Pages

Pages

Monday, November 28, 2016

Tamasha la Mtikisiko laacha gumzo jijini Mbeya

Mr blue akiwapagawisha wakazi wa Mbeya waliohudhuria katika  tamasha la Mtikisiko lililoandaliwa Na kampuni ya simu za Mkononi Tigo Tanzania, wakishirikiana Na Ebony Fm lililofanyika katika uwanja wa CCM Ruanda Nzowe(Shule ya Msingi Mwenge) mwishoni wa wiki iliyopita.

Wakazi wa Mbeya wameisifia sana tamasha la Mtikisiko lililoandaliwa Na kampuni ya simu za Mkononi Tigo Tanzania, wakishirikiana Na Ebony Fm lililofanyika katika uwanja wa CCM Ruanda Nzowe(Shule ya Msingi Mwenge).


Baada ya Tigo kudhamini tamasha la Fiesta katika mikoa 15, nakuibua vipaji vya chipukizi mikoani humo, Tigo waliendelea Na ahadi yao ya kupatia wanamuziki chipukizi jukwa la kuonyesha vipaji kwa kupitia tamasha la Tigo Mtikisiko, linaloratibiwa Na ebony fm katika nyanda za juu kusini.

Akiongea Na mwandishi wetu, msanii anaeibukia kwa kasi jijini Mbeya,,Zax 4Real alikuwa Na haya ya kusema "Ningependa kutoa shukrani kwa wadhimini wa Tamasha hili Tigo, kwa kuweza kunipa fursa hii ili niweze kuonyesha kipaji, Na naamini kila kampuni hapa nchini wakiiga mfano wa Tigo, basi tasnia ya mziki Tanzania itafika mbali."

Wawekezaji kutoka India waaswa

Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi.
Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya akizungumza wakati wa kongamano hilo kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye

Bayport yatoa msaada wa kompyuta za Sh Milioni 500 kwa Serikali

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga akikabidhi moja ya kompyuta zilizokabidhiwa na Taasisi yake kwa ajili ya serikali. Anayepokea ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imeipatia serikali msaada wa kompyuta 205 zenye thamani ya Sh Milioni 500 kwa ajili ya matumizi yao ya kiofisi, kwa kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga wa pili kutoka kushoto waliosimama, akipeana mkono na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mheshimiwa Angellah Kairuki baada ya kukabidhiwa kompyuta 205 na Taasisi ya Bayport, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Laurean Ndumbaro na Kaimu Katibu Mkuu Bi Susan Mlawi.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam, ambapo kompyuta 125 zitabaki Makao Makuu ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kompyuta 80 zilizosalia zitagawanywa na Wizara yenyewe kwa kuangalia mahitaji ya ofisi zao.
Baadhi ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia halfa ya makabidhiano ya kompyuta kutoka kwa Taasisi ya Bayport Financial Services.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema msaada wa kompyuta hizo zinatokana na kiu yao kubwa ya kushirikiana na serikali kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa ajili ya kufanikisha huduma bora kwa Watanzania.

Alisema taasisi yao ilipanga wamalize mwaka kwa kukabidhi kompyuta kwa ofisi za serikali, ikiwa ni mwendelezo wa kusherehekea miaka 10 ya huduma zao tangu Bayport ilipoanzishwa mwaka 2006 nchini Tanzania.

Saturday, November 26, 2016

Wadau wanavyoelezea kifo cha Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro

By Godfrey Dilunga, Dar es Salaam
Asante Bwana Mdogo wa Mwl. Nyerere,
Komandoo Fidel Alejandro Castro Ruz
PUMZIKA Komandoo Fidel Alejandro Castro Ruz, Waziri Mkuu wa kwanza wa Cuba ambaye pia ni Rais wa Kwanza wa Taifa hilo. Komandoo uliyenusurika kuuawa mara 638 na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA). Na moja ya jaribio lililoshindwa ni lile la kukuua kwa kutumia unga wa sumu uliowekwa kwenye sigara ulizokuwa unapenda kuvuta. Majaribio makubwa manane ya kukuua yanatajwa kufanyika dhidi yako Fidel kati ya mwaka 1960 na 1965.

Fabian Escalante, jasusi mstaafu wa Cuba aliyepata kuwa mlinzi wako ewe Fidel anaamini CIA walifanya majaribio hayo 638 ya kukuua, japokuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa CIA, Richard Helms, Machi 5, mwaka 1972, alikanusha CIA kuhusika iwe moja kwa moja au kupitia mawakala wa shirika hilo lenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi zake kwa siri mno.
Majaribio yote ya mauaji dhidi yako Fidel yalishindika lakini, sasa, kwa mapenzi ya Mungu, Fidel umeondoka duniani. Pengine unakwenda kukutana na kaka yako, kwa umri wa kuzaliwa, Julius Nyerere. Naam, Nyerere ni mkubwa kwako Fidel kwa miaka minne hivi – hili unalijua vyema na nchi zenu (CUBA na TANZANIA) zilikuwa marafiki wakubwa.

Fidel kawasalimie magwiji wenzako waanzalishi wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande wowote (Non-Aligned Movement - NAM), umoja mliouasisi mkiwa viongozi wa nchi tano kule Belgrade mwaka 1961, katikati ya kilele cha kelele za vita baridi chini ya Urusi kwa upande mmoja na Marekani kwa upande mwingine.

Heshima nyingi kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa India, Jawaharlal Nehru; Rais wa kwanza wa Indonesia, Sukarno; Rais wa Pili wa Misri, Gamal Abdel Nasser; Rais wa kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah na aliyekuwa Rais wa Yugoslavia, Josip Broz Tito. Pumzika, Fidel, bwana mdogo wa Mwalimu Nyerere, shujaa katika safu ya mstari wa mbele vitani, kinara katika kupinga ubepari wa mabepari - mwanamapinduzi wa kweli, salaamu pia kwa Hugo Chavez.

Nani asiyejua kwamba Cuba ndio nchi mahiri duniani katika matibabu? Nani asiyejua Cuba ndio kisiwa cha madaktari bingwa na mahiri duniani? Diego Armando Maradona – mwanasoka aliyevuma mno duniani, anajua hili, na alifika Cuba kwa matibabu wakati fulani, licha ya kuwa na fedha nyingi za kumwezesha kupata matibabu nchi za Ulaya.

Fidel, bwana mdogo wa Mwalimu Nyerere, nimepata kusikia sauti yako ikitamka kile kilichoitwa Azimio la Havana la mwaka 1979. Katika azimio hilo uliweka bayana mantiki ya kuanzishwa NAM kwamba ni kupigania na kulinda hadhi ya uhuru wa mataifa wanachama (national independence & sovereignty) dhidi ya ukandamizaji wa aina yoyote. Buriani Komandoo Kijeshi na Komandoo wa dunia ya wanyonge

Kiwanda cha cement cha Simba Cement chajenga madarasa mawili Kange, jijini Tanga


Tanga, KIWANDA Cha Saruji Cha Simba Cement kimeijengea shule ya Msingi ya Kange vyumba viwili vya madara na madawati 50 pamoja na matundu mawili vya vyoo vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.

Msaada huo umekuja kupunguza kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na wengine kukaa chini jambo ambalo hupunguza ufahamu wa wanafunzi darasani.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, alisema msaada huo uwe mfano kwa makampuni mengine na wadau wa elimu lengo likiwa ni kuondokana na changamoto ya  baadhi ya shule inazokabiliana nazo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Rasilimali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cment, Anna Malambugi, alisema kiwanda hicho moja ya sera zake ni kusaidia  jamii ikiwemo, Elimu, Afya na Mazingira.


Nae Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Debora Danniel, alisema awali walikuwa wakiwaweka wanafunzi 120 darasa moja kufuatia uhaba wa madarasa. 
Alisema kwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na kuwaomba wadau wa elimu kuisaidia shule hiyo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu yamaji na uchakavu wa majengo.                            

Tuesday, November 22, 2016

Mkuu wa Wilaya Kinondoni aagiza mratibu wa TASAF Kinondoni kutumbuliwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi pichani, amemuagiza Murugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kumvua madaraka Mratibu wa TASAF wa wilaya hiyo Onesmo Kweyamba kutokana ni kasoro mbalimbali zilizosababishs upotevu wa fedha za serikali kwa kuwapatia kaya ambazo hazikustahili kupewa kupitia mradi wa TASAF.
Aidha, wawakilishi 537 wa kaya wamemelipwa kiasi cha Shilingi 266,008,000/= huku wahusika waliokua wakipokea pesa hizo kushindwa kujulikana makazi yao yalipo baada ya uhakiki kufanyika. 

Ulipaji wa watu hao umeelezwa kusimamishwa hadi uhakiki mwingine utakapofanyika kwa kushirikisha vyombo vya dola na kubainisha zilipo kaya hizo ili kujua kama zina sifa za kupewa fedha hizo au la. Baadhi ya waliokuwa wakilipwa fedha hizo za kaya masikini ni pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali, sekta binafsi na watu wenye biashara mbalimbali zinazowaingizia kipato kinyume na masharti ya TASAF.


Aidha, wananchi wote wasio na sifa ambao wamekua wakipokea fedha hizi, watawajibika kuzirejesha zote." Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameagiza wananchi wote ambao wana sifa za kupatiwa ruzuku hiyo ya TASAF waingizwe kwenye orodha baada ya wale wasiostahili kuondolewa. Hapi ameagiza hatua nyingine za uchunguzi na nidhamu kwa mujibu wa sheria kuanza mara moja dhidi ya aliyekua mratibu.


Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi Mh.Hapi amesema fedha taslimu kiasi cha milioni 180,323,000/= zililipwa kwa kaya 515 ambazo hazikua na sifa za kulipwa kulingana na sifa zilizoainishwa huku wananchi wenye sifa wakiachwa.
Hapi amesema, jumla ya kaya 1397 zimebainika kuwa na upungufu wa sifa za kupatiwa fedha hizo za mradi wa TASAF katika wilaya ya Kinondoni na hivyo kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha.
Mkuu huyo wa wilaya ameagiza vyombo vya dola wilayani Kinondoni kuanza uchunguzi mara moja dhidi ya wale wote walioshiriki kuhujumu fedha za serikali na kufanya udanganyifu huo kwa awamu saba tofauti za malipo yaliyofanyika tangu July, 2015. "Nimeagiza vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili kubaini udanganyifu wote uliofanyika, na wahusika wote wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

TANAPA na wadau wa usafiri wa anga kukuza utalii Tanzania

Ndege ya shirika la Precision Air ikiwa tayari imetua katika uwanja wa Seronera ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoa wa Mara ikiwa na watalii 43 kutoka nchi Afrika Kusini iliyowachukua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere hatua inayoelezwa kuokoa muda na kupunguza gharama.

Abiria wakishuka kutoka kwenye ndege ya Shirika la Precision Air ambayo imeanza safari za moja kwa moja kutoka jijini Dar es Salaam na Zanzibar hadi kwenye hifadhi hiyo.

Mzazi anayedaiwa laki tatu Muhimbili aruhusiwa

Mzazi Sakina Lembo

Na Dotto Mwaibale

MZAZI Sakina Lembo (26) mkazi wa Mbagala Kibonde Maji ambaye alizuiliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  (MNH), kutokana na deni la sh. 338,257 baada ya kufanyiwa oparesheni ya uzazi uongozi wa hospitali hiyo umemruhusu kuondoka bila ya masharti yoyote.

Akizungumza wakati akitoka hospitali hapo baada ya kuruhusiwa mama yake na Sakina, Edith Chausa alisema analishukuru gazeti la Jambo Leo kwa kutaoa taarifa hiyo ambapo wahusika wameona na kuchukua uamuzi wa kumruhusu binti yake kuondoka hospitali na mtoto wake bila ya masharti yoyote" alisema Chausa.

Alisema kabla ya kuchukua uamuzi wa kwenda kwenye vyombo vya habari waliomba kuondoka na mzazi huyo lakini walikataliwa kwa kuambia mpaka alipe deni hilo ambalo hawakuwa na uwezo wa kulipa.

"Baada ya kutoka taarifa hii kwenye vyombo vya habari amekuja wodini mkurugenzi wa Muhimbili na kuchukua maelezo kwa binti yangu huku akilalamika kuwa mbona hatukusema kama hatukuwa na fedha badala yake tumewashitaki kwenye vyombo vya habari" alisema Chausa.

Chausa alisema binti yake na mtoto waliruhusiwa kuondoka hospitali hapo saa saba mchana na kuwa hali ya mtoto na mama yake inaendelea vizuri.

Chausa ameiomba serikali kuangalia suala zima la wakina mama wanokwenda kujifungua kulipishwa kiasi kikubwa cha fedha kwani. 

