Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
KAMPUNI ya Clouds Media Group,
imekuwa miongoni mwa wadau waliojitokeza kudhamini Tamasha la Handeni,
linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu na kusubiriwa kwa hamu wilayani
Handeni mkoani Tanga nchini Tanzania.
Mkurugrnzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Kwa sasa maandalizi
kabambe yamekuwa yakipamba moto kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha hilo
linafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa kwa mafanikio makubwa,
sanjari na kutafuta mbinu za kimaendeleo.
Akizungumza jana jijini
Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo linalotambulika pia kama ‘Handeni
Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kuwa kuingia kwa kampuni hiyo ni sehemu ya
kulifanya tamasha hilo liwe na mvuto mkubwa zaidi.
Alisema kuwa juhudi zao
ni kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika wilayani humo na kushirikisha mkoa
wa Tanga na Tanzania kwa ujumla, hivyo ni wakati wa wadau wengine kujitokeza
kuliwekea mguso wazo hilo.
“Tunashukuru kuona Watanzania
wote wanaingia humu ili wazo hili lifanikiwe kwa kiwango kikubwa, ingawa
tamasha hili linafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, huku likiwa na
changamoto lukuki.
“Naamini huu utakuwa
mwanga mzuri kutoka kwa wenzetu Clouds Media Group ambao pia wanamiliki redio
ya Clouds FM na Clouds TV, huku wakiwa ni waandaaji wa Tamasha kubwa la Fiesta
linalofanyika kila mwaka na kuzunguuka mikoa mbalimbali ya Tanzania na kukonga
nyoyo za wapenzi wa muziki wa ndani na ule wa Kimataifa,” alisema Mbwana.
Wadhamini wengine ni
Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho kwa kupitia
Kampuni yake ya Phed Trans, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa
Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine ni duka la mavazi la Chichi
Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa
kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason
Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.
No comments:
Post a Comment