Pages

Pages

Thursday, July 02, 2015

Bonanza la usiku wa Michezo Viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdalla Bulembo wa kwanza kushoto Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni na Kada wa CCM Abass Bahari wakijiandaa kuelekea kukagua timu hizo wakati wa Bonaza hilo linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku kwa michezo miwi kila siku.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Muembeladu kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar, Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Rahaleo,kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar, Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar. 

Kikosi cha timu ya Muembeladu kinachoshiriki michezo ya Bonaza la Kombe la Masauni.
           Kikosi cha timu ya Rahaleo,kinachoshiriki michezo ya Bonaza la Kombe la Masauni.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe Abdalla Bulembo akizungumza na wanamichezo wakati wa mchezo wa Bonaza Kombe la Masauni na kuwataja vijana kukuza michezo ndio mafanikia yao kujipatia ajira, Michezo huleta amani na utulivu katika nchi. Na kuahidi timu itakayoshinda katika mchezo huo ataizawadia shilingi laki moja. kwa bahati mbaya timu hizo zimetoka sare na kukabidhiwa kila moja shilingi 50,000/- baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa sare ya 2--2  
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimiliki mpira huku mchezaji wa Rahaleo akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wa Bonaza Masauni Cup.

Wachezaji wa Rahaleo na Muembeladu wakiwania mpira katika mchezo wa Bonaza Masauni Cup linalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja usiku. 
                           Mchezaji wa timu ya Muembeladu akiondoa mpira.
Wapenzi wa mchezo wa soka Zanzibar wakifuatilia michezo ya Bonaza ya Kombe la Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni. Masauni Cup.Bonaza
                     Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Rahaleo.
Kocha wa timu ya Rahaleo akitowa maelekkezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao na timu ya Rahaleo uliofanyika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Kocha wa timu ya Muembeladu akitowa maelekkezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao na timu ya Rahaleo uliofanyika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya 2--2
                                                      Kizazaa golini kwa timu ya Rahaleo
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Rahaleo akiwa chini, wakati wa mchezo wao wa Bonaza Kombe la Masauni timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Golikipa wa timu ya Rahaleo Saleh Machupa akiokoa mpira golini kwake wakati wa mchezo wao Bonaza Kombe la Masauni inayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni ili kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar.

No comments:

Post a Comment