Pages

Pages

Friday, July 03, 2015

Washindi wanne waibuka na mamilioni ya Bayport, kila mmoja azoa Milioni moja kwenye shindano la Kopa na Bayport

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto, akiwa kwenye heka heka ya droo ya kutafutwa washindi wanne wa shindano la Kopa na Bayport linaloendeshwa na Taasisi hiyo. Aliyefungwa kitambaa usoni ni Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya kifedha nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATEJA wanne waliokopa kwenye Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wameibuka na ushindi wa Sh Milioni moja kila mmoja, ikiwa ni maboresho ya promosheni iliyoanzishwa mapema mwaka huu, ikimuwezesha mteja kushinda Sh Milioni moja endapo atakopa kwa njia ya mtandao.

Mtandao huo ni ule wa www.kopabayport.co.tz, ambapo sasa wateja wanne watatutafutwa kila mwezi mara baada ya kukopa Bayport Financial Services kwa njia ya mtandao, wakala au ofisi yoyote ya taasisi hiyo ya kifedha nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kila mmoja anaweza kushinda kiasi cha Sh Milioni moja, endapo atakopa mkopo kwa njia yoyote kutoka Bayport.
Meneja wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akichagua mmoja wa washindi katika droo ya Kopa na Bayport iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwani ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, wakati kulia ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya kifedha nchini.


Alisema awali bahati nasibu hiyo iliwahusu wateja watatu waliokopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz ambao bado unaendelea kutoa huduma, huku ikiboreshwa zaidi kwa kuchezesha droo ya kutafutwa washindi wanne badala ya watatu, ikiwahusu wateja wote waliokopa kwa kupitia mtandao, wakala au tawi lolote la Bayport nchini Tanzania.
“Lengo letu ni kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, hivyo naamini bahati nasibu hii ni kielelezo tosha cha kutuweka katika ramani nzuri, ukizingatia kuwa washindi wanne kila mmoja atashinda katika bahati nasibu hii itakayoendelea had mwezi wa nane.
 Zoezi la kuchezesha droo hiyo ya Kopa na Bayport likiendelea. Washindi wanne walijishindia Sh Milioni 1,000,000 kila mmoja.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto, akizungumza jambo kwenye heka heka ya droo ya kutafutwa washindi wanne wa shindano la Kopa na Bayport linaloendeshwa na Taasisi hiyo. Aliyefungwa kitambaa usoni ni Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya kifedha nchini.

Wateja walioshinda katika bahati nasibu yetu na maeneo watokayo kwenye mabano ni pamoja na Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule, (Kigoma), Said M Mkinda (Dar es Salaam) na Phelis Nziku ambapo wote kila mmoja watakabidhiwa kiasi hicho cha pesa kutoka Bayport Financial Services. Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo aliipongeza Bayport Financial Services kwa kuendelea kubuni mambo yanayoweza kuwapatia mwanga wateja na Watanzania kwa ujumla.

“Hii ni bahati nasibu nzuri na rahisi kuchezwa na kila mtu, maana haina vigezo zaidi ya mtu kuingia kwenye droo kama atakuwa amekopa tu, iwe kwenye mtandao wao au kufika katika tawi la ofisi yao yaliyoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara,” alisema Ngolo, huku akiwataka Watanzania kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali za Bayport. Huduma zinazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa mbalimbali kama vile vifaa vya ujenzi, bodaboda, injini ya boti, pembejeo za kilimo, zikiwa ni miongoni mwa huduma zinazorahisisha maisha kwa Watanzania wote.

No comments:

Post a Comment