Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI ha hatari imejitokeza katika msiba wa Ofisa Habari wa
Bunge, Ernest Zulu, baada ya jana usiku kutokea mvutano kutokana na upande
mmoja kalazimisha aende kuzikwa kwao Songea, huku watoto wakitaka azikwe jijini
Dar es Salaam.
Marehemu Ernest Zulu kulia enzi za uhai wake.
Kabla ya kifo chake, marehemu alitoa usia kuwa akifa basi
azikwe jijini Dar es Salaam alipozikwa motto wake wa kwanza, hata hivyo kaka wa
marehemu, Emmanuel Zulu, amekuja juu akitaka mdogo wake akazikwe nyumbani kwao.










