Mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga siku ya Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es salaam. Mratibu wa mpambano huo ni kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'. Na Mwandishi Wetu MABONDIA Mada Maugo na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya Sikukuu ya Pasaka katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, ukiwa ni mpambano wa raundi nane KG 76. Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba huo, kocha wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano huo amesema kuwa amewasainisha mabondia hao wanaotamba katika mchezo wa masumbwi nchini. |
No comments:
Post a Comment