Pages

Pages

Wednesday, March 16, 2016

Makala: Bayport yapanua wigo wa mikopo ya viwanja katika maeneo sita mapya


*Kibaha, Bagamoyo, Kigamboni, Kilwa, Morogoro na Chalinze waula
*Kila mtu sasa anaweza kumiliki nyumba

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
LICHA ya kuwa na changamoto mbalimbali za kimaisha, lakini suala zima la umiliki wa nyumba na rasilimali muhimu ya viwanja imezidi kuwa rahisi. Ndio, maana uwapo wa taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, inawapatia mwanga wananchi wa Tanzania juu ya adhma ya kumiliki ardhi na viwanja kwa ujumla.
Bayport taasisi inayojihusisha na mikopo ya fedha na bidhaa, mwaka jana mwezi wa tano ilizindua huduma yamikopo ya viwanja katika mradi wake wa Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, (kulia) akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja vinavyotolewa na Taasisi hiyo nchini.


Katika mazungumzo na Mtandao huu, Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, anasema taasisi yao imepanua wigo wa kibiashara kwa kuanzisha miradi sita mipya ya viwanja katika maeneo ya Kibaha, Chalinze, Temeke, Kilwa, Morogoro na Bagamoyo baada ya kuuzindua Februari 22, katika Hoteli ya Ramada Encore, huku wageni waalikwa wakiwa ni Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, Msaidizi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bertha Minga na wadau wengine wa ardhi nchini Tanzania.

Mradi umezingatia suala la mipango miji, maji na umeme ambavyo ni vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu. Aidha Mbaga anasema ni kusudio lao kuu kutoa huduma bora kwa wateja na Watanzania ili maisha yawe mazuri kwa kufanikisha suala la makazi. Awali tulianza na huduma ya mikopo ya viwanja katikamradi wa Vikuruti, ambao ulihusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali pamoja na walionunua viwanja vyetu kwa pesa taslimu na kuufanya mradi wetu uende vizuri na ndio maana tumepanua huduma hizi za viwanja.

"Tumezindua huduma ya viwanja katika mji wa Bagamoyo eneo la Kimara Ng'ombe vitakavyouzwa Sh 10,000 kwa mita moja za mraba, ikiwa ni Kilomita 6.5 kutoka Bagamoyo Mjini, huku umeme ukipatikana kwa umbali wa kilomita 1.5 tu bila kusahau maji, alisema Mbaga na kuwataka Watanzania wote waiunge mkono taasisi yao katika mahitaji ya mikopo ya fedha taslimu, viwanja na huduma nyingine muhimu.

Naye Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, anasema huduma za viwanja zinapatikana (Boko Timiza) Kibaha, ambapo mita moja za mraba itauzwa kwa Sh 9,000 tu, huku wilayani Temeke ni (Tundwi Songani) ambapo mita moja za mraba itauzwa kwa Sh 10,000 tu na wilayani Chalinze viwanja vyao vipo Kibiki na Mpera na vitauzwa Sh 4,500.\r\n\r\nKwa mujibu wa Mndeme, miradi yote imezingatia urahisi wa upatikanaji wa rasilimali hiyo pamoja na uwezekano mkubwa wa kuboresha maisha ya Watanzania wote. Meneja Biashara huyo anasema njia za kupata huduma hizo ni pamoja na ununuaji wa kiwanja kwa pesa taslimu ambapo mteja anatakiwa kulipia fedha zote za kiwanja kwenye akaunti ya Bayport na kukabidhi nakala za nyaraka za malipo hayo kwenye ofisi za Bayport na kutakiwa asubiri ndani ya siku 90 kwa ajili ya kukabidhiwa hati ya kiwanja atakapokamilisha malipo yote.

Kwa wateja wa mkopo wa upande wa ujasiriamali na watumishi wa kampuni binafsi, wanatakiwa kulipia malipo ya awali ya mita za mraba walizochagua, huku Bayport ikikamilisha malipo yaliyosalia na wateja hao kupatiwa nyaraka watakapokamilisha malipo ya mkopo wao na thamani ya kiwanja inaanzia Sh 550,000 tu, huku gharama za awali zikiwa ni Sh 150,000 kwa kiwanja kisichozidi Mita 200 za mraba.

Watumishi wa umma hawana gharama za awali, badala yake watachagua kiwanja watakacho na watapigiwa hesabu za ulipaji mkopo huo kwa mwezi, huku makato yakiwa ni madogo ili kufanikisha dhamira ya kuwapatia fursa wananchi wote.

Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, anasema baada ya mradi wa Vikuruti kuungwa mkono na Watanzania wengi, wanapiga hatua kubwa zaidi kwa kuanzisha miradi hiyo mipya.

"Sasa kwa kupitia Bayport kujenga ni rahisi kuliko kitu chochote kwa kuwa anaweza kukopeshwa kiwanja na akalipa kidogo kidogo kulingana na kipato chake,hivyo utagundua maisha yatakuwa rahisi na mazuri.

"Bayport tunasema akiba haiozi kwa kujipatia ofa zetu za viwanja vyenye hati na pia anaweza kuendelea na huduma zetu nyingi za mikopo ya fedha kwa ajili ya kufanikisha dhamira zake za kujikwamua kiuchumi,alisema Cheyo.

Anasema kwamba taasisi yao inatanua wigo wa kibiashara kwa watu wote kama vile watumishi wa umma, watumishi wa kampuni binafsi, bila kusahau kundi kubwa la wajasiriamali linaloendelea kujumuishwa kwenye miradi ya viwanja na kuwa mkombozi kwa wengi.

Cheyo anasema malipo yote ya awali na yale ya viwanja yapanaswa kulipwa kwenye akaunti ya Bayport iliyopo benki ya NMB na kuorodhesha nakala kadhaa zinazohitajika kama vile hati halisi ya mishahara za miezi mitatu ya hivi karibuni, nakala ya kitambulisho cha kazi kwa watumishi wa umma, nakala ya kadi ya benki, taarifa za kibenki za miezi sita, kujaza fomu ya kuomba kiwanja, kujaza fomu ya kuomba mkopo wa kiwanja bila kusahau picha 8 za passport size, huku masharti kama hayo yakiendelea isipokuwa kwa mjasiriamali tu hatapaswa kuwa na kitambulisho cha kazi.

Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile aliwapongeza Bayport kwa kuanzisha firsa za viwanja katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, hususan jimboni lake la Kigamboni, huku ofisi ya Mkuu wa wilaya Temeke kwa kupitia msaidizi wa Mkuu wa wilaya, Bertha Minga, ikiwataka Bayport kuendelea kuifanikisha huduma hizo sanjari na kushirikiana na serikali ili wananchi wengi wapate viwanja hivyo kwa utaratibu rahisi na gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment