https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, November 05, 2013

DC Muhingo: Tamasha la Handeni ni fursa ya kimaendeleo, watu washiriki kwa wingi



Na  Mwandishi Wetu, Handeni, Tanga
MKUU wa wilaya Handeni, DC Muhingo Rweyemamu, amewataka wananchi wa Handeni, mkoani Tanga kulitumia Tamasha la Handeni kwa ajili ya kutafuta fursa za kimaendeleo.
Mkuu wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Akizungumza jana mjini Handeni, Muhingo alisema kutokana na tamasha hilo kufanyika mwisho wa mwaka, Desemba 14, itakuwa chachu ya kuwaunganisha watu wote, sanjari na kujadili changamoto zinazoikabiri Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Muhingo alisema kuwa tamasha hilo lina umuhimu mkubwa kutokana na kuandaliwa maalum kwa ajili ya Watanzania kwa ajili ya kuangalia ngoma na matukio mbalimbali ya kijamii.

“Wakati napongeza kwa dhati kuandaliwa kwa tamasha hili wilayani hapa, pia nawaomba watu waje kwa wingi kushuhudia namna gani Handeni imepiga hatua kimaendeleo na kuangalia namna gani wanaweza kusonga mbele.

“Naamini tutafikia hatua nzuri kwa kushirikiana na wadau wote, hivyo wale wanaoishi mbali na Handeni pia ni wakati wao kurudi nyumbani mwishoni mwa mwaka kujifunza mambo ya utamaduni wao, sanjari na kufanya juhudi za kupiga hatua kimaendeleo,” alisema.

Tamasha hilo linaloandaliwa na Mratibu wake Kambi Mbwana, hadi sasa limedhamiwa na Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.

Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com, huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi saa 12 za jioni.

Monday, November 04, 2013

Jeshi la Polisi Zanzibar laipongeza timu ya Polisi Pemba


Na Masanja Mabula -Pemba
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amewapongeza wachezaji wa timu ya Polisi inayoshiriki ligi kuu Visiwani hapa kwa kuonyesha nidhamu na kucheza kwa kujituma na kufanikiwa kuchukua alama sita kutoka Kisiwani Pemba .

Akizungumza na msafara wa timu hiyo huko Ofisini kwake Wete , Kamanda Shekhan amewataka wachezaji na viongozi wa timu hiyo kuongeza juhudi za mazoezi ili kuiwezesha timu kuchukua moja ya nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi na kuiwakilisha Nchi kwenye michuano ya Kimataifa . 

Amesema kuwa bila ya kuwepo na ushirikiano wa dhati  kati ya wachezaji na viongozi pamoja na   kuthaminiana kwa kila mmoja  wawapo nje na ndani ya uwanja mafanikio hayawezi kupatikana .

"Ni jambo la kujivunia kwamba timu umekuja Pemba na kuondoka na alama zote sita , nawaombeni muendelee kushirikiana , kuthaminana na kupendana ndani na nje ya uwanja ili muweze kuiletea mafanikio timu na jeshi la Polisi Visiwani hapa," alieleza Shekhan .

Naye msemaji wa timu hiyo Ramadhan Khamis Ramadhaman amesema kuwa ushindi walioupata kwa mechi za Pemba  umetokana na ushirikiano walionao wachezajio pamoja na Benchi zima la uongozi ambapo kila upande ulitimiza wajibu wake kama ilivyotakiwa.

"Unajua mafanikio haya yametokana na sisi kuwa na ushirikiano, ambapo wachehzaji walitekeleza majukumu yao kama walivyoelekezwa na viongozi nao waliwajibika kwa mujibu na kazi zao," alifamaisha.

Aidha Nahodha wa timu Adam Juma amesema kuwa lengo lao ni kutwa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar  na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono ili waweze kutimiza azma yao hiyo .

"Lengo ni kuwa mabingwa tumewahi kutwa ubingwa  wa ligi kuu  Zanzibar na tunajua utamu wa ubingwa , sisi wachezaji tumewasha moto na kwa sasa sifikirii kama kuna timu utauzima , tunataka kurejesha heshima na hadhi ya timu yetu,"alijinadi Adam .

Ikiwa kisiwani Pemba Timu ya Polisi imecheza michezo miwili ambapo iliifunga timu ya Kizimgbani Unioted mabao 3-1 kabla ya kuifunga timu ya Jamhuri ambayo inahemea chumba cha wagonjwa mahtuti kwa jumla ya mabao 2-1. na kuifanya timu ya Polis kufikisha alama 19 .

CCM Kinondoni kunoana makali mjini Dodoma kwa siku nne

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Kinondoni, kimeanza mikakati ya kuwanoa viongozi wake ili kuwapatia uzoefu wa kukitumikia chama kwa kipindi kijacho na hatimae kuwa na nguvu, kwa kuandaliwa semina itakayofanyika kesho (leo), mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Kinondoni, Salum Madenge, akiwa kwenye moja ya matukio ya kichama.
 Semina hiyo inahusu wenyeviti wa CCM wa Kata zilizopo wilayani Kinondoni, huku ikiwa na dhamira yaa kuhakikisha viongozi hao wanapewa uwezo wa kutimiza majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza leo asubuhi wakati viongozi hao wanaelekea katika semina hiyo ya siku nne mjini Dodoma, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kinondoni, Salum Madenge, alisema kwamba siku zote malengo ya chama ni kushika dola, hivyo anaamini kwa kuandaliwa semina hiyo ni sehemu ya kujenga mfumo mzuri wa kiutendaji ndani ya chama chao.

Alisema ukiacha semina ya wenyeviti wa Kata Kinondoni, pia Makatibu wameshafanyiwa mpango huo, jambo ambalo linaonyesha mwendo mzuri wa chama chao.

Link ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu duniani nje ya nchi yazinduliwa

Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa. Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu.  Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba akiongea machache katika uzinduzi wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link, AbdulMalki Molel akitoa maelezo jinsi mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ambapo jna ilikuwa ndiyo uzinduzi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Sunday, November 03, 2013

Madereva wa bodaboda kupewa mafunzo ili kupunguza ajali za barabarani

pikipikiKampuni ya Ijumba Enterprises inatarajia kuzindua mradi wa Safari Salama {Safer Journey} katikati ya mwezi November, 2013.
Mradi huu unalenga waendesha pikipiki za miguu miwili na mitatu yaani bodaboda. Mradi unalenga kuwaongezea waendesha bodaboda elimu ya udereva salama na kuzijua sharia za usafirishaji.
Kampuni hiyo imegundua kwamba ajali nyingi zinazotokana na bodaboda kwa kiasi kikubwa husababishwa na waendeshaji wake kutokuwa na elimu ya udereva na sharia za barabara. Pia, vijana wengi wanapfanya shughuli hizi wako chini ya umri unaotakiwa au kuruhusiwa kuendesha vyombo vya moto kisheria na asilimia kubwa hawaja hudhuria mafunzo yeyote ya udereva. Hili limikuwa tatizo kubwa na chimbuko la ajali nyingi barabarani zinazo sababishwa na bodaboda.
Kampuni kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi idara ya Usalama barabarani na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji  {NIT} inatarajia kutoa mafunzo kwa Wilaya za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Mafunzo haya yatakuwa niya kivitendo zaidi na kuwasaidia wadau wao kuweza kupata lesini na kusajili vituo vya kuegesha bodaboda zao.
 Wadau mbalimbali wanakaribishwa  kwamaana ya wadhamini wa mafunzo hayo kwani hii ni fursa ya kuisaidia juhudi za serikali na jamii kwa ujumla ya kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.

Mama Tunu Pinda afunga maonyesho ya wanawake wajasiriamali viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam

DSC_0394
Mama Tunu Pinda akikaribishwa kufunga maonyesho ya wiki ya Wakinamama Wajasiriamali na Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza wajasirimali wanawake Tanzania kutoka ILO, Noreen Toroka. kushoto kwa Mama Pinda ni Mwenyekiti wa MOWE, Bi Elihaika Mrema na
DSC_0354
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akifunga rasmi Maonyesho ya Wanawake Wajasirimali (MOWE) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, maonyesho hayo ya wanawake wajasiriamali yalikuwa ya wiki nzima ambapo wakinamama wanapata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa mbalimbali Usindikaji, Mvinyo, Batiki kwa wakazi wa jijini.
DSC_0337
Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali kwa wanawake Tanzania toka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka akizungumza wakati hafla ya kufunga maonyesho hayo ambapo amesema wiki nzima ilikuwa ni maonyesho wanawake toka sehemu mbalimbali nchini Bara na Visiwani wamepata wasaa wakubadilishana mawazo na mbinu za Kibiashara.
DSC_0324
Mwenyekiti wa Kamati ya MOWE, Mama Elihaika Mrema akizungumza wakati wa kufunga maonyesho hayo ya Wajasirimali wakinamama jijini Dar es Salaam.

Duh, hili la likizo ya malipo kwa Angetile Osiah ni balaa lingine kwa kasi ya uongozi mpya wa Jamal Malinzi

KIKAO cha kwanza cha Kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana chini ya Rais, Jamal Emil Malinzi kimemuengua Katibu Mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah Malabeja.

Rais Malinzi, alifungua kikao kwa ajenda ya kumuengua Angetile na Wajumbe wakaafiki, lakini wanamng’oa kistaarabu.
Angetile amepewa likizo ya hadi atakapomaliza Mkataba wake mwezi ujao na kwa sasa, aliyekuwa Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura Mgoyo atakatimu nafasi yake.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.
Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.
Jamal Malinzi
Rais, Dar es Salaam
Novemba 3, 2013

Mwandishi Careen Mgonja amuandalia party ya nguvu mtoto wake kusherehekea kipaimara chake, Buza jijini Dar es Salaam

Carrenflora Mgonja wa kundi la wajasiliamali wa kikundi cha Habari Group akiwa na mumewe Patson Mlandali wakati wa kumfanyia part ya kipaimara bint yao Elizabet iliyofanyika katika ukumbi wa Abiola Buza Dar es salaam jana
Washereheshaji wa shughuli hiyo Anti Latifa kushoto na Sakina Lioka wakiwa na CArren Mgonja wakati wa sherehe ya mwanae
Elizabet
Mwandishi wa habari za michezo, Somoe Ng'itu kulia, akiwa na mfanyakazi mwenzake huku wakionyesha uso wa tabasamu katika party hiyo ya kipaimara jana.

Malinzi:Simba na Yanga kukiona cha moto


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

 RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, amevitaka vilabu vya soka vya Simba na Yanga kukubali matokeo ya uwanjani ili wasiingie kwenye mgogoro kwakuwa ofisi yake watakuwa wakali dhidi yao.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi, pichani.
Malinzi aliyasema hayo katika makabidhiano ya ofisi kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake, Leodgar Tenga, huku yakihudhuriwa na watu mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la aina yake.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema watakaokiuka sheria zitawabana, huku akitumia muda mwingi kuwataka Simba na Yanga wakubali matokeo na kuacha kufanya vurugu.


Alisema yoyote atakayefanya mambo kinyume sheria hazitawaacha watambe, hivyo mchezo wowote utakapokuwa unafanyika mwamuzi ndiyo anakuwa mtu wa mwisho kwenye patashika hiyo.

Saturday, November 02, 2013

Rais Kikwete arejea nyumbani akitokea nchini Uingereza kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali uwazi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2013 akitokea London, Uingereza, alikohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government Partneship Summit). Anayeongozana naye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mwatumu Mahiza.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2013 akitokea London, Uingereza, alikohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government Partneship Summit), akiongozana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali aliyefika kumlaki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mblaimbali baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2013 akitokea London, Uingereza, alikohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government Partneship Summit).  PICHA NA IKULU

Matokeo ya darasa la saba 2013 yatangazwa na serikali leo na kiwango cha kufaulu kupanda kwa asilimia 6.01 na 28.06

LEO Matoke ya Darasa la Saba yametangazwa huku mwaka huu ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 30.72 mwaka jana mbaka asilimia 50.61 mwaka huu kutokana na wanafunzi walio fanya mtihani mwaka huu wa darasa la saba wamefaulu zaidi ukilinganisha na wanafunzi wa mwaka jana Kaimu mtendaji wa Baraza la Mtihani Charles Msonda amesema ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 6.01 na 28.06 ukilinganisha na mwaka 2012 Mwaka huu watainiwa wamefahulu zaidi katika somo la Kiswahilin kwa asilimia 69.06 na somo walilio faulu kwa kiwango kidogo zaidi ni somo la Hisabati wamefaulu kwa asilimia 28.62 Msonda amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya 844,938 walio fanya mtihani huo wamepata alama ya 100 kati ya alama ya 250 idadi hiyo nisawa na asilimia 50.61/
 http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/psle.htm

Hotuba nzito ya Rais Mstaafu wa TFF, Leodgar Tenga wakati anamkabidhi ofisi Jamal Malinzi leo, hebu ipitie hatua kwa hatua



TAARIFA YA MAKABIDHIANO YA OFISI YA TFF YALIYOFANYIKA KATIKA OFISI ZA TFF JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 2 NOVEMBA 2013
 
Rais wa zamani wa TFF, Leodgar Tenga
Mheshimiwa Rais wa TFF,

Pongezi na Shukurani

1.         Naomba nianze kwa kushukuru kwa kukubali kufanyika kwa shughuli hii ya makabidhiano ya Ofisi. Utaratibu huu haupo kikatiba wala katika kanuni zetu, lakini ni muhimu sana kwa vile unatoa taswira ya uongozi endelevu na ushirikiano unaostahili kuwepo baina ya uongozi mpya na ule wa zamani.

2.         Aidha napenda, kwa mara nyingine, kukupongeza kwa dhati wewe binafsi kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Shirikisho letu pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa ushindi wao.

3.         Tumeshuhudia mchakato wa uchaguzi uliofanyika kwa uwazi, na ulio huru na wa haki. Ninawashuru sana na kuwapongeza Wajumbe wa Kamati ya Uchanguzi kwa ueledi na kazi nzuri walioifanya. Kwa kiwango hicho hicho ninawapongeza na kuwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wa Kamati za Maadili – ngazi ya awali na ya rufani – kwa kutekeleza wajibu wao kikamilifu na vyema.

4.         Nawajibika kutoa pongezi kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kukamilisha kazi muhimu ya kutuchagulia viongozi wetu kwa utulivu mkubwa.

5.         Utulivu wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi – kuanzia mwanzo hadi mwisho – ni kielelezo cha ukomavu wa uongozi wa mchezo wa mpira wa miguu nchini. Natoa shukurani za dhati kwa wanachama na wadau wote wa mpira wa miguu nchini kwa mchango wao wa hali na mali katika kufanikisha zoezi hili muhimu kwa mustakabali wa mpira wa miguu nchini.


Dira na Malengo ya Uongozi Uliopita

6.         Dira ya uongozi uliopita ilikuwa ni kujenga mazingira mazuri na endelevu ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu nchini. Hii ilitokana na hali ya migogoro isiyoisha na malumbano ya mara kwa mara yaliyokuwepo kabla ya kuingia madarakani.

7.         Ili kufanikisha dira yetu, uongozi uliopita ulidhamiria kujenga msingi bora wa uongozi wa mpira wa miguu nchini, hivyo kujiwekea malengo yafuatayo:

·         Kutengeneza Katiba mpya na Kanuni zitakazokidhi mahitaji ya nchi yetu ya kudumisha demokrasia na utawala bora – uwazi, uwajibikaji, na kadhalika.