Mafunzo ya biashara ya vijana yafanyika jijini Dar es Salaam

 Mkufunzi Linus Gedi, akiendesha mafunzo ya Biashara kwa Vijana kuhusu, Fursa za Vijana na Taratibu, Sheria za kufanya Biashara ndani ya Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, yanayoendelea kwa siku ya pili leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo ya siku tano yalifunguliwa jana Nov 21 na yanatarajia kumalizika Nov 25. 
  Mkufunzi Linus Gedi, akiendesha mafunzo ya Biashara kwa Vijana kuhusu, Fursa za Vijana na Taratibu, Sheria za kufanya Biashara ndani ya Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, yanayoendelea kwa siku ya pili leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo ya siku tano yalifunguliwa jana Nov 21 na yanatarajia kumalizika Nov 25. 

Friday, November 18, 2016

Baraza la Watoto mkoani Mwanza laeleza mazito


Msimamizi wa Watoto Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Karus Masinde, akizungumza na BMG.
Na George Binagi-GB Pazzo
Baraza la Watoto mkoani Mwanza, umetoa rai kwa wanajamii kuepuka vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto kwani vitendo hivyo husababisha watoto kutofikia malengo yao maishani.


Hivi karibuni msimamizi wa baraza hilo ambalo liko chini ya shirika la Mwanza Youth and Children Networ (MYCN), Karus Masinde, aliiambia BMG kwamba ukatili wa watoto ikiwemo ukatili wa kingono na vipigo husababisha watoto wengi kuyakimbia makazi yao na hivyo mwelekeo wa maisha yao pia kutoweka.

Tamasha la Tano la watu wenye ulemavu lafikia tamati jana jijini Dar es Salaam

 Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la  ‘The Foundation For Civil Society’ Nasim Losai, akitoa mada wakati wa ufungaji wa Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemavu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limefungwa hii leo hayo. 
 Mkufunzi Mwelekezi, Salma Maoulid, akisimamia zoezi la maswali na majibu wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemavu lililoanza jana kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uchumi Mwandamizi, Mchambuzi na Mipango, Andrea Aloyce, akitoa mada kwa washiriki wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemabu lililoanza Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Thursday, November 17, 2016

Mchakato wa ndege za Saudi Arabia na Tanzania waanza kusukwa

*Ni matokeo ya kikao kati ya balozi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu Saudi Arabian Airline
*Vivutio vingi vya utalii nchini Tanzania vyatajwa kwenye kikao hicho cha aina yake
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser, katika kikao chao maalum cha kujadili namna ya ndege za shirika hilo kuanza safari za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania. Picha zote kwa Hisani ya Ofisi ya Balozi wa Tanzania Saudi Arabia.


Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia
WATALII, wafanyabiashara, mahujaji wa Watanzania pamoja na watu kutoka nchi za Kiarabu hususan Saudi Arabia, huenda wakapata fursa ya kuwasili Tanzania kwa urahisi endapo mchakato Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines wa kutoa ndege za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania utakapofanikiwa kama ulivyoanza kushughulikiwa.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser kushoto. 
Mapema wiki hii Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser, ambapo shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vya Tanzania vilijadiliwa, kama njia ya kuangalia namna bora ya ndege hizo kufanya safari zake vizuri kwa kuzingatia mkataba wa ushirikiano wa mambo ya anga baina ya Tanzania na Saudi Arabia Bilateral Air Service Agreement (BASA).

Wednesday, November 16, 2016

Rais Mstaafu Dr Jakaya Kikwete atunuku digrii ya awali DUCE

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha  Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali.

Digrii walizotunukiwa ni Elimu ya Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii (B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science) wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190. Picha kwa hisani ya Richard Mwaikenda.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuwatunuku digrii ya awali ya elimu ya jamii  na ualimu  wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo jioni. Jumla ya wanafunzi 864 walitunukiwa digrii hiyo.

Chadema mkoani Mbeya waingia kwenye mgogoro wa viongozi na madiwani



Na Mwandishi Wetu, Mbeya.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Wilaya ya Mbeya mjini, kimeingia kwenye mgogoro baina ya viongozi  na madiwani.

Mgogoro huo, ambao unatajwa  kujikita zaidi kwenye maslahi binafsi ya watu, huenda ukakiathiri chama hicho kwa kutengeneza mpasuko, kama uongozi wa juu hautachukua hatua za haraka.

