Pages

Pages

Friday, September 30, 2016

TEGETA ESCROW yamtisha Profesa Anna Tibaijuka

 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
MBUNGE wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000 alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya  Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.

Tuzo hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalme Khalifa bin Al Khalifa.

Wateja wa viwanja vya Bayport Kilwa waanza kupewa hati

Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed katikati akimkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao aliyenunua kiwanja cha Kilwa, Mubarack Kirumirah kulia. Kushoto ni Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATEJA wa viwanja vya Bayport Financial Services wilayani Kilwa, mkoani Pwani wameanza kupewa hati zao kutoka mradi wa Kilwa Msakasa unaoendeshwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo, huku ikiwa na dhamira ya kuwakwamua wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Mradi wa Kilwa Msakasa ni miongoni mwa miradi kadhaa inayoendeshwa na taasisi hiyo ikiwamo Bagamoyo, Vikuruti, Kigamboni na Kibaha na kujikita kurahisisha pia utoaji wa hati kwa wateja wao waliokamilisha utaratibu rahisi wa malipo ya viwanja hivyo.



Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano, Mercy Mgongolwa, alisema kwamba kuanza kutolewa kwa hati za mradi huo wa Kilwa ni sehemu ya mwendelezo wa kuboresha huduma zao za mikopo ya viwanja inayotolewa sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Mteja wa Bayport Financial Services, Mubarack Kirumirah kulia akitia sahihi kabla ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Kilwa. Anayeshuhudia ni Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed.

Thursday, September 29, 2016

Maalim Seif anywea kutinga Buguruni kesho na watu wake

KUAHIRISHA MAPOKEZI YA VIONGOZI SIKU YA KESHO.
Kwa niaba ya Wabunge wote wa CUF napenda kuwajulisha wanachama wa CUF walioko Dar Es Salaam kwamba tumeahirisha mapokezi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la CUF, Kamati ya Uongozi ya chama na Katibu Mkuu tuliyopanga kuyafanya kesho Ijumaa saa 2.00 asubuhi kwenye Ofisi Kuu ya CUF Buguruni.
Tumefanya uamuzi huu baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama wa wanachama watakaohudhuria na viongozi watakaopokelewa siyo nzuri.
Tunazo taarifa kuwa yapo makundi hatari ya watu yanayoishi ndani ya Ofisi huku yakilindwa na vyombo vya dola tangu Ofisi hiyo iporwe na aliyewahi kuwa mwanachama na kiongozi wa juu wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akishirikiana na watu wanaomuunga mkono.
Wakati tunaahirisha mapokezi ya kesho tunajipa muda wa kushauriana na viongozi wa juu wa chama chetu huku tukiwaomba wanachama wote walioko DAR, MIKOANI na ZANZIBAR wawe watulivu kwani chama na viongozi makini hawawezi kuwa tayari kuona maisha na usalama wa wanachana na viongozi vinahatarishwa kwa kuigeuza Ofisi Kuu kuwa uwanja wa mapambano (battle ground).
Imetolewa na
RIZIKI SHAHARI (MB),
KIONGOZI WA WABUNGE,
THE CIVIC UNITED FRONT,
9 Septemba 20
16

Tuesday, September 20, 2016

Ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL yatua nchini

Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.

Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).

Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).

Wakadiriaji majengo na wabunifu kunolewa kesho


Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi, Jehad A. Jehad (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu semina ya 26 siku moja itakayo washirikisha wadau wa Sekta ya  ujenzi itakayofanyika kesho kutwa Septemba 22, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa.

Na Dotto Mwaibale

BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi kesho kutwa inatarajia kuendesha semina ya siku moja kwa ajili ya kuwanoa wadau wa sekta ya ujenzi nchini.




Hayo yamebainishwa na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Jehad wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu semina hiyo muhimu itakayofanyika kesho kutwa ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere. "Semina hii ambayo ni ya 26  ni muhimu sana kwetu sisi watu wa sekta ya ujenzi hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linatutegema" alisema Jehad.
Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Utawala, Angelo Ngalla, Mwanasheria, Ibrahim Mohamed na Ofisa Uhusiano, Hamisi Sungura.

