Hassan Mazala amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Singida Mjini. Akizungumza na kundi la Vijana wa CCM kwenye ukumbi mdogo jana, Mazala amesema kuwa amefungua ukurasa mpya wa maisha yake kwa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mohammed Dewji aliyestaafu.

Watanzania kuendelea kuula viwanja vya Bayport Vikuruti

Meneja Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavula.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATANZANIA wenye nia ya kumiliki ardhi, wataendelea kuipata fursa hiyo baada ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kuwapatia nafasi wateja wao katika mradi huo ulioanza rasmi Mei 22 mwaka huu na kuzinduliwa katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na Meneja Biashara wa Taasisi hiyo, Thabit Mndeme, alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam, juu ya huduma hiyo ya viwanja vinavyotolewa kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.

Kwa mujibu wa Mndeme, wameamua kuendelea kutoa huduma hiyo ya viwanja katika eneo ya Vikuruti, baada ya kufanya tathmini kwa kuangalia umuhimu wa Watanzania kuweza kumiliki viwanja ili kujenga nyumba za kuishi, nyumba za biashara na mahitaji mengineyo wapendayo.
Mbali na huduma hiyo ya viwanja, Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa bila kusahau bima ya elimu kwa uwapendao, huku huduma zote hizo zikifanikisha maisha bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Tuesday, July 07, 2015

Bonanza la kukuza vipaji Kikwajuni, mchezaji bora kupewa ofa ya kusomeshwa kompyuta

Viongozi wa meza kuu wakifuatiliac mchezo huo kati ya Mwembeladu na Kisimajongoo katika Bonanza la kukuza vipaji kwa Vijana lililodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Masauni na kutoa ofa kwa mchezaji bora kupata fursa ya kusoma kozi ya kompyuta katika kituo cha Vija cha TAYI  

               Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Kisimajongoo.timu ya Muembeladu imeshinda mabao 4-1

Monday, July 06, 2015

Kwachaga stars kuiwinda Masharika Julai 13

Na Mwandishi Wetu, Handeni
TIMU ya Soka ya Kwachaga Stars, yenye maskani yake kijiji cha Kwachaga, wilayani Handeni, mkoani Tanga, inatarajia kuingia uwanjani Julai 13, katika Uwanja wa Magamba, kukwaana na wapinzani wao Masharika, ikiwa ni michuano ya kuwania Kombe la Ng’ombe, linaloendelea kutimua vumbi. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wilayani Handeni, inafanyika siku chache baada ya Kwachaga Stars kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Kideleko.
Akizungumza mwishoni mwa wiki wilayani Handeni, Nahodha  wa timu ya Kwachaga Stars, Zakaria Nambuje, alisema kwamba vijana wake wamejipanga imara kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono dhidi ya Masharika. Alisema wamejipanga imara kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri katika mashindano hayo ya kuwania Ng’ombe, ikiwa ni michuano yenye nguvu katika maeneo ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.
“Huu ni wakati mzuri wa kuwaandaa vijana wangu kwa ajili ya kuonyesha kiwango cha juu katika mashindano haya na mengineyo yatakayokuja. “Naamini kila tufanyalo kwa sasa ni kuifikiria mechi ijayo kwa sababu tunahitaji kufanya vyema na kuonyesha namna gani tumepania,” alisema.
Kwachaga ni miongoni mwa maeneo ya wilaya ya Handeni yenye vijana wengi wanaojua kucheza soka, jambo linalohitaji mipango kabambe kuhakikisha kwamba wanamichezo hao wanaendelezwaa ili waweze kupiga hatua.




SIWEZI KUVUMILIA: Hatuwezi kuendelea bila soka la vijana lenye dira

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), kwa kupitia Rais wake Jamal Malinzi, limesema halina makosa katika ufanyaji vibaya wa timu yake ya Taifa, akiaminisha kwamba wachezaji ndio wa kulaumiwa.

