Pages

Pages

Monday, July 29, 2013

Wadau wa soka wilayani Handeni waomba msaada wa kufanikisha ujenzi wa Uwanja wao wa michezo


Na Rajabu Athumani, Handeni
Wadau wa michezo wilayani Handeni mkoani Tanga wameombwa kutoa ushirikiano wa kufanikisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo wilayani humo ili uweze kukamilika.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wilayani Handeni,(HDFA) Essau Ngadallah alibainisha hayo jana katika mkutano wa kuzindua tawi la mashabiki wa timu ya Yanga wilayani humo na kusema kuwa wadau wa michezo wilyani humo hawana budi kusaidia ujenzi huo.

Ngadallah alisema kuwa walitarajia timu ya Mgambo JKT ya wilayani humo kuufanya uwanja huo kuwa uwanja wao wa nyumbani lakini imeshindikana kwa msimu huu hivyo watatumia uwanja wa Mkwakwani kuwa uwanja wao wa nyumbani.

Uwanja huo wa Azimio upo katika matengenezo kwa kuoteshwa majani pia kutarajiwa kuwekwa majukwaa ambapo wadau wameombwa kuchangia kwani kunahitajika kujengwa vyoo, vyumba vya kubadilishia nguo,chumba cha huduma ya kwanza na magoli ambapo mdau yeyote yule aliyetayari anatakiwa kusaidia.

Handeni.Wadau wa michezo wilayani Handeni mkoani Tanga wameombwa kutoa ushirikiano wa kufanikisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo wilayani humo ili uweze kukamilika.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wilayani Handeni,(HDFA) Essau Ngadallah alibainisha hayo jana katika mkutano wa kuzindua tawi la mashabiki wa timu ya Yanga wilayani humo na kusema kuwa wadau wa michezo wilyani humo hawana budi kusaidia ujenzi huo.

Ngadallah alisema kuwa walitarajia timu ya Mgambo jkt ya wilayani humo kuufanya uwanja huo kuwa uwanja wao wa nyumbani lakini imeshindikana kwa msimu huu hivyo watatumia uwanja wa Mkwakwani kuwa uwanja wao wa nyumbani.

Uwanja huo wa Azimio upo katika matengenezo kwa kuoteshwa majani pia kutarajiwa kuwekwa majukwaa ambapo wadau wameombwa kuchangia kwani kunahitajika kujengwa vyoo,vyumba vya kubadilishia nguo,chumba cha huduma ya kwanza na magoli ambapo mdau yeyote yule aliyetayari anatakiwa kusaidia.

Pia Ngadallah alisema tatizo kubwa kwasasa ni jinsi ya kuweza kuotesha majani uwanjani hapo kwani kuna tatizo la upatikanaji wa maji ya kutosha.

No comments:

Post a Comment