Pages

Pages

Monday, November 14, 2016

Airtel, VETA kuendesha masomo kwa njia ya simu ya mkononi

Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA Eng, Lucius mwishoni mwa  wiki akizungumza na baadhi ya walimu na wanafunzi  VETA kuhusu mfumo wa masomo kwa njia ya simu za mkononi wa VSOMO ambapo zaidi ya vijana  28 elfu  wamejiandikisha ili kusoma kwa mtandao wa VSOMO. Mkuu huyo pia amesema ndani ya miezi miwili chuo chake kitaongeza kozi zingine 10 ili wanafunzi wanaozipenda waanze kusoma.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel wakishirikiana na VETA wameanza kuona mafanikio ya mfumo wa Masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kwa njia ya simu za mkononi ujulikanao kama VSOMO ambapo tayari umefanikiwa kupokea maombi na kuaandikisha vijana  zaidi ya elfu ishirini na nane  kuomba kusoma kozi za VETA kwa njia ya simu za Airtel toka ulipozindiliwa mwaka huu mwezi mei.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa hafla fupi ya kueleza mafanikio ya mfumo wa VSOMO iliyofanyika katika Ukumbi wa VETA kipawa Mkuu wa Chuo cha Ufundi VETA Eng, Lucius Luteganya alisema “Airtel na VETA baada ya kuanzisha mfumo wa VSOMO yaani masomo kwa njia ya simu za mkononi na kupeleka taarifa katika vituo vya VETA vilivyopo katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Dar es salaam, Arusha na Mbeya, leo hii zaidi ya vijana  28 elfu  wameshajiunga na mtandao wa VSOMO kwa lengo la kutaka kuanza kusoma, hii inaonyesha kuwa mfumo huu wa kusoma kwa njia ya simu umekubalika na pia kunauhitaji mkubwa wa vijana kutaka kusoma VETA”


Eng, Lutejanya alisema kuwa “Kwa vijana wote ambao tayari wameshapakua aplikesheni ya VSOMO katika simu zenu sasa ivi wanaweza kuchagua kozi na kuanza kusoma papo hapo popote walipo mara tu baada ya kulipia, kozi zilizopo sasa tayari kwa kusoma ni kozi ya Umeme wa nyumbani, kuchomelea, ufundi wa pikipiki, maswala ya urembo, kutengeneza aluminum, pamoja na ufundi simu”

“Baada ya kuona ongezeko la vijana kujisajili na huduma hii ya VSOMO tayari tumewasiliana na baadhi ya vijana kwa kushirikiana na mdhamini wa mradi huu Airtel ili kubaini kozi wanazotaka, hivyo basi tumeshazijua na tumejipanga ndani ya miezi miwili kuanzia sasa tutapandisha kozi zingine 10 kwenye mfumo wetu wa VSOMO ili vijana wote waliojiandikisha waweze kuchangua kozi wanazotaka” alieleza  Eng, Luteganya.


Mradi wa VSOMO uko chini ya mradi wa kijamii wa Airtel FURSA ukiwa na lengo la kuwasaidia vijana kuweza kujisomea kozi za ufundi  stadi ili kujipatia ajira za uhakika.  Mradi wa VSOMO ulibuniwa kwa ushirikiano kati Airtel na Mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)  hivyo kufanya simu ya mkononi kuwa Darasa.

No comments:

Post a Comment