Pages

Pages

Thursday, February 25, 2016

Benki ya Amana yazindua tawi lake Mbagala

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya Amana, wakati alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Tawi hilo lililofunguliwa leo Feb 25, 2016 Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki hiyo, Dkt. Muhsin Salim Masoud (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Al- Nahdi. Picha na Sufianimafoto Blog
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, akisoma hotuba yake ya uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Amana lililofunguliwa Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Kijaji alimwakilisha Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwenye uzinduzi huo.

Monday, February 22, 2016

Bayport yazindua miradi sita ya mikopo ya viwanja, serikali yapongeza

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja vinavyotolewa na taasisi yao katika maeneo sita ambayo ni Kilwa, Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Morogoro. Kulia kwake ni Zahra Moore kutoka kwenye kampuni yao ya BlackWood na Mwanasheria wao Ntiiba Muganga. Picha na Story kwa Hisani ya Bayport Financial Services.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, imezindua miradi sita mipya ya mikopo ya viwanja katika maeneo ya Kibaha, Bagamoyo, Chalinze, Temeke, Kilwa na Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa utoaji huduma bora za viwanja baada ya ule wa Vikuruti kuungwa mkono Watanzania wengi.

Kuzinduliwa kwa huduma hizo mpya za viwanja huku wakiongozwa na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Bertha Minga, kunatanua wigo wa urahisishaji wa maisha ya Watanzania, hususan katika suala la ardhi linalozidi kupanda thamani siku hadi siku, jambo linalohitaji juhudi za taasisi kama Bayport za kuwasaidia wananchi wake kupata maeneo ya makazi kwa utaratibu rahisi na nafuu.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Bertha Minga, aliyesimama akizungumza katika uzinduzi wa hudumaya viwanja inayotolewa na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, leo mchana katika Ukumbi wa Ramada Encore, Posta, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwanasheria wa Kampuni ya BlackWood, Ntiiba Muganga na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa BlackWood Zahra Moore.

Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo mipya ya viwanja, Mkurugenzi Mkuu Bayport Financial Services, John Mbaha, alisema huduma zao zitakuwa na njia rahisi kwa ajili ya

Saturday, February 20, 2016

Ni hatari, Yanga yaitandika Simba bao 2-0 Uwanja wa Taifa leo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MASHABIKI na wanachama wa klabu ya Simba, leo watalala wakiwa hoi bin taabani baada ya timu yao kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga, mpira uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. 

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mechi uwanjani.
Mabao hayo yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili katika mechi hiyo ya kusisimua ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara yalifungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 na Amis Tambwe dakika ya 72 ya mchezo huo.

Hata hivyo Yanga wametumia udhaifu wa hasimu wao kutolewa kwa kadi nyekundu mchezaji wao Abdi Banda na kuifanya timu hiyo ipate unafuu wa kuifunga Simba.

Mpira ulikuwa wa ushindani wa pande zote mbili katika ya kwanza hadi ya 25. Hata hivyo licha ya kufungwa mabao hayo, lakini Simba walitulia zaidi kipindi cha pili, maana wamepata kona 8, huku Yanga wao wakipata kona moja tu na mashuti yaliyolenga goli yaliyopigwa na Yanga yakiwa sita na Simba wao wakipiga mashuti matano.


Hadi mpira unamalizika, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya mtani wao wa jadi Simba.

Monday, February 15, 2016

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mabalozi wapya watatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau. Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

Hashim Lundenga ambeba mgongoni Hoyce Temu

Hashim Lundenga
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (pichani) amezungumza na mtandao huu kuhusu habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kumhusu Miss Tanzania 1999, Hoyce Tamu. Lundenga amesema kuwa yeye kama Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania na Mtanzania wa kawaida amesikitishwa na maneno hayo na kuwa hayapendezi kusemwa kwa mtu kama Hoyce ambaye amejitoa kusaidia jamii.

Alisema kuwa anashangazwa na mtu ambaye amekuwa akiandika maneno hayo mtandaoni kwani hawakuwa na utofauti wowote na kilichokifanya ni kumuandika Hoyce ambaye hakuhusika katika ugomvi uliokuwepo baina ya mtu huyo na mdogo wake Hoyce, Rachel.
“Nimesikia habari hizo kumhusu Hoyce kwa kweli nimesikitishwa sana, sio jambo zuri ambalo amelifanya huyo aliyemuandika,” alisema Lundenga.

Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwataka watumiaji wa mtandao kuwa na matumizi mazuri ya mtandao ili kuzidi kuifanya mitandao ya kijamii kuwa sehemu salama kwa ndugu na marafiki kuwasiliana.

