https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, November 17, 2015

Nay wa Mitego anaposema Mwanamke hateswi, mwanamke hapigwi, anatulizwa kwa mapenzi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Nguvu ya sanaa ni pale inapotumika kuijenga jamii bora. Tumeishuhudia sanaa mara kadhaa ikitumika kujenga misingi ya kijamii hali inayopelekea kuweka uhusiano bora na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. Mtu anapofanya kazi kwa muda mrefu, anapaswa kutuliza akili yake kwa kusikiliza kazi za aina mbalimbali za kisanii kulingana na matakwa yake na mahitaji yake kwa ujumla. Unapoburudishwa na sanaa, kwa kiasi kikubwa unatuliza akili yako katika kuwaza mambo yenye tija katika mpangilio wako wa kimaisha. Katika kusikiliza sanaa, hususan ya nyimbo za kimapenzi ndio kabisa. Raha tupu. Unavuta hisia na kuondoa upweke na uchovu uliokuwa nao awali.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nay wa Mitego pichani.
Kama ilivyokuwa kwa watu wengine, msanii Nay wa Mitego ni miongoni mwa vijana waliowahi kuishi maisha magumu mno. Wakitafutwa wasanii 10 walioishi maisha magumu, kama Nay hajashika namba moja, basi hawezi kucheza namba tano kushuka. Hata hivyo kujituma, kumuomba Mungu na kufanya kazi kwa bidii kumemfanya leo hii Nay awe miongoni mwa wasanii wa kiume wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva. Katika wimbo wake wa 'Mwanamke Hapigwi', Nay anadhihirisha jinsi anavyoweza kutuliza akili yake kutunga wimbo unaofundisha jamii. Ni wale wanaume wanaotesa na kuwapiga wanawake. Nay anachukizwa na hilo. Anakemea. Anasema kama umemchoka binti wa watu basi mrudishe kwao badala ya kumnyanyasa kila uchao. Katika wimbo huu niupendao sana, nakufa sana na shairi hili, 
@Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
@Acha nimbembeleze kipenzi changu wee
@Najua thamani ya mwanamke  bwana wee
@Acha nimbembeleze kipenzi changu wee

Kiitikio

Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake. Wanaume feki hao, wanawatesa mademu. Sio malijali hao, wanawapiga wanawake.
Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiiiiii) Mwanamke hapigwi bwana wee, mwanamke hateswi bwana wee, anatulizwa kwa mapenzi. (Mapenziiii).

Miriaam Odemba kuwa jaji maalum shindano la Miss Universe


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Maandalizi ya fainali ya shindano la Miss Universe Tanzania 2015 bado yanaendelea Mwanamitindo wa Kimataifa Miriam Odemba atakuwa jaji maalum katika kinyang’anyiro hiki cha kumpata mrembo wa Miss Universe  anzania 2015. Majaji wengine watakaoshiriki katika kumtafuta mnyange  wa mwaka huu ni Sheria Ngowi, Maria Sarungi Tsehai, Mariam Ndaba na Priyal wa sia couture.

Zoezi la usaili limeshakamilika na hatimaye kupata warembo watakaojiunga na kambi ya Miss Universe kesho siku ya jumatano kabla ya fainali tarehe 20 mwezi huu.
Warembo waliobahatika kuingia kambini ni 14 tu, majina na mikoa  waliyotoka kwenye mabano Mariam Isack (Dar es salaam), Lilian Luth(Dar  es salaam), Stacey Sulul(Dar es salaam),Willice Donard(Dar es salaam),  


Lorraine Marriot(Dar es salaam), Dalena David(Dar es salaam), Mercy Zephania(Dar es salaam), Dinnah Kaijage(Dar es salaam), Melody Typhone(Dar es salaam), Joselyn Mirashi(Arusha), Nancy Matta(Mbeya),  


Christina Shimba(Iringa), Belinda (Mwanza).
Mwaka huu Miss Universe imefanya usaili katika mikoa sita tofauti ikiwamo Tanga, Iringa, Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es salaam.

Wafanyabiashara jijini Mbeya waaswa kuzingatia usafi ili kujiepusha na ugonjwa wa Kipindupindu


Wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.

Na Mwandishi wetu, Mbeya

Halmashauri ya jiji la Mbeya limewataka wafanyabiashara ndogondogo hususani wa chakula  kujijengea tabia ya kuchoma taka nyakati za jioni mara wamalizapo kuuza biashara zao na si kusubiri gari la taka lije kuzoa. Aidha imewataka  wakazi hao kuondokana na fikra duni  ya kuamini kuwa kazi ya uzoaji wa taka na kusafisha mazingira ni ya halmashauri ya Jiji na sio mali ya mtu.



Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Lazaro, amesema, wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya usafi na sio kusubili kupigizana kelele na serikali kwa kuwahimiza kufanya usafi kwani adui mkubwa wa afya ni uchafu hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwezake katika kutunza mazingira.



Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa malimbikizo mengi ya taka  kwenye sehemu zisizorasmi  ndani ya JIji la Mbeya na kupelekea jiji hilo kuwa chafu hususani katika maeneo ya  sokoni. Amesema, hivi sasa halmashauri ilianzisha mpango wa uzoaji wa taka barabarani ambapo mpango huo umeonekana  kupokelewa na wananchi kwa asilimia 100 changamoto inakuja kwa upande wa halmashauri kuonekana kuzidiwa kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.



“Halmashauri ilianzisha zoezi la kupitia taka zinazozalishwa na wananchi ambazo huziweka barabarani na magari yanapitia lakini mapango huu umeonekana kuzaa matunda kwa jamii kuupokea lakini tatizo ni uhaba wa vitendea kazi,”alisema.



Alisema, ili zoezi hilo lifanikiwe halmashauri inahitaji zaidi ya gari saba za ubebaji taka na kontena 80 lakini mpaka sasa magari yaliyopo ni manne na kontena 30 .



Hata hivyo kutokana na changamoto hiyo, Lazaro anawasihi wananchi kujenga tabia ya kuweka mazingira safi hasa kipindi hiki cha mvua kwani ndipo magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu yanapoibuka na kusababisha vifo vya watu.


Monday, November 16, 2015

DC wa Kinondoni Paulo Makonda awafunda waoka keki nchini Tanzania


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa tatu kulia) na Mdau wa Keki, Mama Cynthia Henjewele (wa pili kushoto), wakikata keki maalumu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Watengeneza keki Tanzania (TCBA), uliofanyika katika Mgahawa wa City Lounge Posta mpya Dar es Salaam jana. Kulia ni Mshehereshaji, Makena na Mdau wa Keki, Philip Mbonde.


Na Rahel Pallangyo, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewataka waokaji keki kufanya kazi yao kwa kushirikiana kwani inasaidia kuinua uchumi wa nchi. Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua Chama cha Waokaji keki Tanzania (TCBA) katika hafla iliyofanyika ukumbi wa City Lounge Posta mpya ambapo alikuwa mgeni rasmi.

 DC Makonda akitoa hutuba ya uzinduzi.

Saturday, November 14, 2015

Kongamano la Epowerment Empowerment of Economic Diplomacy in Tanzania lafanyika jijini Dar es Salaam

Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Ahmed Kiwanuka, Nduwayo Mzonya, Hussein Melele, na Rashid Njenga wakiwasikiliza wachangaji mbalimbali katika kongamano hilo lijulikanalo Empowerment of Economic Diplomacy in Tanzania.
Balozi mstafu wa Tanzania Nchini India ambaye pia ni mwalimu katika chuo cha diplomasia Balozi Ahmed Kiwanuka akitoa mhuadhara elo kuhusu namna Tanzania inavyoweza kutekeleza diplomasia ya uchumi kupitia ekta mbalimbali na kwa kutumia makundi mbalimbali.

