Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa
nchini, Mbwana Matumla, amesema mchezo wa ngumi unakwenda kwa kusua sua
kutokana na ukosefu wa watu wenye mapenzi kiasi cha kuandaa mapambano
mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mbwana Matumla, Bondia wa Tanzania
Tangu alivyopigana na Mkenya
David Chalanga mwishoni mwa mwaka jana, Matumla hajapata pambano lolote licha ya
kuwa na uwezo wa juu katika tasnia ya masumbwi nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Matumla alisema ni wakati wa watu wenye uwezo na
mapenzi kuandaa mapambano ili kukuza mchezo wa ngumi hapa nchini.
Alisema bila hivyo mchezo wa
ngumi utakuwa kwa kusua sua maana wenye makali yao wanashindwa kuyaonyesha
kutokana na kukosa watu wa kuingia nao ulingoni.
“Napenda mchezo wa ngumi na ni
sehemu ya maisha yangu, ila Tanzania tuna uhaha wa mapromota, hivyo ni jukumu
lao sasa kuhakikisha kuwa wanaingia na kuwekeza kwa kupitia mchezo huu.
“Ngumi ni moja ya vitu vyenye
mguso wa aina yake, maana watu wanapenda kuucheza na hata mashabiki wanaingia
kwa wingi kunapokuwa na mapambano ya mabondia mbalimbali,” alisema Matumla.
Matumla ni miongoni mwa
mabondia wanaofanya vizuri katika mchezo wa masumbwi, huku akinolewa na mkongwe
Hamis Kinyogoli aliyewahi kuwika pia katika mchezo huo ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment