Juu kabisa msanii Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C akiwa katika pozi.
Juma Nature akiwa jukwaani. Msanii kama huyu anatakiwa awe makini ili aweze kufikia malengo ya kuwa nyota kama wengine wanavyowika duniani.
NIMEKUWA makini mno kufuatilia maisha ya wasanii wetu nchini
na kujua mambo mengi yanayowahusu kila uchwao. Nafanya hivi maana ni mdau na
mwenye kupenda zaidi kazi zao kila siku ya Mungu.
Katika hilo , mengi nimeyaona
na kuyaacha kama yalivyo. Najua kabla ya
kuyaacha yapite, huwa kwenye wakati mgumu kusumbua akili yangu nikitaka wafanye
lile na kuaacha hili, hata hivyo mwisho wa siku wao ndio wahusika wakuu.
Hata hivyo katika hili siwezi kuliacha mara baada ya
kuling’amua siku chache baada ya kumaliza uchunguzi wangu kwa wasanii
mbalimbali hasa wa muziki wa Bongo Fleva, wanaotamba kwa muda zaidi ya bigijii.
Huo ndio ukweli, maana ni makosa na yanatakuwa yafanyiwe
kazi kwa faida yao ,
ukizingatia kuwa supu inanywewa ikiwa ya moto. Sasa naanza. Wasanii wa Bongo
fleva wana kasumba kuwa boashara wanayoweza kuifanya ni kuuza nguo.
Yani mara baada ya kupata kajina kadogo, hutafuta flemu ya
duka na kufungua sehemu ya kuuza nguo. Ni biashara nzuri pia, ila inaishia hapo
hapo au nini malengo yao ?
Hivi biashara ni kuuza nguo peke yao ?
Mbona biashara ni nyingi mno zinazoweza kufanywa na vijana
hao wanaona sanaa ndio maisha yao na hawawezi
kuishi bila kuwa kwenye kundi hilo ?
Hapa lazima tufanye jambo.
Ni wasanii wengi wanaofanya kazi hiyo japo kuwa maduka hayo
hufa maara baada ya wao kupotea katika ramani ya sanaa, hivyo kuonyesha kuwa
hawakuwa na malengo ya aina yoyote katika kufungua biashara hiyo, zaidi ya
kupoteza muda.
Sitaki nionekane tofauti hapo, maana haya ni mawazo yangu
nikitaka wasanii hao wafike mbali zaidi kuliko kupoteza muda wao. Kwa bahati
mbaya aina yao
ya sanaa ni ya siku tatu na kupotea kabisa.
Maisha yao
huwa magumu mno wanapofilisika kisanaa hivyo kusumbua ndugu na marafiki zao,
wakitaka wapewe msaada kimaisha. Ni wengi japo kuwa ni ngumu kuwataja maana
hawakawii kupayuka wakisema wameharibiwa majina yao .
Hapa hakuna kufichana, japo kuwa tunaheshimiana, ukizingatia
kuwa nia ni kuwafanya wasanii hao wafike mbali zaidi. Ipo haja ya wasanii hao
kukaa chini na kuangalia biashara za kufanya, ikiwamo zile zenye tofauti na
mavazi.
Nasema hivyo kwasababu biashara zipo nyingi kama wamejipanga
na kuumiza vichwa vyao kwa ajili ya
maisha yao .
Angalia msanii Judithi Wambura maarufu kama
Lady Jay D. Huyu ni msanii aliyefika mbali zaidi kibiashara.
Ameweza kufungua vitega uchumi vyake zaidi ya vitatu na
kumuingizia kipato kikubwa. Nzuri zaidi, bendi yake nayo inaendelea kufanya
vema na kulinda jina la heshima yake. Labda ni kwasababu Jay D yupo na mtu
makini, Gadna G Habash.
Habash aliweza kuacha kazi yake ya utangazaji Clouds FM kwa
nia ya kuambatana na mke wake huyo mwenye uwezo mkubwa kisanaa. Sawa, ila
nadhani hata mwanadada huyo pia anashaulika, kitu kinachompatia maendeleo.
Vipi hawa wengine? Je, hawana watu wa kuwaongoza kwa faida yao ? Jibu wapo wengi tu,
ila mawazo yao
nahisi ni ya kupelekena katika majumba ya starehe wakikata kilaji kwa raha zao,
maana wanasema maisha yenyewe kimini.
Haya ni mawazo mgando. Nasema hivyo maana pesa inayotoka
bila kuingia kamwe haiwezi kukaa muda mrefu. Nadhani huu ni wakati wa wasanii
hao kukaa na kuangalia aina yao ya maisha kwa
faida yao
wenyewe.
Napenda kuona wasanii hao wakipiga hatua kubwa kimaisha,
maana majina yao ni tofauti na maisha yao baada ya muda
mchache. Kwanini kila msanii aone biashara ni ya kuuza nguo. Tena duka moja,
lililozunguukwa na mangine?
Huo ni upungufu mkubwa. Jina la Ahmad Ally Madee ni kubwa
ndio, ila linaweza kumuingizia fedha nyingi kwa kubuni biashara yenye tija. Wapo
wengi, ila sidhani kama inaweza kuwa chachu yao
ya kupiga hatua na kuishi maisha mazuri, kama watafungua vijibiashara vya
kupoteza muda, kama wanavyofanya sasa.
Wakati ndio huu. Kaeni chini muangalie aina yenu ya maisha.
Uvivu wa kufikiria usiwafanye mfe maskini, hali ya kuwa mngekuwa matajiri hata kama kuna kasumba ya kuibiwa kazi zenu, maana hao
mnaowata wadosi hawawezi kuingia hadi kwenye biashara zenu.
Zindukeni kwa faida yenu wenyewe.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment