Pages

Pages

Saturday, July 27, 2013

Taifa Stars yapata kipigo cha mbwa mwizi nchini Uganda na kutolewa kwenye michuano hiyo ya kuwania kufuzu CHAN kwa kufungwa mabao 3-1

Na Mwandishi Wetu, Uganda
TIMU ya Taifa, (Taifa Stars), leo imetolewa katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN baada ya kutandikwa mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Uganda The Cranes, mchezo uliochezwa nchini Uganda leo.
Nyota wa Taifa Stars, Mrisho Ngassa
Kwa matokeo hayo, Stars itakuwa imetolewa kwa mabao 4-1, huku yakiwa ni matokeo magumu na yenye kukera watu wengi wenye mapenzi na mpira wa miguu hapa nchini.

Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1, ambapo kipindi cha pili ilionekana kuwa nyanya na kudhalilishwa vikali na wapinzani wao hao wa Uganda.

Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar, wakati Amri Kiemba, aliisawazishia Stars na baadaye kipigo cha Stars kuendelea na kutoka vichwa chini.


No comments:

Post a Comment