Pages

Pages

Friday, March 25, 2016

Patashika ya mbio za uspika Visiwani Zanzibar zaanza rasmi

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
HEKAHEKA zimeanza Visiwani Zanzibar ambapo wagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Wawakilishi wameanza kupigana vikumbo kuwania nafasi hiyo huku sura mpya za vijana wenye damu mbichi zikijitokeza kuchuana na mkongwe aliyechukua tena fomu ya kutetea nafasi yake Mhe Pandu Ameri Kificho, pichani.

Kificho ni Spika wa Bunge la Wawakilishi kwa muda wamiaka 25 sasa ambapo wanachama wa CCM Zanzibar tayari wameanza kutilia mashaka uamuazi wa spika huyo aliyechukua fomu za kugombea tena akitaka kuendelea na kuongoza kiti cha uspika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, jambo, inalozua maswali mengi yasiyo na majibu.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar, walitoa maoni yao juu ya sakata hilo na kusema kuwa Kificho hakustaili kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kijacho bali alitakiwa kuiga mfano wa baadhi ya viogozi kama Spika Pius Msekwa na wengine walioamua kuachia ngazi kwa kujiuzuru madaraka na kuwaachia vijana wenye hali ya kuongoza ili kupata radha mpya katika Bunge hilo la Wawakilishi.

Naye mgombea, Mahamud Muhamed Mussa, alisema kuwa amejitokeza kuchukua fomu ili kuwania nafasi hiyo kutokana na uwezo alionao na Zaidi akijiandaa kuongoza kisasa Zaidi na kuleta mabadiliko ili Bunge la Wawakilishi liwe lakisasa na kuendana na kaulimbiu ya Mhe Rais wa Jamhuri ya 'Hapa kazi tu', alisemaMussa. 

''Kiukweli Kificho sasa anaelekea kuwaudhi Vijana ambao nao sasa ni muda wao wa kuongoza ili waweze kuchangia mengi waliyonayo ili kuendana na Kasi ya Rais wa awamu ya tano Mhe Dkt. Magufuli, Kificho amekalia kiti cha Spika Bunge la Wawakilishi kwa muda wa miaka 25 sasa ni kwa nini asipumzike na kuwaachia vijana wafanye kazi, sidhani kama bado ana jipya'', alisema Mwanachama mmoja wa CCM aliyejitambulisha kwa jina la Kijeshi.

Aidha Wanachama hao walikwenda mbali Zaidi kwa kukumbushia wakati wa zoezi la Kura ya maoni kuhusu Serikali mbili,ambapo Mhe. Kificho alionekana kwenda kinyume na msimamo wa Chama chake wa Serikali mbili huku yeye akionyesha msimamo wake Zaidi wa kudai Serikali tatu akidai 'eti' ni msimamo wa Baraza la Wawakilishi.

Waliojitokeza kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa, Zuberi Ali Maulid, Muhamde Ali Amhed, Jajh Janeth, Sadifa Juma, David Mwakanjuki, Perera Silmg na Abdallah Wazisi, ambapo mchuano mkali unaonekana kuwa kwa ni kati ya Spika aliyemaliza muda wake akijaribu kutetea kiti chake, Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa na Jaji Janeth Sekihola.

Wagombea wote walifika kuchukua fomu jana Machi 23,2016  na kurejesha jana hiyo hiyo, zoezi la kupitiamajina na kufanya mchujo na kupata majina matatu lilifanyika jana na kuwapata hao wanaochuana.

No comments:

Post a Comment