Na Mwandishi
Wetu,Mbeya
SERIKALI ya
Mkoa wa Mbeya, zimewataka watumishi wa umma katika mkoa wao,hususan kupitia
ofisi zitakazonufaika na msaada wa kompyuta nane kutoka kwenye taasisi ya
kifedha ya Bayport Financial Services, kuongeza ufanisi wa kazi kwa kupitia vitendea kazi hivyo vilivyotolewa.
Majadiliano yakiendelea katika makabidhiano hayo ya kompyuta kutoka Bayport Financial Services mwishoni mwa wiki, mkoani Mbeya.
Akizungumzia
hilo, Enock alisema kwamba haitakuwa na maana kama msaada wa kompyuta za
Bayport hautaongeza ufanisi kazini na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa
kutumia vyema vitendea kazi hivyo vipya vinavyoweza kuleta tija kama kila
mtumishi atafanya kazi kwa nguvu zote ili kuwatumikia wananchi.
“Huu ni msaada mkubwa kwa mkoa wetu, hususan wale ambao kwa namna moja ama nyingine watazipokea kompyuta hizi kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ukizingatia kwamba mpango huu ulizinduliwa kwao tangu mwaka jana.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock akigawa kompyuta hizo kwa wahusika baada ya kukabidhiwa na Bayport Financial Services.Ugawaji wa kompyuta ukiendelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya.
“Nawaomba
wale ambao watapokea kompyuta hizi wakafanye kazi kwa nguvu zote tukiamini kuwa
wenzetu wa Bayport watakapoamua kufanya utafiti wa vifaa vyao jinsi
vilivyotumika, basi kuwe na tija ili waendelee kushirikiana na sisi kwa mambo
mengine,” Alisema Enock.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial
Services, Mercy Mgongolwa, alisema ni furaha yao kuzifikisha kompyuta hizo kwa
mkoa Mbeya, ikiwa ni siku chache baada ya kuingia mwaka mpya wa 2017.
“Tunaamini
kwa kiasi kikubwa kuwa wenzetu wa Mbeya watazitumia kompyuta tulizo wapa kama
sehemu ya kupanua wigo wa kuwatumikia wananchi kwa ajili ya kukuza uchumi wao
na Watanzania kwa ujumla kwa namna moja ama nyingine.
“Baada ya
kuingia mwaka mpya wa 2017, Mkoa wa Mbea wamekuwa wa kwanza kupokea kompyuta
zetu na tunaamini utaratibu huu utaendelea kwa mikoa nyingine kama
tulivyojipanga kuhakikisha kwamba tunapunguza changamoto za ukosefu wa kompyuta
kwa ofisi za serikali kwa sababu ni jambo la msingi na serikali haiwezi kufanya
kila kitu,” alisema Mercy.
No comments:
Post a Comment