Monday, September 19, 2016

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro lawatunuku vyeo baadhi ya askari wake

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali waliotekeleza vyema majukumu yao.kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Wilbroad Mutafungwa.

Wingi wa mahabusu magerezani wazua gumzo nchini Tanzania

Mkurugenzi  wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf.

Na  Humphrey   Shao, Dar es Salaam
WITO umetolewa kwa wadau wa sheria  kusaidia kupunguza mahabusu Magerezani kutokana na wingi wao ambao aikuwa lazima kuweka humo .

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF),Joaquine De Mello,  wakati wa Hafla ya miaka mitano ya shirika hilo na kukabidhi fedha kwa mashirika mapya ya wanaufaika.

“nimeweza kuzunguka magereza yote nchini na kujionea namna gani wafungwa walivyojazana kwa wingi lakini robo tatu ya wafungwa waliopo humo ni mahabusu ambao awaja hukumiwa” alisema Jaji Joaquine De Mello.
 Wajumbe wa Bodi wa Legal Services Facility katika picha ya pamoja.

HUSSEIN MSOPA: Sharifu majini aliyejikita kuwaombea wenye matatizo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
“IKIWA hujawahi kupata tatizo huwezi jua kama wapo binadamu wenzetu wanaotabika kusaka dawa au vitu vinavyoweza kuwaondoshea maswahibu yao yanayoendelea kuwapa wakati mgumu katika maisha yao bila kuangalia wanaishi kwa mtindo gani,”. Ndivyo alivyoanza kusema Sheikhe Hussein Msopa maarufu kama Sharifu Majini.
Chifu Hussein Msoma maarufu kama Sheikhe Sharifu Majini akiwa katika majukumu yake ya kawaida kama anavyoonekana pichani.
Ndio, sheikhe huyo mwenye maskani yake Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, unaweza kushangazwa na idadi kubwa ya watu wanaotembelea katika ofisi ya sheikhe hiyo, huku kila mmoja wake akiwa na shida yake inayohitaji utatuzi. Kwa wale ambao hawajui lolote kuhusu sheikhe Sharifu majini, pindi wanapopita katika mtaa huo, wanaweza kudhani labda kuna harusi, msiba ayu shughuli yoyote ya kijamii kutokana na ingia tokay a watu katika nyumba ya sheikhe huyo inayotoa huduma mbalimbali za kuombea watu, kuwapatia dawa zikiwamo zinazohusiana na mambo ya majini.
Sheikhe Sharifu Majini pichani.
Watu wanaweza kushangaa au kujiuliza. Je, ni kweli mtu mwenye tatizo anaweza kupata ufumbuzi wa shida yake atakapomuona sheikhe huyo? Katika mazungumzo na mtandao huu yaliyofanyika wiki iliyopita, sheikhe Sharifu anasema kwamba amedhamiria kuwakomboa wale wenye mahitaji na matatizo yanayohusu majini, ukosefu wa uzazi kwa njia za ushirikiana, kusumbuliwa na majini pamoja na kuzitafsiri ndoto mbalimbali zinazohusiana na mifumo ya maisha ya mwanadamu. Sheikhe huyo anasema kwamba uamuzi wake wa kuamua kujihusisha na masuala hayo umetokana na kufahamu adha kubwa inayowakumba binadamu, jambo linalowafanya waishi kwa mashaka katika kipindi chote cha maisha yao.
“Mtu anaweza kwenda hospitali kufanya uchunguzi wa afya ya matatizo ya uzazi na kukuta hana tatizo lolote. Lakini kila anavyojitahidi ili ashike mimba kwa ajili ya kufurahisha nafsi au ndoa yake anajikuta anashindwa kufanikiwa.

Wednesday, September 14, 2016

Waimbaji 10 wa injili waingia fainali


Kikundi cha Makerubi kutoka Manyara ambao walijiandikisha wakitokea Temeke waliweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika shindano la Gospel Star Search 2016 kwa kuweza kuimba kwa ustadi mkubwa. Shindano la Nusu fainali lilifanyika katika viwanja vya Biafra - Kindononi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason blog.

