Pages

Pages

Tuesday, July 30, 2013

Vikundi vinne vya kilimo wilayani Kilindi kujifunza katika maonyesho ya nane nane mkoani Morogoro



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
VIKUNDI vinne vya kilimo kutoka wilayani Kilindi mkoani Tanga, vinatarajiwa kuweka kambi ya siku nane katika maonyesho ya Wakulima mkoani Morogoro na kwenda kuwa mfano bora wilayani kwao.
Mkuu wa Wilaya Kilindi, mkoani Tanga, Selemani Liwowa, pichani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, DC Selemani Liwowa, alipozungumzia faida zinazoweza kupatikana katika maonyesho hayo ya wakulima yanayofanyika Morogoro kwa Kanda ya Mashariki.

Akizungumza zaidi, Liwowa alisema kuwa maonyesho ya kilimo yamekuwa na tija kwa kiasi kikubwa, hivyo anaamini kwa vikundi vyao vilivyopata nafasi hiyo vitakuwa kwenye mazingira mazuri.

Alisema wao wilaya wametoa ofa ya vikundi viwili, ambapo wadau wao wakuu, Shirika la  World Vision nao wametoa ofa ya vikundi vingine viwili kwa ajili ya kujumuika na wakulima wenzao.

“Katika maonyesho haya ya wakulima, sisi tunaamini kuwa mpango huu utakuwa na mafanikio makubwa, hivyo kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kuongeza umakini kwenye kujifunza.

“Nane Nane imepangwa kwa makundi, hivyo wilaya Kilindi inayotokea mkoani Tanga ipo katika Kanda ya Mashariki, ambapo shughuli mbalimbali zitaonyeshwa na kujifunza kwa wakulima wetu,” alisema.

Wilaya ya Kilindi inatokea katika wilaya Handeni kabla ya kugawanywa na kuwa wilaya mbili, ambapo zote zipo mkoani Tanga, chini ya Mkuu wa Mkoa wake, Chiku Gallawa.

No comments:

Post a Comment