Malinzi aliyasema hayo siku alipotangaza kusitisha ajira kocha wake Mart Nooij, ambaye sasa nafasi yake imechukuliwa na kocha mzawa, Charles Boniface Mkwassa. Hata hivyo katika kuangalia mwenendo wa soka la Tanzania, ni wazi TFF inaweza kuingia kwenye makosa, maana bado haliweki mkazo katika soka la vijana, hususan maeneo ya mikoani.Huko kuna vijana wengi wenye vipaji vya kucheza soka. Hakuna juhudi za kuwaibua na kuwaendeleza. Tumeendelea kusubiri mashindano ya Diwani Cup ambayo mara kadhaa hufanyika wakati wa Uchaguzi Mkuu. Hapa ndipo nisipoweza kuvumilia. Hii ni kwa sababu tusipokuwa na mipango ya dhati, hatuwezi kusonga mbele. Kama TFF itawabana viongozi wa vyama vya soka vya mikoani na wilaya ili kuona namna bora ya kuwa na mashindano makubwa yenye tija, walau tutasonga mbele.

Lakini kuendelea kusubiria wachezaji kutoka Simba na Yanga ni kujisumbua, kwa sababu bado si wote wanaweza kupata nafasi katika timu hizo kongwe za Tanzania. Lazima tukubali kuwa mfumo wetu wa soka la Tanzania una tatizo kubwa, kwakuwa hakuna mbinu za kuibua vijana wazuri kwa maendeleo ya mpira wa miguu wa Tanzania.  Hatuwezi kupiga hatua. Tutaendelea kulalama kila siku, huku muda mwingi ukipotea na pengine kushuka chini zaidi na zaidi. Mkwassa si suluhisho la soka la Tanzania. Mwarobaini wa soka la Tanzania ni kuona wachezaji wengi vijana wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Kinyume cha hapo hakuna kitu. Tutatimua makocha kila siku. Matokeo yake hata wadau wanaosaidia soka, kama vile makampuni au hata mashabiki watachoka, kwakuwa huwezi kushabikia kitu kisichokupa furaha. Huo ndio ukweli wa mambo. Tunapaswa kuweka mipango na mikakati yenye tija kwa mustakabali wa soka la Tanzania. Kinyume cha hapo hakuna kitu.Tuonane wiki ijayo.
kambimbwana@yahoo.com
+255 712053949




Global Education Link yapongezwa na wazazi


Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel akiongea na Mwanafunzi ambae aliambatana na wazazi wake (kulia) kupata huduma ya vyuo vya nje ya nchi katika ofisi yao iliyopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Bw. Sourabh Chaudhary ambaye Meneja Miradi wa Chuo Kikuu cha Lovely cha nchini India na
Afisa Masoko wa GEL, Bi. Regina Lema. 
Picha zote na Cathbert Kajuna
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel akiongea na wanafunzi ambao waliambatana na wazazi wao (kulia) kupata huduma ya vyuo vya nje ya nchi katika ofisi yao iliyopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Saturday, July 04, 2015

Bayport Financial Services yafutulisha wadau wake, DC Klwa na Balozi wa Saudi Arabia wajumuikaamoja

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, kushoto, akitembelea katika ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services katika futuru iliyoandaliwa na taasisi hiyo. Pichani ni wadau wengine walioalikwa katika futari hiyo. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imefuturisha wadau wake wanaoendelea na mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, huku ikiwataka kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala wa Bayport Financial Services, Evelyine Hall, katika futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wadau wake mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Viongozi wa Taasisi ya Bayport Financial Services na wageni waalikwa wakijadiliana jambo katika futari ya Bayport iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mwenye koti jeusi na kofia ni Haruna Mbeyu, akifurahia jambo.
Akizungumza katika futari hiyo, Evelyine alisema ni vyema Watanzania wote, hususan Waislamu kuutumia vyema mwezi huo, ikiwa ni nguzo muhimu katika Dini ya Uislamu Tanzania na duniani kwa ujumla. Alisema Bayport inaheshimu misingi ya dini zote, hivyo kwakuwa mwezi wa Ramadhan ni sehemu ya ibada kwa Waislamu, vyema wakautumia vizuri, sanjari na kulinda Amani, upendo, umoja, mshikamano, bila kusahau jamii kuishi kwa kuheshimiana ili nchi yetu iweze kupiga hatua.

