Pages

Pages

Saturday, February 20, 2016

Ni hatari, Yanga yaitandika Simba bao 2-0 Uwanja wa Taifa leo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MASHABIKI na wanachama wa klabu ya Simba, leo watalala wakiwa hoi bin taabani baada ya timu yao kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga, mpira uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. 

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mechi uwanjani.
Mabao hayo yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili katika mechi hiyo ya kusisimua ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara yalifungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 na Amis Tambwe dakika ya 72 ya mchezo huo.

Hata hivyo Yanga wametumia udhaifu wa hasimu wao kutolewa kwa kadi nyekundu mchezaji wao Abdi Banda na kuifanya timu hiyo ipate unafuu wa kuifunga Simba.

Mpira ulikuwa wa ushindani wa pande zote mbili katika ya kwanza hadi ya 25. Hata hivyo licha ya kufungwa mabao hayo, lakini Simba walitulia zaidi kipindi cha pili, maana wamepata kona 8, huku Yanga wao wakipata kona moja tu na mashuti yaliyolenga goli yaliyopigwa na Yanga yakiwa sita na Simba wao wakipiga mashuti matano.


Hadi mpira unamalizika, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya mtani wao wa jadi Simba.

No comments:

Post a Comment