Wadau wa afya wakutana mkoani Mbeya kujadiliana juu ya kuelekea Siku ya Ukimwi duniani

Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stellah Kategile akiwasilisha maada kwa wadau wa Sekta ya Afya Mkoani Mbeya katika kikao cha kujadili juu ya kuelekea katika siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani Tarehe 1 Desemba mwaka huu.
Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoani Mbeya (RACC-Regional AIDS Control Coodinator ) Dkt Francis Philly akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya afya mkoani  katika ukumbi wa Cofee Garden jijini Mbeya

Tuesday, November 10, 2015

Mkurugenzi wa CRDB Dkt Charles Kimei aongoza harambee ya KKKT mkoani Kilimanjaro

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango Mkoani Kilimanjaro. Ibada hiyo ilikwenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ambapo zaidi ya shs Milioni 100 zilipatikana. (Picha na Francis Dande)
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiijili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Cuthbert Temba akiongoza ibada.

Monday, November 09, 2015

Rais Magufuli awa mbogo, acharuka, avunja Bodi ya Afya Muhimbili

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.
“ Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko”. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.
Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine. Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.
Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini. Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).
Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.
“Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza Balozi Sefue.

Makamu wa Rais mpya akabidhiwa ofisi yake rasmi

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo. Picha zote na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Nov 9, 2015  Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wake, ....baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo.

Saturday, November 07, 2015

Masanja Mkandamizaji kuwania ubunge jimbo la Ludewa

Msanii wa komedy Emmanuel Mgaya Masanja Mkandamizaji, kushoto akisikiliza maelezo baada ya kujitosa kuwania jimbo la Ludewa kwa tiketi ya CCM, kufuatia kifo cha Deo Filikunjombe, katika jimbo la Ludewa, lililopo mkoani Njombe.

TNRF wamataka Dr Magufuli adhibiti upotevu wa wanyama pori Tanzania

 Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel.
  Mkurugenzi wa Shirika la Haki kazi Catalyst Alais Moridant akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel.

Mwanamuziki Papa Wemba atua Tanzania, kutumbuiza Tamasha la Karibu Music Festival 2015 mjini Bagamoyo

Mwanamuziki Papa Wemba (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie akimtambulisha kwa wenyeji wao.


Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.

Friday, November 06, 2015

Pata picha kali za sherehe ya Dr Magufuli IKULU

 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi usiku kwa ajili ya mchapalo maalum ulioandaliwa na Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli kusherehekea kupishwa kwake
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi 
 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein.

Thursday, November 05, 2015

Sherehe za kuapishwa Dr John Magufuli zafana, aanza kazi rasmi ya kuwatumikia Watanzania, ona picha tano kali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli, aliyesimama kushoto, akipewa hati ya kiapo chake jijini Dar es Salaam katika sherehe zilizofanyika leo na kuhitimisha rasmi utumishi wa Dr Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli, akiapa.

Diamond apewa ujali Dstv, ndio balozi wao rasmi na kuzindua pia huduma zao mpya

DSC_0168
Mwanamuiki nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Adndrew Chale
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini. Akimtambulusha rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za sikukuu.

Wednesday, November 04, 2015

SELCOM yampongeza Rais mteule Dr John Pombe na Magufuli na mama Samia Suluhu Hassan


Rais Kikwete aifanya kesho iwe sikukuu kwa ajili ya kumkabidhi IKULU rasmi Dr John Pombe Magufuli

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015

Sunday, November 01, 2015

Chadema yakanusha kushitaki ICJ nchini Uholanzi juu ya kushindwa Uchaguzi Tanzania Bara

Salaam
Ziko habari zimezushwa, kuenezwa na sasa zinakuzwa kuwa mgombea urais wa CHADEMA na chama kwa ujumla kimefungua shauri Mahakama za Kimataifa, kuhusu ubakwaji wa demokrasia na hujuma dhidi ya Watanzania uliofanyika kwenye Uchaguzi (uchafuzi?) Mkuu uliofanyika Oktoba 25. Itoshe tu kusema kuwa hadi kwa hatua ya sasa habari hizo si za kweli. Ni uzushi.
Watawala, wanaotuhumiwa kupoka haki ya Watanzania ya kuchagua viongozi wanaowataka, wanajua dhambi waliyowafanyia wananchi ni sawa na ile hadithi ya Mzee Mvuvi kwenye Vitabu vya Alfu Lela Ulela, aliyefungulia jini kutoka kwenye chupa. Dhambi inawawinda. Mzimu wa walichokifanya unawaandama. Maana safari hii ukatili (kuvuruga uchaguzi) ulikuwa wazi wazi mno.
Wanajaribu kuchokonoa kujua ukimya wa Ndugu Edward Lowassa, kama mgombea chaguo la watu, CHADEMA, UKAWA na wapenda mabadiliko unaweza kuwa na kishindo gani! ICJ, ICC au wapi hasa! Hivyo wanatunga tunga mambo na kusambaza wakitaka kupima hisia, fikra za wanamabadiliko waliotapakaa nchi nzima wakilia kilio cha kudhulumiwa haki katika uchaguzi, zinawaza nini! Maana hata wao wanashuhudia namna nchi ilivyokumbwa na msiba tangu walipotangaza matokeo yasiyooana na uhalisia wa hisia za wapiga kura na matakwa ya waliyo wengi katika demokrasia.

Saturday, October 31, 2015

Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Moshi David Mosha atangaza kuachana na siasa

Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penfold kwa lengo la kuwashukuru wana CCM waliompigia kura.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.

Picha mbalimbali wakati Dr John Pombe Magufuli anakabidhiwa cheti cha Urais wa Tanzania

 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe. Anna Mghwira  na wagombea wengine wakiwa  katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais

Friday, October 30, 2015

Janet Mbene awashukuru wana Ileje kwa kumpa kura za kishindo Dkt John Magufuli

Na Mwandishi Wetu, Ileje
MBUNGE mteule katika Jimbo la Ileje mkoani Songwe pichani, Janet Mbene (CCM) amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na  Dkt. Jonh Magufuli anayewania urais.
Akizungumza na wakazi wa Ileje, Mbene alisema ushindi wa kura 27,583 aliopewa na wana Ileje dhidi ya Emmanuel Mbuba wa NCCR Mageuzi aliyepata kura 14,578 atahakikisha anawapa wananchi hao kupitia ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakalibi.

“Awali ya yote niwashukuru wana Ileje kwa kuonesha imani kubwa kwangu, madiwani na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Jonh Magufuli. Wana Ileje wametupa kura za kishindo nami ninawahaidi sitawaangusha katika utekelezaji wa ahadi nilizozitoa kwenu wakati wa kampeni,” alisema Mbene.

Mbunge huyo mteule alisema kuwa, kipaumbele chake cha kwanza  kitakuwa mindombinu ya barabara na kuwajengea uwezo wajasiriamali  ili kuzalisha bidhaa bora ikiwemo kuongeza thamani na mauzo. Mbene alisema, hatua hiyo itasaidia kuondoa umaskini wa kipato na msisitizo utakuwa kwenye ufugaji wa samaki, kuku, nyuki na mifugo yakisasa.

Pia alisema, kilimo nacho atakipa kipaumbele hususani cha alizeti, kunde, choroko, dengu, mbaazi,  soya , karanga  zikiwemo njugu mawe kwa wingi  kama mazao ya  iashara. “Nitahakikisha pia kilimo cha nafaka  ambacho kitahusisha mahidi,mpunga, ulezi , mtama na kilimo cha matunda aina mbalimbali yakiwemomananasi , maembe, maparachichi, mapera zikiwemo mbogamboga ilikuwainua wana Ileje kupitia kilimo chenye tija,” alisema Mbene.

Mbali na hayo alisema, kwa kushirikiana na wananchi ataibua vyanzo vya asili ambavyo ni vivutio vya watalii wilayani Ileje ili viweze kuwavutia watalii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.Pia alisema, atahakikisha anashirikiana na wananchi ili kuhakikishawanatatua kero mbalimbali katika sekta ya elimu, afya na miundombinuhatua ambayo itasaidia kuinua vipato vyao, jimbo na taifa kwa ujumla.

Thursday, October 29, 2015

NMB Moshi watembelea Hospitali ya KCMC


Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB katika matawi ya Nelson Mandela na Mawenzi wakiwasili katika hosptali ya rufaa ya KCMC .