Friday, July 03, 2015

Washindi wanne waibuka na mamilioni ya Bayport, kila mmoja azoa Milioni moja kwenye shindano la Kopa na Bayport

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto, akiwa kwenye heka heka ya droo ya kutafutwa washindi wanne wa shindano la Kopa na Bayport linaloendeshwa na Taasisi hiyo. Aliyefungwa kitambaa usoni ni Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya kifedha nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATEJA wanne waliokopa kwenye Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wameibuka na ushindi wa Sh Milioni moja kila mmoja, ikiwa ni maboresho ya promosheni iliyoanzishwa mapema mwaka huu, ikimuwezesha mteja kushinda Sh Milioni moja endapo atakopa kwa njia ya mtandao.

Mtandao huo ni ule wa www.kopabayport.co.tz, ambapo sasa wateja wanne watatutafutwa kila mwezi mara baada ya kukopa Bayport Financial Services kwa njia ya mtandao, wakala au ofisi yoyote ya taasisi hiyo ya kifedha nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kila mmoja anaweza kushinda kiasi cha Sh Milioni moja, endapo atakopa mkopo kwa njia yoyote kutoka Bayport.
Meneja wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akichagua mmoja wa washindi katika droo ya Kopa na Bayport iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwani ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, wakati kulia ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya kifedha nchini.


Alisema awali bahati nasibu hiyo iliwahusu wateja watatu waliokopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz ambao bado unaendelea kutoa huduma, huku ikiboreshwa zaidi kwa kuchezesha droo ya kutafutwa washindi wanne badala ya watatu, ikiwahusu wateja wote waliokopa kwa kupitia mtandao, wakala au tawi lolote la Bayport nchini Tanzania.

Katibu wa CCM Mkoa Dar es Salaam afungua semina ya mabalozi

Mbunge wa Jimbo la Temeke na Kamanda wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu, akizungumza na mabalozi  wa mashina ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  Kata ya Vituka Jimbo lake, ambapo mgeni Rasmi wa semina ya mabalozi hao alikuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam  Abillahi Mihella.

Thursday, July 02, 2015

Bonanza la usiku wa Michezo Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdalla Bulembo wa kwanza kushoto Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni na Kada wa CCM Abass Bahari wakijiandaa kuelekea kukagua timu hizo wakati wa Bonaza hilo linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku kwa michezo miwi kila siku.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Muembeladu kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar, Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Rahaleo,kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar, Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar. 

Waziri wa Uwezeshaji Zanzibar atoa vifaa vya elimu Chuo cha Ualimu Raha Leo

Wanafunzi wa Skuli ya msingi Rahale wakimpokea Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar alipowasili katika viwanja vya Skuli hiyo kukabidhi Vifaa viliotolewa na Mwakilishi wa Rahaleo kwa Wananchi wa jimbo hilo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Rahaleo kuhudhuria hafla ya kukabidhi Vifaa kulia Mwakilishi wa Rahaleo na kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Rahaleo Ndg Daudi Amani Bakari
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo lake iliofanyika katika Skuli ya Msingi Rahaleo Zanzibar.

Wednesday, July 01, 2015

Angalia mwonekano wa ofisi ya Global Education viwanja vya sabasaba

Muonekano wa Ofisi ya Global Education Link iliyopo ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa Bonaza Kombe la Masauni Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Hamad Masauni akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Kikwajuni Bondeni iliolazimika kuchukua kipigo cha mabao 2--1 katika mchezo wa ufunguzi wa Bonaza hilo linalofanyika usiku katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, Mhe Hamad Masauni akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Kisimamajongoo iliotoa kipigo cha mabao 2--1 katika mchezo wa ufunguzi wa Bonanza hilo linalofanyika usiku katika viwanja vya Mnazi mmoja Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Hamad Masauni akizindua michuano ya Bonaza la Kombe la Masauni, yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku na kushirikisha timu mbalimbali za vijana ili kukuza vipaji vya mchezo huo Zanzibar.