·         Kuhakikisha kuwa Katiba yetu na Kanuni zetu zinazingatiwa na kuheshimiwa.

·         Kuweka Kanuni za Fedha na kuchukua hatua za kujenga uaminifu katika usimamizi wa ukusanyaji, utunzaji na matumizi ya fedha.  Tuliazimia kuona hesabu za Shirikisho zinakaguliwa na wakaguzi wenye sifa za kimataifa, na taarifa ya ukaguzi kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu kila mwaka, bila ya kukosa.

Hafidh Kido apewa usemaji Coastal Union ya Tanga baada ya Edo Kumwembe kujiweka kando



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANDISHI na mdau wa karibu mno na timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, Hafidh Kido, amefanikiwa kurithi mikoba ya msemaji wa zamani Edo Kumwembe kwa ajili ya kazi ya kupashana habari zinazoihusu klabu hiyo.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Raia Mwema sasa ndio msemaji mpya wa Coastal Union baada ya Edo Kumwembe.

Akizungumza jana kwa njia ya simu akitokea mkoani Tanga, Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Aurora, alisema kuwa wamefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuiweka nafasi hiyo kwa mtu makini na mwenye kuimudu zaidi.
Edo Kumwembe, pichani.
Alisema kuwa Kido alikuwa mdau wa Coastal huku akifanya kazi kwa karibu na Kumwembe wakati ni msemaji wa klabu hiyo, hivyo wanaamini kuwa atafanya kazi zake kwa moyo naa ujasili wa aina yake.

“Tumeamua kumpa rasmi Kido ili awe msemaji wa klabu yetu akirithi mikoba ya Kumwembe ambaye kwa sasa sio msemaji, huku tukiamini kuwa atafanya kazi zake kwa kujituma kama alivyofanya wakati wote.

Cheka:Umaarufu wangu unanipa uchungu



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Francis Cheka, amesema kwamba umaarufu wake unampa uchungu kwasababu hauendani na maisha halisi anayoishi kutokana na mchezo huo kutawaliwa na njaa ya kutisha.
Bondia Francis Cheka, pichani.
Akizungumza jana kwa njia ya simu akitokea mkoani Morogoro, Cheka alisema mfumo mzima wa maisha yake umekuwa wa njaa na hakuna kampuni inayofikiria namna ya kuingia naye mkataba ili afike mbali zaidi.

Alisema amekuwa akipata fedha kiduchu mara chache anapokuwa na pambano, huku gharama za maandalizi za mchezo huo kuwa kubwa na kumpa wasiwasi wa maisha yake ya baadaye atakapoachana na masumbwi.

Cheka alisema ukata huo ndio unaomfanya ashindwe kutembelea kaatika mikoa mbalimbali ya Tanzania kujionea hali ya masumbwi ilivyo sanjari na kushirikiana na wadau wengine kuweka mipango ya kimaendeleo.

Friday, November 01, 2013

Kamishna wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja akabidhi vyeti vya udereva kwa mafunzo ya maaskari magereza

image 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(mbele katika Jukwaa) akipokea Saalam ya heshima na Utii kutoka kwa Gadi Maalum ya Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu 72 wa Mafunzo Maalum ya Udereva katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro. Hafla fupi ya ufungaji Mafunzo hayo imefanyika leo Novemba 1, 2013 katika viwanja vya Kingolwira, Morogoro.
2 

