Pages

Pages

Friday, September 27, 2013

JB sasa amshauri Lameck ajisalimishe Kanumba The Great, kampuni ya marehemu Kanumba



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI wa filamu hapa nchini, Jacob Stephen, maarufu kama JB, amemshauri Lameck Chalres Kanumba, anayejiita ni ndugu wa marehemu Kanumba kufanya mazungumzo na ndugu zake sanjari na kupewa nafasi katika Kampuni Kanumba The Great.
Msanii mahiri wa filamu Tanzania, JB pichani.
JB aliyasema hayo siku chache baada ya kuona Lameck naye ameonyesha nia ya kuingia katika soko la filamu na kufuata nyayo za marehemu Kanumba aliyefanikiwa kuwa na jina kubwa kabla ya kufariki Dunia na kuacha pigo kwa wapenzi wa sanaa nchini.
Lameck Charles Kanumba, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema si vyema Lameck akaanza kuhangika katika kampuni nyingine wakati kaka yake ameacha kampuni ya filamu.
Marehemu Steven Charled Kanumba, pichani enzi za uhai wake.
Alisema ni vyema msanii huyo akakutana na familia yake na wale walioachiwa kampuni hiyo ili ikiwezekana wafanye kazi kwa pamoja badala ya kuzunguuka kwa watu wengine.

“Nimekuwa nikimuona Lameck anayesema ni ndugu wa Kanumba katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii akizungumzia kipaji chake na jinsi alivyozaliwa katika familia moja na Kanumba.

“Pamoja na yote hayo, sioni sababu ya Lameck kuzunguuka kwenye kampuni za watu wengine na badala yake ipo kampuni ya Kanumba nab ado inaendelea na shughuli ya uzalishaji wa filamu,” alisema JB.

Kwa mujibu wa JB, Lameck ingekuwa rahisi sana kupata nafasi katika kampuni ya Kanumba the Great hasa kama kweli naye ni ndugu wa marehemu Kanumba kama anavyodai mwenyewe.

No comments:

Post a Comment