Bondia Said Mbelwa kuvaana na Ibrahim Tamba, Machi 26 Dar es Salaam

Promota Jaffari Kitemo 'katikati' akiwainua mikono juu mabondia Ibrahimu Tamba kushoto na Said Mbelwa wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana utakaofanyika march 26 katika ukumbi wa frends corner Manzese, Dar es Salaam. 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABONDIA Ibrahimu Tamba na Said Mbelwa jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 26 katika ukumbi wa Frends corner manzese Dar es salaam, mpambano uho wa raund nane kg 76 umeratibiwa na  Jaffari Kitemo.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mikataba ya kuzipiga Kitemo alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ukiondoa pambano hili na tumeandaa mpambano uhu kwa ajili ya kuondoa ubishi wa nani zaidi mana kila mmoja anatamba mtaani kuwa yeye ni zaidi ya mwenzie sasa jibu tutalipata Machi 26 pale Manzese

Naye bondia Mbelwa amesema kuwa kawaida yake ni kugawa dozi kwa kumpatia kipigo kitakatifu Tamba akijibu majigambo hayo Tamba amesema mkuwa yeye ana makuu huvyo atakikisha anafanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya kumpiga Mbelwa kwani ngumi ni ngumi tu.

Mwanachama wa Coastal Union Hafidh Kido asema mwenyekiti wao ni jipu

Niliamua kukaa kimya kuhusu kinachoendelea katika Klabu ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ hasa katika kipindi hiki tunachopambana tusishuke daraja. Uzalendo umenishinda.
Niliwahi kuwa msemaji wa timu, lakini mbali ya utumishi huo ndani ya nafsi yangu ninaipenda Coastal Union. Natamani siku zote iwe inanipa raha hata nikikaa na wenzangu nijisifie kuzaliwa Tanga.

Mdau wa soka na mwanachama wa klabu ya Coastal Union, Hafidh Kido, pichani.
Kuna kitu wengi hawakijui, Coastal Union iliyoanzishwa mwaka (1948) ni miongoni mwa timu zilizofanya vizuri katika miaka ya mwanzo ya kuanzishwa ligi kuu wakati huo ikiitwa ligi daraja la kwanza.  Hata Simba na Yanga hazikufua dafu, katika miaka ya mwanzoni baada ya uhuru timu zilizokuwa zikishika nafasi za juu katika msimamo wa ligi ni Simba, Yanga, African Sports na Coastal Union. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, timu za Tanga zinaonekana kituko.

Tulishawahi kukaa chini tukajadiliana tatizo ni nini, majibu tuliyopata ni uongozi; hiyo ni baada ya kupima vitu vinne, Kocha, Mashabiki, Wachezaji na Uongozi. Tulipoangalia morali ya mashabiki tukabaini ipo juu, maana yake kila mechi hamasa inatolewa. Tukaangalia nafasi ya wachezaji labda hawana uwezo, tukabaini wachezaji kuna baadhi ya mechi wakiamua kukaza wanapata ushindi, maana yake uwezo wanao.


Tukaangalia upande wa makocha, wengi baada ya kutimuliwa walifanya vizuri katika timu walizokwenda, tukianzia na Yusuf Chippo, Juma Mgunda, Hemed Morocco, Ally Jangalu, Mayanja na wengine wengi ambao walipita Tanga wakaonekana wabovu lakini baadaye walifanya vizuri kwengine.

Friday, February 12, 2016

Milioni 20 zazua balaa msikitini

Waumini wa dini ya Kiislam wakizozana nje ya Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam katika swala ya Ijumaa leo mchana, baada ya kutokea tafrani ya waumini hao dhidi ya viongozi wao ambao wanatuhumiwa kutafuna fedha zaidi ya sh.milioni 20 walizochanga kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
Muumini wa Msikiti huo, Mbarouk Mohamed Makame (kushoto), akizungumza kuhusu fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao. Kulia ni mmoja wa wazee wa msikiti huo, Mzee Selasela.

Waziri Jenister mhagama afunga mkutano wa 25 wa PPF




Waziri wa Sera, Bunge, Vijana Ajira na Walemavu Jenista Mhagama, akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano mkuu wa 25 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni PPF, uliomalizika leo Feb 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani/MafotoMedia. 
Wadau wa Mfuko huo wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri Jenista Mhagama.

Thursday, February 04, 2016

Bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi kuparuana Sikukuu ya Pasaka

Mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga siku ya Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es salaam. Mratibu wa mpambano huo ni kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'.
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Mada Maugo na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya Sikukuu ya Pasaka katika Uwanja wa Ndani wa  Taifa, ukiwa ni mpambano wa raundi nane KG 76.
Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba huo, kocha wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano huo amesema kuwa amewasainisha mabondia hao wanaotamba katika mchezo wa masumbwi nchini.
Mratibu wa mpambano wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka utakaofanyika  uwanja wa ndani wa Taifa.

