Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho
la Soka nchini (TFF), Michael Wambura, amepokea kwa furaha kuitwa kwenye Kamati
ya Mpango Mkakati ya klabu ya Simba, huku akisema kuwa hana ugomvi wala mgogoro
na klabu ya Simba.
Michael Richard Wambura
Mbali na Wambura, uteuzi huo pia umewahusisha watu
mbalimbali, akiwamo Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group,
Ruge Mutahaba, ambao wote kwa pamoja wameingizwa kwa ajili ya kufanya juhudi za
kuipatia maendeleo klabu hiyo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Wambura alisema kuwa
amepokea kwa furaha uteuzi huo kwasababu hana mgogoro na wanachama wala
viongozi wa klabu ya Simba, hivyo yupo tayari kutoa ushirikiano wake wakati wowote
unapohitajika.
Alisema kuwa klabu ya Simba inahitaji mipango na
uendelezaji, hivyo kitendo cha kuundwa kwa Kamati hiyo ni sehemu ya kuikomboa
Simba ambayo kwa sasa inakabiriwa na changamoto za aina yake.
“Nashukuru kwa viongozi wa Simba kuona kuwa nafaa kuwapo
kwenye kamati hiyo mpya ambayo naamini kwa pamoja tutafanya kazi kwa
ushirikiano kwa ajili ya maendeleo ya klabu kwa ujumla.
“Sina mgogoro na mtu yoyote kwenye suala la michezo hususan
mpira wa miguu, hivyo kwa sasa akili yangu yote ni kujaribu kutoa mawazo mazuri
kwa ajili ya maendeleo ya soka Tanzania,” alisema Wambura.
Joseph Itang’are, Swedy Mkwabi, Francis Waya, Ramesh Patel, Evance Aveva,
Mulamu Ng’hambi, Salim Mhene, Mtemi Ramadhani, Moses Basena, Henry Tandau,
Omary Gumbo, Michael Wambura, Glory Nghayomah, Crensencius Magori, Honest Njau,
Ruge Mutahaba, Evodius Mtawala na Dr
Mwafyenga.
No comments:
Post a Comment