Wednesday, October 28, 2015

CCM yalalamika matokeo ya majimbo manne, yawashangaa UKAWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wana-CCM na kwa umma:

MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO
Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe. Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi. Kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya. Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa. Bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura. Hata hivyo, tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi, na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI

CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi. Tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru, uliofanyika kwa uwazi na kwa amani – na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa. Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC yasikitishwa na Maalim Seif kujitangaza mshindi wa urais Zanzibar

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema imesikitishwa na kitendo cha mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kujitangazia ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili tarehe 25 Oktoba, 2015 na imevitaka vyombo vinavyosimamia utii wa sheria kumchukulia hatua kiongozi huyo wa CUF.

“kitendo cha Maalim Seif kujitangaza mshindi amevunja kifungu cha 42 (5) cha sheria ya mwaka 1984 ambacho kinaipa mamlaka Tume ya Uchaguzi kuwa chombo pekee chenye mamlaka hayo” Mwenyekiti huyo alifafanua. Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo, Mweyekiti wa ZEC Jecha Salum Jecha alisema kuwa Maalim Seif ametenda kosa la jinai hivyo mamlaka zinazohusika zinapaswa kumchukulia hatua. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu akithibitika ametenda kosa hilo atahukumiwa kulipa faini ya Tzs laki tano au kwenda jela miaka mitano au adhabu zote.

“Tume haina mamlaka ya kumkamata wala kumhoji Maalim lakini viko vyombo vyenye mamlaka hayo hivyo itakuwa ni vyema vikatimiza wajibu wao kwa kumkamata na kumhoji mhusika hasa ukizingatiwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kutenda kosa kama hilo” Mwenyekiti wa Tume alieleza. Alibainisha kuwa Tume yake imekijadili kitendo hicho kwa makini na uzito unaostahiki na kubainisha kuwa tangazo hilo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini. Bwana Jecha alibainisha kuwa Maalim Seif, kama walivyo wagombea wengine 13 wa nafasi ya urais wa Zanzibar wanaelewa fika sheria hiyo hivyo alitoa wito kwa wagombea wengine kuwa watulivu kama walivyo wananchi.

Kuhusu kasi ndogo ya Tumeyake kutangaza matokeo, Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa kazi kubwa wanayoifanya ni kuhakiki kura kujua kama hakuna tofauti ya kura baina ya zile zilizoandikwa na hali halisi. “Wanaoandika na kuhesabu kura wote ni binadamu hivyo wanaweza kuchanganya mahesabu na ndio maana kazi yetu hivi sasa ni kulinganisha kura”alisisitiza Mwenyekiti wa Tume. Kuhusu kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura huko katika jimbo la uchaguzi la Chonga, Wilaya ya Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba, Bwana Jecha alikiri kutokea kwa hilo na kwamba suala hilo sasa liko chini ya mikono ya Jeshi la Polisi. Alitahadharisha juu vitendo vya baadhi ya wagombea kuchukua vyeti bandia vinavyoonesha kuwa tayari wao wameshinda nafasi za ubunge au ujumbe wa Baraza la Wawakilishi. Bwana Jecha alitoa wito kwa wananchi kufanya subira wakati huu Tume yake ikifanya kazi ya kukusanya na kuhakiki kura na baadae kuwatangaza washindi.

Sunday, October 25, 2015

Dk John Pombe Magufuli apiga kura wilayani Chato

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli akipiga kura yake jimboni kwake Chato mapema leo asubuhi Oktoba 25, 2015. (PICHA NA MWANDISHI WETU).

Kambi Mbwana akiwa kwenye foleni ya kupiga kura kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga

Mmiliki wa Mtandao huu na aliyekuwa mgombea ubunge katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kambi Mbwana, wa tatu kutoka kushoto, akiwa kwenye mstari wa upigaji wa kura katika Uchaguzi Mkuu, katika moja ya kituo kilichopo kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga leo Oktoba 25 kwa ajili ya kuchagua mbunge, diwani pamoja na rais. Picha kwa hisani ya group la HANDENI KWETU kwenye facebook.

Thursday, October 22, 2015

Dkt John Magufuli mgombea Urais wa CCM sasa kuomba kura kwa njia ya simu

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25 baada ya kubuni mkakati mpya wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura. 

