Pages

Pages

Wednesday, July 31, 2013

Serikali yatangaza kutambua mchango wa blogs Tanzania, huku ikizundua Kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii

 Msanii wa muziki wa asili Tanzania ambaye pia ni msanii wa maigizo na filamu, Mrisho Mpoto akizungumza jambo mbele ya waaandishi wa habari na wamiliki wa blogs mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mrisho alisimama kuzungumza dakika chache baada ya wimbo alioimba na Banana Zoro kuzinduliwa, unaojulikana kama 'Futa, Delete Kabisa'. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),John Nkomo katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkomo, akizungumza mbele ya wamiliki wa blogs mbalimbali Tanzania, waandishi wa habari katika warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha suala zima la maendeleo.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), waandishi mbalimbali wa habari pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii, Blogs, wakisikiliza maneno mazuri kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Tanzania, Profesa John Nkomo, hayupo pichani. Hii ni sehemu maalumu ya kuonyesha kuwa TCRA wanatambua mchango wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na wamiliki wao kwa ujumla.
Afisa Uhusiano wa TCRA,Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali wa mambo ya habari za kwenye mitandao,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano,Warsha hiyo imefanyika leo Makao makuu ya Ofisi hizo,zilizopo barabara ya Sam Nujoma jijini Dar.
 Wadau wa mawasiliano wa mitandao ya kijamii, blogs, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA katika uzinduzi wao wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya Taifa.

MGODI UNAOTEMBEA:Nautafuta utukufu wa Samuel Sitta ndani ya CCM

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI jambo lisilowezekana hata kidogo kukaa wiki moja au mbili bila kuona tamko lolote kutoka kinywani mwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta.


 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, akizungumza jambo. Lowassa ametajwa katika mbio za urais mwaka 2015.

 Mwenyekiti wa CCM, akiwa kwenye kazi za chama chake. Jakaya Kikwete pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha mwaka (2005-2010).

Kiti cha sita baadaye kilikaliwa na Spika Anne Makinda, ambapo bila woga wala soni, Sitta aliwaambia wafuasi wake kuwa nafasi yake imehujumiwa kwasababu ya kuchukia ufisadi.

Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akizungumza na Mwana CCM mwenzake, Rostam Aziz kushoto. Rostam aliachia ngazi nafasi zake ukiwamo ubunge kwa madai ya kuchafuliwa.

Waziri Sitta amesema hayo, akiamini kuwa mafisadi wamehujumu cheo chake kwa kisingizio cha jinsia. Yani mwanamke ashike nafasi hiyo ambayo yeye hakutaka iwe hivyo.

Tuesday, July 30, 2013

Vikundi vinne vya kilimo wilayani Kilindi kujifunza katika maonyesho ya nane nane mkoani Morogoro



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
VIKUNDI vinne vya kilimo kutoka wilayani Kilindi mkoani Tanga, vinatarajiwa kuweka kambi ya siku nane katika maonyesho ya Wakulima mkoani Morogoro na kwenda kuwa mfano bora wilayani kwao.
Mkuu wa Wilaya Kilindi, mkoani Tanga, Selemani Liwowa, pichani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, DC Selemani Liwowa, alipozungumzia faida zinazoweza kupatikana katika maonyesho hayo ya wakulima yanayofanyika Morogoro kwa Kanda ya Mashariki.

Akizungumza zaidi, Liwowa alisema kuwa maonyesho ya kilimo yamekuwa na tija kwa kiasi kikubwa, hivyo anaamini kwa vikundi vyao vilivyopata nafasi hiyo vitakuwa kwenye mazingira mazuri.

Mtihani wa mawakala wa soka Tanzania kufanyika Septemba 26 mwaka huu



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MTIHANI wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.

Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.

Bondia Kibonge kutoana ngeu na Mwafyela siku ya Idd Pili

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela, pambano litakaalofanyika Siku ya Idd Pili, Ukumbi wa Friends Corner, Manzese, jijini Dar es salaam.
  Bondia Iddy Kipandu, maarufu kama Iddy Bonge kulia, akijinoa kwa kupewa maelekezo na kocha Kwame Mkuluma.