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja  (kulia) akikagua Gadi Maalum ya Gwaride lililoandaliwa Maalum kwa ajili ya Ufungaji Mafunzo ya Udereva Kozi No. 19 ya Mwaka 2013 ambayo yamefanyika leo Novemba 1, 2013 katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro. 3 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akikagua moja ya Gari aina   Bedford ambalo hutumika kufundishia Madereva Wanafunzi katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva kilichopo Kingolwira, Mkoani Morogoro. Mafunzo Maalum ya Udereva yamefungwa rasmi leo Novemba 1, 2013 na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini.
4 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja akimkabidhi cheti mmoja wa Wahitimu wa Kozi ya Udereva, Cpl. Nuru kutoka Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam. Cpl. Nuru ni minongoni mwa askari 11 wa Kike ambao wamehitimu mafunzo Maalum ya Udereva leo Novemba 1, 2013  na Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa Mwezi mmoja katika Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro ambapo jumla ya Askari 72 wamehitimu Mafunzo hao kwa ustadi mkubwa.

Temeke sasa waja na mapya ya kuondoa uchafu katika manispaa yao

IMG_8912
Afisa Afya Usafishaji toka  Manispaa ya Temeke Ernest Mamuya akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na manispaa katika kukabiliana na wachafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutozwa faini isiyopungua 50,000,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).katikati ni Afisa Afya Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Willium Muhemu na mwisho ni Afisa Habari wa Manispaa hiyo Bi.Lynn Chawala. IMG_8915
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Manispaa ya Temeke. IMG_8916
Afisa Afya Mazingira toka Manispaa ya Temeke Bw. Willium Muhemu akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) mikakati mbalimbali ya Manispaa hiyo inayotumika katika kuhakikisha wakazi wa manispaa husika wanatekeleza sheria na kanuni za afya zilizoweka ,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kulia ni Afisa Habari wa Manispaa hiyo Bi.Lynn Chawala.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Na Frank Mvungi Maelezo
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yatenga zaidi ya shilingi milioni 434 katika bajeti ya 2013/2014 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya usafi wa mazingira.
Hayo yamesemwa naAfisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Temeke  Bw. Ernest Mamuya leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.
Alisema manispaa hiyo imeweza kuendesha ukaguzi  katika maeneo ya kutolea huduma kama hoteli na katika makazi ya watu ili kuwabaini wanaochafua mazingira.

Picha za matukio ya bungeni mjini Dodoma leo

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Arumeru Mashariki na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Mideye, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 1, 2013. 
 Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola akichangia Bungeni Mjini Dodoma Novemba  1, 2013
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akiteta  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephene Wasira (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Uratibu, William Lukuvi (wapili kulia) na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Clouds Media Group kudhamini tamasha la Handeni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Clouds Media Group, imekuwa miongoni mwa wadau waliojitokeza kudhamini Tamasha la Handeni, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu na kusubiriwa kwa hamu wilayani Handeni mkoani Tanga nchini Tanzania.
Mkurugrnzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Kwa sasa maandalizi kabambe yamekuwa yakipamba moto kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa kwa mafanikio makubwa, sanjari na kutafuta mbinu za kimaendeleo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo linalotambulika pia kama ‘Handeni Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kuwa kuingia kwa kampuni hiyo ni sehemu ya kulifanya tamasha hilo liwe na mvuto mkubwa zaidi.

Alisema kuwa juhudi zao ni kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika wilayani humo na kushirikisha mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla, hivyo ni wakati wa wadau wengine kujitokeza kuliwekea mguso wazo hilo.

“Tunashukuru kuona Watanzania wote wanaingia humu ili wazo hili lifanikiwe kwa kiwango kikubwa, ingawa tamasha hili linafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, huku likiwa na changamoto lukuki.

“Naamini huu utakuwa mwanga mzuri kutoka kwa wenzetu Clouds Media Group ambao pia wanamiliki redio ya Clouds FM na Clouds TV, huku wakiwa ni waandaaji wa Tamasha kubwa la Fiesta linalofanyika kila mwaka na kuzunguuka mikoa mbalimbali ya Tanzania na kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa ndani na ule wa Kimataifa,” alisema Mbwana.

Wadhamini wengine ni Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho kwa kupitia Kampuni yake ya Phed Trans, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD,  Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.

Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.



LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...