Vijana 10 wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali katika shindano la kumtafuta mkali wa kuimba nyimbo za injili 'Gospel Star Search 2016' lililofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali alisema kuwa ni vyema vijana wakazingatia mafundisho yote waliyopatiwa na walimu wao ili waweze kushindana kwa uweledi na ustadi wa hali ya juu. Alisema wakati umefika wa vijana kutambua talanta au vipaji walivyopewa na mwenyezi Mungu ili viwaletee manufaa katika kumtangaza Bwana Yesu Kristo.

"Tokea tumeanza kuzunguka kukusanya vijana hakika tumeweza kupata vijana wengi wenye vipaji na kuonyesha kuwa mwamko wa vijana katika kutambua vipaji vyao umekuwa mkubwa, hakikuwa jambo jepesi sana ila yote kwa yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyeweza kufanikisha yote",  alisema Sasali.


Umati wa watu waliohudhuria shindano la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mshiriki namba 4. Grace Madole akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu hakuweza kupenya hatua ya fainali.
Mshiriki namba 5. Winnypraise William akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu alipenya kuingia hatua ya fainali.
Shindano la Gospel Star Search lilikuwa ni vuta nikuvute pamoja na mshiriki namba 6. Willansia Lema kuimba kwa hisia ila hakuweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ambayo iliweza kuingiza washiriki wapatao 10 na kufanya washirikiki watano (5) kuaga mashindano.
Mshiriki namba 10. Flora Kachema alifanikiwa kuingia fainali.
Majaji wa shindano la Gospel Star Search (GSS) kutoka kulia ni Mchungaji Sam Mwangati, Sarah Ndossi na Fred Msungu wakiwa wamenyanyuka kuonyesha heshima ya pekee kwa mshiriki ambaye aliweza kuvuta hisia zao.
Mshiriki Mdogo kuliko wote akiwa aliwavuta hisia majaji wakajikuta wanatoa heshima ya pekee kwa kusimama.
Wageni waliohudhuria shindano hilo wakifurahia kwa shangwe.
Nderemo na vifijo vilitawala.
Mshiriki huyo akiwa amewateka na kujikuta wakiimba kwa hisia wageni waliohudhuria.
Mshiriki Sunday Lunkombe alifanya vyema kuliko wenzake na kufanikiwa kuongoza hakua ya kuingia fainali kwa kujizolea alama nyingi.
Washiriki wakionyesha umahili wa kuimba pamoja kabla ya kutangazwa kumi bora.

Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano mkali.
Kiongozi wa Majaji, Mchungaji Sam Mwangati akisoma majina ya vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali ya shindano la Gospel Star Search 2016 lililofanyika katika uwanja wa Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Fainali za shindano hili zinatarajiwa kufanyika jumapili ya Septemba 18, 2016 katika ukumbu wa Milado, Sinza jijini Dar es Salam.

Aliongeza kuwa shindano la Gospel Star Search 2016 liliweza kupata  washiriki wengi ila wakafanyiwa mchujo na kupatikana wapatao 15 ambao  waliweza kuingia hatua ya nusu fainali na wakafanya mchuzo katika  viwanja vya Biafra wakapatikana 10 ambao wameingia katika kikaango na  ipatapo Septemba 18, 2016 Jumapili katika ukumbi wa Milado, Sinza ndipo  fainali zitakapofanyika.

Vijana 15 waliokuwa wameingia nusu fainali ni 1. Makerubi,  2. Enighenja Mmbaga, 3. Upendo John, 4. Grace Madole,   5. Winnypraise William, 6. Willansia Lema, 7. Rogate Kalengo, 8. Suleiman Wilson, 9. Innocent Eliya. Wengine ni 10. Flora Kachema, 11. Steve Njama, 12. Winnifrida Dudu, 13. Calvin John, 14. Sunday Lunkombe na 15. Beda Andrew.