Akizungumza katika maandalizi ya mchezo huo, muandaaji wa pambaano hilo, Waziri Rosta, alisema kuwa kila kitu kinaendelea vizuri kwa ajili ya kuwaona maabondia hao wanatoana macho ukumbini humo.

Alisema mabondia wote wapo katika kiwango cha juu kuchuana katika siku hiyo, hivyo wadau na mashabiki wa masumbwi wajiandaye kupata burudani kamili ya mchezo wa ngumi hapa nchini.

Monday, July 29, 2013

Barabara kadhaa jijini Dar es Salaam kufungwa kupisha ujio wa Waziri Mkuu wa Thailand kesho Julai 30

Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi kwamba Nchi yetu imepata heshima ya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye atawasili Nchini tarehe 30/07/2013.  

Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya saa 6:30 mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.

Pitia Tamko lote la Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji juu ya kupinga kuonyeshwa mechi zao Azam TV, akisema itakuwa ngumu


Hivi karibuni, Tanzania Football Federation (TFF)  iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina  mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akizungumza na waandishi wa Habari katika moja ya matukio ya kimichezo hapa Tanzania.

1.     bodi ya TPL

1.1  Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe  ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.

1.2Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.

1.3Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.

2.   utaratibu wa dunia nzima

Maonyesho ya Elimu kufanyika Viwanja Vya Posta kuanzia Agosti 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo katikati akizungumzia maonyesho ya elimu yaliyozinduliwa leo Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom ambao ndio wadhamini wakuu, Kelvin Twissa, wakati kulia kwake ni muandaaji, Joel Njama. Picha ya juu ni Kelvin Twissa akizungumza jambo linalohusu maonyesho hayo..

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo, jana alizindua rasmi maonyesho ya elimu yaliyopangwa kufanyika kuanzia Agosti 30 mwaka huu katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo watu mbalimbali wanatarajiwa kushiriki kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu hapa Tanzania...

Katika maonyesho hayo, watu mbalimbali ikiwamo Kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania, imethitibisha kuwezesha katika maonyesho hayo yanayoandaliwa na Elimu Expo kwa ajili ya kuruhusu muingiliano wa majadiliano kati ya watengenezaji wa sera, wapenda maendeleo, watunzi mbalimbali, wazazi, wanafunzi, na jamii kwa ujumla.

Wadau wa soka wilayani Handeni waomba msaada wa kufanikisha ujenzi wa Uwanja wao wa michezo


Na Rajabu Athumani, Handeni
Wadau wa michezo wilayani Handeni mkoani Tanga wameombwa kutoa ushirikiano wa kufanikisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo wilayani humo ili uweze kukamilika.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wilayani Handeni,(HDFA) Essau Ngadallah alibainisha hayo jana katika mkutano wa kuzindua tawi la mashabiki wa timu ya Yanga wilayani humo na kusema kuwa wadau wa michezo wilyani humo hawana budi kusaidia ujenzi huo.

Ngadallah alisema kuwa walitarajia timu ya Mgambo JKT ya wilayani humo kuufanya uwanja huo kuwa uwanja wao wa nyumbani lakini imeshindikana kwa msimu huu hivyo watatumia uwanja wa Mkwakwani kuwa uwanja wao wa nyumbani.

Washindi saba wa Miliki Biashara Yako kutoka Tigo watangazwa leo na mtandao huo

 
Meneja Chapa wa Kampuni ya Simu za Mikononi ya Tigo Tanzania, William Mpinga, kushoto akichezesha droo yao ya Miliki Biashara Yako kutoka kwenye kampuni hiyo, ambapo mshindi anapewa bajaj Mpya kabisa. 

Anayefuata ni Husni Seif, Meneja Bidhaa wa Tigo na kulia ni Bakari Maggid, Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Jumla ya washindi saba walijishindia zawadi zao za bajaj kutoka kwenye mtandao huo wa Tigo na watakabidhiwa haraka iwezekanavyo. Picha na Kambi Mbwana.



Sunday, July 28, 2013

Coastal Union yaitungua Simba bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo



TIMU ya Wagosi wa kaya wameendelea kutuma salamu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara kwa kuwachapa 1-0 Simba SC kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom.
  