Chanzo cha mgogoro huo,unadaiwa umetokana na viongozi wa chama hicho kujaribu kutengeneza mazingira ya kuwafuta uanachama baadhi ya madiwani kutokana na mienendo ya utendaji kazi wao kutoridhisha.



Inatajwa kuwa chama hicho, hakikuridhishwa na utendaji kazi wa madiwani hao hivyo kuwaandikia barua  yenye kumbu kumbu namba CDM/MBY/11/2016/41 iliyosainiwa na Kaimu Katibu Raphael Mwaitege inayowataka  kuhudhuria mkutano mkuu wa wilaya mbeya mjini.



Pia,Madiwani  wote wametakiwa kutoa  maelezo ni kwa nini hawakuudhulia kikao kilichopita cha tarehe 28/9/2016, kushindwa kushiriki shughuli za kijamii kama vile misiba, kutaja idadi ya vikao vya baraza walivyoshiriki pamoja michango ya kifedha waliyokichangia  chama.



Mratibu wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini(CHADEMA), Franky Mwaisumbe, amesema ofisi baada ya kupokea taarifa hiyo iliunda tume ili kufanya uchunguzi wa madai hayo na kwamba imeanza kufanya kazi  November 14, mwaka huu.



Kazi kubwa itakayofanywa na tume hiyo ni  kuwaita na kuwahoji madiwani wanaotuhumiwa, kuwahoji wananchi juu ya utendaji kazi wa madiwani wao.



Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Obadia Mwaipalu alipohojiwa kuhusu mkanganyiko huo, alikana taarifa za chadema Wilaya kuwaandikia madiwani hao barua kwa lengo la kutaka kuwahoji na kwamba hakuna mgogoro ndani ya chama hicho.



Huku hayo yakiendelea kwa upande wa uongozi, baadhi ya madiwani  wameeleza kusikitishwa na hatua za viongozi wa chama ngazi ya Wilaya kujikita katika kutengeneza migogoro ndani ya chama badala ya kuwapa woa nafasi ya kuwatumikia wananchi ambao ndio waliofanikisha kuiweka chadema madarakani na kushika halmashauri.



Wamesema, ni mambo mengi yamekuwa yakifanywa na uongozi wa juu wa Wilaya ambayo yamekuwa hayana ustawi mzuri kwa ndani ya chama.



“Kunaviongozi wamefika mahala, wamekuwa wakidiriki hata kuwatukana kwa kuwarushia matusi ya nguoni madiwani viti maalum  na ukiuliza sababu huioni, ukiacha hilo viongozi hao wamekuwa wakiwashawishi wenyeviti wa serikali za mitaa kufanya maandamano wakitaka Meya ajiuzulu kutokana na kushindwa kushughulikia posho zao,”kilisema chanzo cha habari hii.



Sasa ukiangalia posho za wenyeviti zinahusisana nini na meya…. kwani licha ya suala lao kushughulikiwa na mkurugenzi wa halmashauri lakini bado viongozi hao wameendelea kutengeneza malumbano yasiyokuwa na tija.



Tunafahamu kinachotakiwa hapa ni nafasi ya Umeya na si kingine  lakini ni vema taratibu zikafuatwa kuliko kutengeneza skendo zisizokuwa na maslahi kwa chama na kwa wananchi kwa ujumla.

