Pages

Pages

Tuesday, March 08, 2016

Bagamoyo wapokea vizuri mradi wa viwanja vya Bayport


Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, akizungumza na waandishi wa Habari walipotembelea mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na taasisi yao, katika eneo la Kimara Ng'ombe, Bagamoyo, mkoani Pwani jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu, Bagamoyo

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
WAKAZI na wananchi wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, wamepokea vizuri mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wakisema kuwa mradi huo utachangia kwa kiasi kikubwa kuupanua na kuuweka mji wao katika kiwango cha juu kimaendeleo.

Meneja wa Bayport Financial Services wilayani Bagamoyo Francis Ndunguru akionyesha alama za viwanja vilivyopimwa katika eneo la mradi wa Kimara Ng'ombe, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinauzwa kwa mkopo kwa watu wote wenye kuhitaji kumiliki ardhi.

Kwa mjini Bagamoyo, mradi huo wa viwanja vya Bayport unapatikana Kimara NG’ombe, huku maeneo mengine ya nchi viwanja hivyo vikipatikana KIbaha, Chalinze, Morogoro, Kilwa na KIgamboni, vikihusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.
Meneja akionyesha barabara zilivyochongwa kuonyesha ubora wa mradi huo wa Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akizungumza na mtandao huu, mkazi wa Bagamoyo, Said Juma, alisema kwamba huduma za viwanja vya Bayport vinavyopatikana kwa fedha taslimu na mikopo si vya kukosa, kwa sababu zitachangia kuuweka mji wa Bagamoyo kwenye kiwango cha juu pamoja na kujibu malalamiko ya wananchi kushindwa kumiliki viwanja kwa njia rahisi na isiyokuwa na gharama kubwa.
Mwandishi wa habari Phillip Daud, akimhoji mwananchi wa Bagamoyo, Mwanaisha Khalfany juu ya ubora wa viwanja hivyo na uwezekano wa Watanzania hususan wakazi wa Bagamoyo kuvichangakia viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati.

“Uwezekano wa kumiliki viwanja Bagamoyo mjini ni mgumu kwa sababu vinauzwa bei ghari, hivyo kwa Bayport kuanzisha huduma hizi kwa watu wote bila kusahau sisi wajasiriamali, hakika ni jambo la kushukuru na kuwapongeza kwa mawazo yao mazuri yenye kutuendeleza sisi wananchi na wateja wao,” alisema Juma na kuwataka watu wa Bagamoyo na Watanzania wote kuchangamkia fursa hizo.
Mwananchi mwingine aliyekutwa kwenye mradi huo, Bi Mwanaisha Khalfany Sultan, alisema kwa kuanzisha mradi huo wa viwanja mji wao wa Bagamoyo utapanuka na kuongeza idadi ya watu wilayani humo.

“Tunafurahia kwa kiasi kikubwa mno kupata mradi huu wa mikopo ya viwanja vya Bayport tukiamini mji wetu utapiga hatua kubwa, hivyo tunawaomba kila mwenye uwezo wake na hitaji la kujenga achangamkie fursa hii muhimu kwa Watanzania wote, ukizingatia kuwa rasilimali ya ardhi ni muhimu na imekuwa ikiongezeka thamani kwa haraka nchini kote, huku katika eneo la mradi wa Kimara Ng’ombe mahitaji ya maji, umeme na barabara yakipatikana kwa urahisi,” alisema Mwanaisha.

Naye mwananchi Patrick Mwilongo, aligusia ubora wa mradi wa viwanja vya Kimara Ng’ombe akisema kuwa utakuwa umejibu swali na malalamiko ya wanasiasa waliokuwa hawataki Bagamoyo iingie kwenye Mamlaka ya Mji mdogo kwa madai kuwa mji utakuwa mdogo, ukizingatia kuwa endapo eneo hilo litajengwa mji huo utakuwa mkubwa na utapiga hatua kubwa kimaendeleo.

“Ni miongoni mwa wadau muhimu wa hapa Bagamoyo ambao hakika tumeendelea kuthamani mradi huu kwa sababu utakuwa na tija kwetu sote, hivyo ni wazi tunapaswa kujitokeza kupata viwanja hivi ili tujenge kwa sababu uwezo wa kununua kiwanja kwa fedha taslimu kwa baadhi yetu ni mgumu, ukizingatia kwa masharti nafuu unaweza kupata kiwanja kwa kukopeshwa na Bayport.


Naye Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, alisema kwamba lengo ni kusudio lao kuu kuona mji wa Bagamoyo unakuwa na wananchi wanamiliki viwanja hivyo kwa utaratibu rahisi, hivyo ni budi kutembelea kwenye tawi lao la MJini Bagamoyo pamoja na matawi yote Tanzania ili kupata viwanja hivyo kwa ajili ya kuweka makazi ya kifamilia, kibiashara na mengineyo.

“Tunawaomba Watanzania wote popote walipo kutembelea ofisi zetu au mawakala wetu walionea nchi nzima ili wapate fursa ya kukopa viwanja hivi kwa mji wa Bagamoyo au vilivyopo kwenye maeneo mengine ya Tanzania, tukiamini Bayport imeendelea kuwa mkombozi wa watu wote kwa kumiliki kiwanja kwa utaratibu rahisi,” alisema Ndunguru, Meneja wa Bayport Bagamoyo.

Mita Moja ya mraba kwa viwanja vya Bagamoyo inapatikana kwa Sh 10,000, Kigamboni (Tundi Songani) Sh 10,000, Kibaha (Boko Timiza) Sh 9000, Kilwa (Msakasa) Sh 2000, Morogoro (Kiegea B) Sh 3500, Chalinze (Kibiki na Mpera) Sh 4500 tu, huku utaratibu wa kuweza kupata viwanja hivyo ukiwa rahisi kwa Watanzania wote, wakiwamo waaajiriwa wa serikali, waajiriwa binafsi na wajasiriamali.

No comments:

Post a Comment