Timu za Simba na Coastal zikijiandaa kwa mchezo huo ambao uliisha kwa wagosi wa kaya kushinda bao 1-0.

Mfungaji wa bao hilo ni mshambuliaji Mkenya, Crispian Odula aliyesajiliwa kutoka Bandari ya Mombasa.

Edgar Mosha, mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, David Mosha afanyiwa majaribio Chelsea nchini Uingereza


DAVIS MOSHA AHOJIWA NA VOA (VOICE OF AMERICA)

Edgar Davis Mosha mtoto wa mfanyabiashara tajiri na maarufu boss wa kampuni ya DELINA  Bwana Davis Mosha ahojiwa na VOA (Voice of America). Edgar na baba yake wametua kwa kishindo nchini Marekani wakitokea Uingereza ambapo Edgar amepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuitwa  kufanya majaribio na klabu ya Chelsea ya Uingereza. Swahili TV itakuletea Exclusive video karibuni.

Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe Aung'uruma Tabora akimwaga sera kwa wananchi kibao

Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe akihutubia  Mamia ya wafuasi wa chadema kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika  kwenye viwanja vya chipukizi Mjini Tabora Jana.Picha na Chadema.

Mkuu wa wilaya mstaafu azikwa jana makaburi ya Kinondoni

 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Shilatu likipelekwa eneo atakalozikiwa maeneo ya makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Enzi za uhai wake, marehemu aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya na kulitumikia Taifa kwa moyo wake wote.

Saturday, July 27, 2013

Taifa Stars yapata kipigo cha mbwa mwizi nchini Uganda na kutolewa kwenye michuano hiyo ya kuwania kufuzu CHAN kwa kufungwa mabao 3-1

Na Mwandishi Wetu, Uganda
TIMU ya Taifa, (Taifa Stars), leo imetolewa katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN baada ya kutandikwa mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Uganda The Cranes, mchezo uliochezwa nchini Uganda leo.
Nyota wa Taifa Stars, Mrisho Ngassa
Kwa matokeo hayo, Stars itakuwa imetolewa kwa mabao 4-1, huku yakiwa ni matokeo magumu na yenye kukera watu wengi wenye mapenzi na mpira wa miguu hapa nchini.

Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1, ambapo kipindi cha pili ilionekana kuwa nyanya na kudhalilishwa vikali na wapinzani wao hao wa Uganda.

Picha mbalimbali za kusisimua, Dar es Salaam na wilayani Handeni



Ukifika wilayani Handeni, mkoani Tanga, lazima ukutane na bango hilo hapo linaloelimisha masuala ya afya na Ugonjwa wa Ukimwi. Eneo hili lipo karibu kabisa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya Handeni pamoja na ofisi nyingi za serikali wilayani humo. Picha na Kambi Mbwana, aliyekuwa wilayani Handeni.



Maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam hali hii ni kawaida kabisa. Pichani gari la taka likiwa limesheheni uchafu maeneo ya jiji. Mara kadhaa gari hili linapopita watu wengi hujikuta wameziba pua zao kwa harufu kali kutokana na takataka hizo. Picha na Kambi Mbwana.



Raha ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani Kujisitiri kwa mavazi yenye heshima na kuziba sehemu yote ya mwili, kikiwamo kichwa, kama alivyokutwa dada huyu Grace Misango, maeneo ya Kimara, jijini Dar es Salaam leo. Akina dada wengi katika kipindi cha mwezi huu wa Ramadhani unaoendelea wamekuwa wakivaa nguo za heshima zaidi jambo linalowatofautisha kabisa na kipindi chote cha maisha, hivyo kuna ulazima wa mwezi huu kuendelea? Picha na Mpiga Picha Wetu.



Mfanyabiashara huyu alikutwa hivi karibuni kijiji cha Sindeni, wilayani Handeni mkoani Tanga, akipandisha mbuzi wake kwenye gari, halipo pichani akiwasafirisha wilayani Korogwe mkoani Tanga. Picha na Kambi Mbwana, aliyekuwa Handeni.