Monday, November 14, 2016

Leo Novemba 14 ni Siku ya Kisukari Duniani 2016

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Ugonjwa wa Kisukari ni tatizo linalopamba moto hapa nchini kwetu. Takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa kulikuwa na jumla ya wagonjwa 822,880 wa kisukari.
Waziri wa Afya pichani Mheshimiwa Ummy Mwalimu pichani.
Utafiti uliofanywa mwaka 2012 katika Wilaya 50 nchini ulionyesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 - 64 wana ugonjwa wa kisukari. Hii inamaanisha kuwa katika kila watu wazima 100 Tanzania, watu 9 wana ugonjwa wa kisukari!
Kwa upande wa watoto wenye kisukari takwimu za 2015 zinaonyesha ni kati ya asilimia 15 - 20 ya wagonjwa wote wa kisukari ambao wanatibiwa kwenye klinik nchini. Wagonjwa wengi hawajitokezi kwenye klinik kwa sababu mbalimbali ikiwemo imani potofu, ukosefu wa elimu juu ya tatizo hili, gharama pamoja na umbali wa huduma za afya zilipo.
Watu wengi hawajitambui kama wana ugonjwa huu. Wengine wanakuwa na dalili lakini hawachukui hatua mapema. Dalili za kisukari ni rahisi kuzitambua. Nazo ni: kiu isiyoisha, kukojoa mara kwa mara, kupungua uzito, kusikia njaa kila wakati na mwili kukosa nguvu. Ukiwa na dalili mojawapo kati ya hizi, wapi Hospitali ukapime sukari.
Yapo mambo kadhaa yanayopelekea watu kupata ugonjwa wa kisukari ikiwemo Ulaji Usiofaa, Kutofanya Mazoezi ya mwili, Matumizi ya Pombe kupita kiasi na Matumizi ya Tumbaku. Hebu sasa tufumbue macho zaidi kwamba kisukari ni tatizo na kila mmoja wetu aongeze nguvu katika kuhakikisha kuwa anajikinga na ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo;-

Airtel, VETA kuendesha masomo kwa njia ya simu ya mkononi

Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA Eng, Lucius mwishoni mwa  wiki akizungumza na baadhi ya walimu na wanafunzi  VETA kuhusu mfumo wa masomo kwa njia ya simu za mkononi wa VSOMO ambapo zaidi ya vijana  28 elfu  wamejiandikisha ili kusoma kwa mtandao wa VSOMO. Mkuu huyo pia amesema ndani ya miezi miwili chuo chake kitaongeza kozi zingine 10 ili wanafunzi wanaozipenda waanze kusoma.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel wakishirikiana na VETA wameanza kuona mafanikio ya mfumo wa Masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kwa njia ya simu za mkononi ujulikanao kama VSOMO ambapo tayari umefanikiwa kupokea maombi na kuaandikisha vijana  zaidi ya elfu ishirini na nane  kuomba kusoma kozi za VETA kwa njia ya simu za Airtel toka ulipozindiliwa mwaka huu mwezi mei.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa hafla fupi ya kueleza mafanikio ya mfumo wa VSOMO iliyofanyika katika Ukumbi wa VETA kipawa Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA Eng, Lucius Luteganya alisema “Airtel na VETA baada ya kuanzisha mfumo wa VSOMO yaani masomo kwa njia ya simu za mkononi na kupeleka taarifa katika vituo vya VETA vilivyopo katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Dar es salaam, Arusha na Mbeya, leo hii zaidi ya vijana  28 elfu  wameshajiunga na mtandao wa VSOMO kwa lengo la kutaka kuanza kusoma, hii inaonyesha kuwa mfumo huu wa kusoma kwa njia ya simu umekubalika na pia kunauhitaji mkubwa wa vijana kutaka kusoma VETA”

Thursday, November 10, 2016

Madarasa matatu ya Bayport kwa EOTF yamkuna DC wa Kibaha


Mkuu wa Wilaya Kibaha, Mheshimiwa Assumpter Mshama, akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya majengo ya madarasa matatu yaliyojengwa na Taasisi ya Bayport Financial Services kwa ajili ya Kituo cha Kibaha Children Village Centre jana, wilayani humo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Assumpter Mshama, amekunwa na majengo ya madarasa matatu ya kisasa na ofisi ya walimu yaliyojengwa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kwa ajili ya msaada wa kituo cha kulea watoto yatima cha Kibaha Children Village Centre (KCVC) chenye mpango wa kuanzisha shule.
Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga  akizungumza katika halfa ya kukabidhi majengo iliyojenga kwa ajili ya kituo cha KCVC.

Majengo hayo yaliyojengwa wilayani Kibaha, yamekabidhiwa jana na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwamo DC Kibaha, aliyeambatana na watumishi kadhaa wa ofisi yake na wale waliotoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani wanaohusiana na elimu.
Watoto wa Kituo cha Watoto yatima cha KCVC wakiimba.
Akizungumza jana katika makabidhiano hayo yaliyopokewa kwa furaha, DC Mshama, alisema hajatarajia kwamba angekuta majengo bora na yenye kuvutia maalum kwa watoto yatima na wale watakaofanikiwa kusoma katika kituo hicho, hususan wale wanaotoka maeneo ya karibu na kituo hicho.

