Pages

Pages

Thursday, July 16, 2015

Kakore kugombea Ubunge Same Magharibi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
Mwandishi wa gazeti la DIMBA, Ahadi Kakore pichani, ametangaza kugombe Ubunge Jimbo la Same Magharibi, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Kakore alisema kuwa baada ya kujipima na kutafakari juu  ya matatizo yaliyopo kwenye Jimbo la Same Magharibi ameamua kuwania nafasi hiyo ili kupeleka mbele maendeleo yaliyokwama kwa miaka mingi.
“Nimetafakari kwa kina nikajipima nikaona kuwa wakati wa kuwatumikia Wanasame Magharibi umefika na kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji mtu makini na mwenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kulingana na matatizo waliyonayo.

“Naelewa Same tangu Uhuru tuna matatizo ya Barabara, Maji, Afya, Mazingira na Michezo mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa miaka mingi hivyo zinahitaji mtu makini na kijana ambaye anaweza kusaidia kuyatatua kwa haraka na wakati unaofaa,” alisema Kakore.


Alisema kuwa Jimbo la Same Magharibi ni miongoni mwa majimbo yenye matatizo mengi ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa wa Kilimanjaro jambo alilodai kuwa kwa wakati huu anahitaji mtu makini, anayefahamu matizo ya Wanasame lakini mwenye uwezo wa kuyashughulikia kwa uhakika.


Kakore ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo kazi ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka 15 ambapo alishafanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.
Jimbo la Same Magharibi kwa sasa linashikiliwa na David Mathayo David ambaye amekaa kwenye kiti hicho kwa miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa. Mionggoni mwa watu wa kwanza kuwa wabunge kwenye Jimbo hilo ni aliyewahi kuwa waziri katika katika serikali ya awali ya kwanza, Marehemu Chediel Mgonja. 

No comments:

Post a Comment