FOS yatoa ripoti ya ushirikishwami wa wanawake kwenye Uchaguzi Mkuu

Meneja wa Mradi wa kitengo cha haki Jinsia kutoka Oxfam Bi. Rishida shariff akielezea kwa kina namna walivyofanya mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa
 Mtafiti mkuu wa kuhusiana na ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Profesa Ruth Meena akifafanua kwa kina namna ya utafiti ulivyofanyika.

Wednesday, February 03, 2016

Mchaka mchaka wa kuondosha simu feki Tanzania wazidi kupamba moto

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali  unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06#  na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15  mfano   IMEI 12456789067654  Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY  C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.

Barabara mbovu yawatoa chozi wananchi wa Mnyonzole/Kibesa

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
WAKAZI na wananchi wa vijiji vinavyounda Kata ya Panzuo,  wilaya Mkuranga, mkoani Pwani, wameendelea kuililia barabara mbovu inayoanzia Kijiji cha Kimanzichana, hali inayowalazimu akina mama kujifungulia njiani na kuuweka uhai wao rehani.
Mwendesha bodaboda Ramadhan Rajab akijaribu kupita katika barabara mbovu inayotokea Kimanzichana, kuelekea vijiji vya Mnyonzole na Kibesa,wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, nauli kwa safari moja wakitoza Sh 20,000 hadi 30,000 kwa safari moja. Nyakati za mvua barabara hiyo haipitiki hali inayozidisha ugumu wa maisha kwa wananchi hao.

Vijiji hivyo ni Marui, Kisegese, Mbezi Muungwana, Msanga Visiga, Kibayani na vinginevyo vinavyoitumia barabara hiyo inayopitika wakati wa jua kali na zinapoanza mvua mawawasiliano yao kutoka katika maeneo yao hadi kwenye barabara Kuu ya Lindi Dar es Salaam kukosekana.
Mkazi wa kijiji cha Mnyonzole Kibesa, Cosmas Kisabo, akizungumza jambo kuhusiana na kero kubwa ya barabara wanayokutana nayo wananchi hao, inayaopelekea akina mama wengi kujifungulia njiani, mvua kubwa zinapoanza kunyesha.

Mwandishi wa mtandao huu ametembelea katika maeneo hayo na kujionea hali mbaya ya barabara hiyo ambayo inaweza kuwa chanzo cha kuinua uchumi wa wananchi hao endapo itakarabatiwa japo kwa kiwango cha changarawe ngumu.

Akizungumza jana wilayani hapa, dereva wa bodaboda anayejulikana kama Ramadhan Rajab, alisema kwamba mvua kubwa inaponyesha huwezi kutoka ulipokuwa kwenda sehemu yoyote, kwa sababu barabara inakuwa mbovu.
Mkazi wa kijiji cha Kibesa, Bi Sofia Michael anayejishughulisha na kilimo na biashara ndogo ndogo, akiwa nje ya kibanda chake akizungumza na mtandao huu. Bi Sofia anasema maisha yamekuwa magumu zaidi kutokana na kukosa barabara.

“Watu wa huku tunaishi magumu mno, maana hata sisi wa bodaboda hatuwezi kufanya kazi zetu vizuri ukizingatia kuwa watu wengi wanaoishi mjini wakija kwetu tunawasafirisha katika

Tuesday, February 02, 2016

Unilever yaendelea kuwazawadia wanafunzi shule mbambali Dar

Mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Maarifa, Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam  Ester Lawrence akipokea fulana kutoka kwa Balozi wa Blue Band Neema Upendo shuleni hapo jana akiwa ni mmoja wa washindi wa shindano la Blue Band ‘Kula Tano’ linalowamasisha wanafunzi kutambua umuhimu wa kula vyakula vyenye virutubisho. Kushoto ni mwalimu wa michezo Edith Katundu.

Mkuu wa wilaya Kinondoni aendelea kupokea mifuko ya cement ya msaada kujengea shule

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500. 
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.

Monday, February 01, 2016

Mahakimu 508 wawekwa kikaangoni nchini Tanzania

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana , kuhusu utendaji wa mahakimu wa mahakama za hakimu mkazi, mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo ambapo alitoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo kwani ni wasifunguliwe mashitaka ya nidhamu na kuwajibishwa kwa kufanya kazi chini ya kiwango. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omari Mallungu na kulia ni Jaji Kiongozi wa Tanzania, Shaban Omari Lila. Jaji Chande alitoa kauli hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, akikaribishwa kutembea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo.

Na Dotto Mwaibale
JAJI Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508  watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango. Jaji Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.

Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana. Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu  wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.