Pages

Pages

Tuesday, July 30, 2013

Bondia Kibonge kutoana ngeu na Mwafyela siku ya Idd Pili

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela, pambano litakaalofanyika Siku ya Idd Pili, Ukumbi wa Friends Corner, Manzese, jijini Dar es salaam.
  Bondia Iddy Kipandu, maarufu kama Iddy Bonge kulia, akijinoa kwa kupewa maelekezo na kocha Kwame Mkuluma.

Akizungumza katika maandalizi ya mchezo huo, muandaaji wa pambaano hilo, Waziri Rosta, alisema kuwa kila kitu kinaendelea vizuri kwa ajili ya kuwaona maabondia hao wanatoana macho ukumbini humo.

Alisema mabondia wote wapo katika kiwango cha juu kuchuana katika siku hiyo, hivyo wadau na mashabiki wa masumbwi wajiandaye kupata burudani kamili ya mchezo wa ngumi hapa nchini.

“Pambano hili limeshakuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hawo wanatafutana kwa muda mrefu, hivyo naamini kila kitu kitakwenda kamaa kilivyopangwa.

Tunawaomba wadau wa masumbwi wajiandaye vizuri kwa ajili ya kuangalia burudani ya mchezo wa ngumi ambao kwa siku kadhaa sasa umezidi kuwa na hamasa ya aina yake jambo linalowasisimua mashabiki wao,” alisema.

Aidha katika pambano hilo, pia mabondia chipukizi na wanaotamba hapa nchini wanatarajiwa kupanda ulingoni, akiwamo Hassan Mandula,  Twalib Mchanjo, Fadhili Majia, Ally Mahiyo, Mustapha Doto, Hashimu Mjeshi na wengineo.


No comments:

Post a Comment