Pages

Pages

Monday, November 14, 2016

Leo Novemba 14 ni Siku ya Kisukari Duniani 2016

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Ugonjwa wa Kisukari ni tatizo linalopamba moto hapa nchini kwetu. Takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa kulikuwa na jumla ya wagonjwa 822,880 wa kisukari.
Waziri wa Afya pichani Mheshimiwa Ummy Mwalimu pichani.
Utafiti uliofanywa mwaka 2012 katika Wilaya 50 nchini ulionyesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 - 64 wana ugonjwa wa kisukari. Hii inamaanisha kuwa katika kila watu wazima 100 Tanzania, watu 9 wana ugonjwa wa kisukari!
Kwa upande wa watoto wenye kisukari takwimu za 2015 zinaonyesha ni kati ya asilimia 15 - 20 ya wagonjwa wote wa kisukari ambao wanatibiwa kwenye klinik nchini. Wagonjwa wengi hawajitokezi kwenye klinik kwa sababu mbalimbali ikiwemo imani potofu, ukosefu wa elimu juu ya tatizo hili, gharama pamoja na umbali wa huduma za afya zilipo.
Watu wengi hawajitambui kama wana ugonjwa huu. Wengine wanakuwa na dalili lakini hawachukui hatua mapema. Dalili za kisukari ni rahisi kuzitambua. Nazo ni: kiu isiyoisha, kukojoa mara kwa mara, kupungua uzito, kusikia njaa kila wakati na mwili kukosa nguvu. Ukiwa na dalili mojawapo kati ya hizi, wapi Hospitali ukapime sukari.
Yapo mambo kadhaa yanayopelekea watu kupata ugonjwa wa kisukari ikiwemo Ulaji Usiofaa, Kutofanya Mazoezi ya mwili, Matumizi ya Pombe kupita kiasi na Matumizi ya Tumbaku. Hebu sasa tufumbue macho zaidi kwamba kisukari ni tatizo na kila mmoja wetu aongeze nguvu katika kuhakikisha kuwa anajikinga na ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo;-

Tuepuke usiofaa kwa vyakula vyenye mafuta mengi, vyakula vyenye chumvi nyingi, sukari nyingi, nk, huku watu wakitakiwa kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka matumizi ya pombe kupita kiasi na matumizi ya tumbaku.
Nitoe wito kwa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anapima afya yake mara kwa mara ili kutambua hali yako ya afya. Endapo utatambuliwa kuwa una ugonjwa wa kisukari basi tumia huduma za afya kulingana na ushauri utakaopewa na wataalam wa afya.
Jambo kubwa litakalofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kutoa Elimu kwa wananchi juu ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kisukari sambamba na kuboresha upatikanaji wa huduma za matibabu ikiwemo dawa. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kuna kliniki za kisukari hadi katika ngazi ya Vituo vyote vya Afya.
Tuhakikishe tunapima afya zetu kutambua kama tuna tatizo la kisukari au la.

No comments:

Post a Comment