Ujumbe huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais. Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa kuwa rais. Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani mkubwa.

Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi. Kutokana na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa awamu ya tano wa taifa hili. Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache zijazo.

Joyce Msiru ndio Mkurugenzi mpya wa mamlaka ya maji na mazingira Moshi


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi, MUWASA, Sharry Raymond akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo wakati wa utamburisho wa Mkurugenzi mpya wa MUWSA. Picha zote na Dixon Busagaga 

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA.
Mwenyekiti wa Bodi ya MUWSA,akizungumza.

CCM kufunga kampeni kwa mtindo wa aina yake, Rais Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Kinana kufanya mashambulizi mikoani

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.

Kufunga Kampeni
CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo.  Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
 1.    Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
 2.    Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
 3.    Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
 4.    Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5.    Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6.    Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7.    Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu  Mstaafu
Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi saba.

Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.  Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

Makamu wa Rais Dkt Bilal aagana na watumishi wa ofisi yake

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewashukuru watumishi wa ofisi yake kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha miaka mitano kiasi cha kuweza kutekeleza majukumu ya msingi ya ofisi hiyo ya kudumisha Muungano na uhifadhi wa mazingira kwa ufanisi mkubwa.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Saz Salula, akizungumza kutoa shukurani wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya Mhe. Makamu wa Rais kuagana na Watumishi wa Ofisi yake. Hafla hiyo ilifanyika juzi Okt 20, 2015 kwenye Makazi ya Dkt. Bilal. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watumishi wa Ofisi yake (baadhi hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam, juzi Okt 20, 2015. Picha na OMR

Akizungumuza katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es salaam Dkt. Bilal alisema kuwa, anayo furaha kufikia kipindi hiki na kwamba alifanya majukumu yake vema kutokana na kuwa na wasaidizi mahiri na waliojitoa kufanya kazi zao kwa weledi na uvumilivu mkubwa muda wote.

“Natumia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote. Walinisaidia sana katika kipindi nikifanya kazi ya kuitumikia nchi yangu. Niwashukuru ninyi wafanyakazi wa ofisi yangu, mlifanya kazi kwa kujituma sana na majukumu yetu kwa mujibu wa taratibu tuliyatekeleza kwa ufanisi,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais na kuongeza:

“Nakutakieni kila la kheri katika utendaji wenu. Jitahidini kufanya kama mlivyofanya kwangu kwa yule atakayekuja baada yangu. Nakushukuruni kwa zawadi hasa ya vitabu maana mimi ni muumini wa kusoma, nitavisoma”. 

Wateja wa Bayport sasa kukopeshwa simu za mikononi

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani akizungumza jambo katika moja ya shughuli za taasisi hiyo nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SEKTA ya mawasiliano ni kati ya mambo muhimu na mazuri inayoweza kufanikisha kwa vitendo kukuza uchumi wa Taifa letu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kusimamia vyema sekta hiyo, uchumi wa Wwatanzania utakuwa kwa kasi.

Na katika mambo yaliyokuwa kwenye kundi hilo la mawasiliano, ni kuona Watanzania wanawasiliana kwa kumiliki simu imara ili waweze kuwasiliana katika mahitaji yao ya kimaisha, bila kusahau biashara na wajasiriamali.

Si lazima mtu aende mkoani Mbeya, Tanga, Arusha kufuata au kupeleka bidhaa zake bila kufanya uchunguzi swa soko, hususan kwa kuwasiliana na watu wanaoishi huko, au wale wanaoshirikiana katika majukumu yao ya kila siku.

Mke wa Dkt Shein achanja mbuga kumuombea kura mumewe visiwani Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Bububu kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi wa Wanawake wa Wilaya ya Mfenesini Unguja Kichama kuwaombea Kura Wagombea Wote wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Mfenesini Unguja Kichama akitowa salamu za Wilaya yake kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kabla ya kuaza kwa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Bububu.
Viongozi wa UWT Wilaya ya Mfenesini Unguja wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kuwaomba kura kuwapigia Wagombea wote wa CCM.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...