Pages

Pages

Saturday, July 18, 2015

Washindi wanne wa Kopa Bayport wakabidhiwa fedha zao

 
Meneja wa Bayport Mkoani Lindi, Jovin Mapunda, kulia, akimkabidhi kiasi cha Shilingi Milioni moja mshindi wa Kopa Bayport, Said Mkinda, katika droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Fedha hizo alikabidhiwa juzi. Jovin Mapunda. Picha zote kwa hisani ya Bayport Financial Services.

Washindi wanne wa Kopa Bayport wakabidhiwa fedha zao
Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamWATEJA wanne wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, walioshinda Sh Milioni Moja kila mmoja katika bahati nasibu ya Kopa Bayport, wataisherehekea vizuri Sikukuu ya Eid el Fitr, baada ya kukabidhiwa fedha zao jana. Wateja hao ambao ni Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule (Kigoma), Phelis Nziku (Arusha) na Said Mkinda (Lindi), ambao washindi wote hawa walikabidhiwa fedha zao kwa kupitia Ofisi za Mkoa za Taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima.
 Mteja wa Bayport Phelis Nziku wa Arusha kushoto akikabidhiwa kiasi cha Sh Milioni moja baada ya kushinda bahati nasibu ya Kopa Bayport.

Akizungumzia hatua ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mauzo wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, alisema kwamba ni furaha yao kuona washindi wao wote wamepata haki zao kutokana na kushinda kwenye shindano la Kopa Bayport. 

 Mteja wa Bayport akipewa fedha zake
Alisema wanaamini wateja hao wataendelea kufurahia huduma za Bayport zinazotoa picha halisi ya namna gani taasisi yao ina lengo la kuwakomboa na kuwakwamua pia kwa kutoa huduma bora kwa ajili ya maendeleo ya watanzania wote. “Kama tulivyotangaza hapo awali kwamba tulikuwa na washindi wanne waliokopa Bayport na kushinda Sh Milioni Moja kila mmoja, hivyo tumekabidhi kwa kupitia mameneja watu katika maeneo waliyoshinda wateja hawa.

“Tunawaomba wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kutuunga mkono ili tuwapatie huduma bora kama vile mikopo ya bidhaa, mikopo ya fedha taslimu bila kusahau Bima ya Elimu kwa Uwapendao, huku huduma ya ukopaji kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz ukiwarahishia wateja wetu kukopa kwa njia ya haraka popote walipokuwapo,” alisema Mgeta.

Kwa mujibu wa Mgeta, promosheni ya Kopa Bayport imeanzishwa kwa lengo la kuwashukuru wote wanaokopa kwenye taasisi yao, huku wahusika wakuu wakiwa ni wale wanaokopa kwenye taasisi yao inayoongoza kwa huduma bora za kifedha.

No comments:

Post a Comment