Pages

Pages

Saturday, September 28, 2013

January Makamba aongoza mamia ya semina ya Kamata Fursa jijini Mwanza leo

 
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kusubiri Serikali iwafanyie ama iwaletee kila kitu hapo walipo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh Januari Makamba akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina, sambamba na fursa ya matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu, iliyofanyika leo, ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzetu,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada mbalimbali zilikuwa zikizungumzwa. 
  Mmoja wa wasanii wa bongofleva, Nikki Wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twendzetu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max Malipo, Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya Max Malipo inavyoweza kuisadia jamii kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi Washiriki wakifuatilia.
Mmoja wa waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael akijulikana zaidi kwa la kisanii kama Lulu akiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,ambapo pia atazungumzia mambo kadhaa mbalimbali kwenye semina hiyo,ambayo itawakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba, Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini na watoa mada wengine mbalimbali

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha alipokuwa akiwasili kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu, ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii.

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele (mwenye miwani) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Bi.Magreth Chacha walipokuwa wakiwasili kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu, ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,pichani kati ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group, Bwa.Ruge Mutahaba.

Baadhi ya Wakazi wa mji wa Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii. 
 Sehemu ya meza kuu.

No comments:

Post a Comment