Alisema kwamba Bayport wamefanya mambo ya kiungwana na yanapaswa kuungwa mkono na taasisi zote ili kuhakikisha watoto yatima na Watanzania kwa ujumla wanaishi vizuri kwa kupata haki zao za msingi.

Picha za baadhi ya Madaktari Bingwa watakaowasili Tanzania Nov 11 kutoka Saudi Arabia

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza kushoto, akishuhudia Viongozi wa Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY nchini hapa wakisoma ramani ya Tanzania katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh, ili kuifahamu vizuri Tanzania na maeneo watakayofikia katika msafara wao wa kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma za afya bure kwa siku 10 kwenye Hospitali za Chake Chake na Wete. Picha na Mpiga Picha Wetu, Riyadh.   
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akiwa na viongozi wa Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY ambao walifika Ubalozini mjini Riyadh kujitambulisha na kukamilisha taratibu za safari kuingia Tanzania. Madaktari hao wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Novemba 11.

Wednesday, November 09, 2016

Madaktari Bingwa 17 wa Saud Arabia kutua Zanzibar Nov 11

Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia
JOPO la Madaktari Bingwa 17 kutoka nchini Saudi Arabia, wanatarajiwa kuwasili Zanzibar Novemba 11  kwa ajili ya kuweka kambi ya kutoa matibabu (Medical Camp)  katika Hospitali za Chake Chake na Wete kwenye Kisiwa cha Pemba. 
Balozi Hemed Mgaza kushoto alipokwenda kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Dkt Mohamed Ali Shein akiwa nchini Tanzania. Picha na Maktaba.
Programu hii inaratibiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu ya Saudi Arabia World Assembly of Muslim Youth – WAMY kwa ajili ya kwenda nchini Tanzania katika kisiwa cha Pemba kutoka huduma hiyo ya afya.

Akizungumza mjini hapa, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Hemed Mgaza, alisema kwamba msafara wa madaktari hao utakuwa na tija kwa Watanzania wote, hususan wa Kiwa cha Pemba.

Alisema kwamba taratibu zote za madaktari hao zimekamilika, huku ratiba yao ikionekana kwamba watahudumia kuanzia Novemba 11 hadi 22 kabla ya kuekea na ratiba zao ambapo ni jambo la kujivunia kwa wataalam hao kuamua kwenda nyumbani Tanzania kutumia taaluma zao.

“Madaktari hao watatoa huduma ya matibabu kwa muda wa siku kumi bila malipo kuanzia tarehe 11 hadi 22 mwezi Novemba, 2016 kama taarifa za msafara wao zinavyoonekana katika ofisi zetu.

“Pamoja na kutoa huduma za matibabu, Madaktari hao watakwenda na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo mwisho wa kambi hiyo watavitoa msaada kwenye hospitali hizo,” alisema.

Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, ujio wa madaktari hao ni wa mara ya kwanza nchini Tanzania na wanatarajia kutoa huduma hizo sehemu nyingine za Tanzania siku zijazo baada ya kukamilisha awamu ya kwanza, huku madaktari hao wakiwa wameshatoa huduma kama hizo katika nchi za Comoro,  Cameroon na kwingineko.

Tuesday, November 08, 2016

Mwili wa marehemu Samuel Sitta kuletwa Alhamisi jioni

Mwili wa marehemu Samuel Sitta utaingia toka Ujerumani alhamisi jioni, na utahifadhiwa nyumbani Masaki, na Ijumaa saa 3 asubuhi tutaaga pale karimjee kwa ibada itakayoongozwa na Askofu Malasusa na Mch Mwaipole wa KKKT Kinondoni na saa sita kamili utaelekea Dodoma kwa Ndege na saa 8 wabunge wataaga, na saa kumi jioni utaelekea Tabora, na jumamosi mchana mazishi yatafanyika Urambo.

Kampeni ya TUNAWEZA yaendelea kushika kasi

Katibu Tawala wa Mko wa Dar es Salaam, Theresia Mbando, akizungumza wakati akifungua rasmi Mafunzo ya Kampeni ya awamu ya tatu ya 'TUNAWEZA' lenye lengo la kuondoa aina zote za Ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake, yaliyofanyika leo Nov 8, 2016 kwenye Hoteli ya Jamirex iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam,leo.  Kushoto ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Rehema Msami, kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC).
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa bize kunakili kile anachokiwasilisha Katibu Tawala wakati wa ufunguzi huo.