Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 28
imefanyika leo, huku mkazi wa Goba, jijini Dar es Salaam, Moses Matagili,
akifanikiwa kuibuka kidedea kwa kushinda Sh Milioni 20.
Kajala Masanja Balozi wa Biko Tanzania.
Droo hiyo iliyofanyika jana, ilichezeshwa na Balozi wa Biko,
Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, Jehud Ngolo.
Akizungumza baada ya kumpata mshindi huyo, Mratibu wa Matukio
na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema sasa ni wakati wa kuchangamkia
fursa ya kuibuka na mamilioni kwa kucheza Biko inayotoa ushindi wenye fursa ya
kiuchumi.
Alisema kwamba droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 inafanyika
Jumatano na Jumapili, huku Jumatano hii ikienda kwa Matagili, ambaye ni mkazi
wa Goba, sanjari na washiriki kuvuna zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia
Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.
“Tunampongeza mshindi wetu wa droo ya 28, Matagili kwa kuvuna
donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko, hivyo tunawaomba Watanzania wengine
waendelee kucheza Biko ili waweze kujipatia zawadi mbalimbali kutoka kwetu.
“Jinsi ya kucheza ni rahisi maana bahati nasibu yetu
inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu
za Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na
kumbukumbu ni 2456,”Alisema.
Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Jehud Ngolo, alisema mchezo wa Biko unachezwa kwa kufuata sheria zilizowekwa,
jambo linaloongeza ufanisi kwa Watanzania wote kucheza na kushinda zawadi za
Biko.
“Tunawakumbusha Watanzania kuwa Biko ni mchezo rahisi na
ambao unachezeshwa kwa uangalizi mkubwa wa bodi yetu, hivyo kwa wale wanaocheza
waelewe kuwa huu ni mhcezo salama,” Alisema.
Wakati Matagili akiibuka kidedea kwa kuzoa Sh Milioni 20
kutoka Biko huku akitarajiwakukabidhiwa fedha zake mapema iwezekanavyo, tayari
mshindi wa droo ya 27, Viane Kundi wa Irnga, akiwa ameshapokea fedha zake
Jumatatu iliyopita.
No comments:
Post a Comment