Waliofanikiwa kuingia Fainali ni vijana 10 ambao ni 1. Makerubi, 2. Beda Andrew, 3. Winnypraise William, 4. Rogate Kalengo, 5. Suleiman Wilson, 6. Flora Kachema. Wengine ni 7. Steve Njama, 8. Winnifrida Dudu, 9. Calvin John na 10. Sunday Lunkombe.

Shindano la GSS limedhaminiwa na Maendeleo Bank,  Grace Product, Brand exponetial, Kiango media, Clouds Media Group, Fm studios (Faith music lab) na 3D. 

Mkiuu wa wilaya Same awapa tano wamasai wilayani kwake



Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akisikiliza kwa makini maelezo ya mmoja ya wazee wa kabila la Kimasai kuhusu umuhimu wa elimu katika maeneo hayo.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule amewapongeza baadhi ya vijana wa kimasai kwa kuachana na imani potofu na hatimaye kuanza kumwabudu Mungu kwa kuhudhuria Misa mbalimbali katika makanisa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu huyo wa Wilaya hiyo wakati wa sherehe maalumu kwa waliokuwa vijana wa Kimasai (Morani) kuingia hatua kubwa ya uzeeni na ya heshima katika kabila hilo.


 Sherehe hiyo ilifanyika katika uwanja wa Kitongoji cha Endevisi, Kijiji cha Emuguru na ibada hiyo kuongozwa na Mchungaji Joshua Laiser kutoka kanisa la Kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) Wilaya ya Hai Dayosisi ya Moshi na Mchungaji Andrea Sangolo wa Usharika wa Bonde la Ruvu Same na baadaye kufuatiwa na shughuli za kutoa Baraka kwa vijana hao zoezi lililofanywa na viongozi wa dini, Serikali na Wazee wa Mila.
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule, Viongozi wa dini na wananchi wakishuhudia sherehe ya vijana wa kimasai (Morani) kuingia stage ya uzeeni.
 Baadhi ya vijana wa Kimasai wakipandisha Mori kwa furaha ya kuingia stage ya uzee

Tigo Tanzania yatoa msaada wa madawati 335 Singida

Mkuu wa Mkoa wa  Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe akinyanyua  mikono juu na mkurugenzi wa  Tigo  kanda  kaskazini, George Lugata na Meneja wa  kandakaskaziniTigo, Aidan Komba.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe akipokea msaada wa madawati 335 yenye thamani ya milioni 56, toka kwa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata kwenye makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya mkuu wa mkoa leo.

Tuesday, September 13, 2016

Wananchi 69 kulipwa fidia ili kupisha uchimbaji wa dhahabu Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi.

Na Mathias Canal, Singida
KAMPUNI ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu (Shanta Gold Mining  Limited) iliyopo katika kijiji cha Sambaru Kata ya Mang’onyi Wilayani Ikungi, Mkoani Singida imetakiwa kuwalipa wananchi 69 waliosalia kulipwa fidia zao kwa ajili ya kupisha mradi wa uchimbaji dhahabu.


Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kufuatia malalamiko ya wananchi wa maeneo mbalimbali waliopo kwenye eneo la mradi huo waliotaka kufahamu hatima ya malipo yao kutokana na awamu ya kwanza kuonyesha kuwa watu 67 ndio watakaolipwa mwishoni mwa wiki hii na wengine waliobaki kulipwa katika awamu zijazo.
Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi wakijadili jambo nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla ya kuingia kwenye kikao.
Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd Philbert Rweyemamu akielezea namna ambavyo watawalipa wananchi 67 ndani ya wiki hii

Chadema yatoa pole kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kanda ya Ziwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHADEMA kinatoa salaam za pole kwa wananchi wote walioathirika na tetemeko la ardhi katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Tabora na kwingine, tukio ambalo limesababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali.
Kupitia taarifa hii, chama kinatoa wito kwa Watanzania wote katika maeneo yaliyopatwa na tetemeko hilo na wengine kutoka nje ya sehemu hizo, kuguswa na tukio hilo na kuwiwa kuwasaidia waathirika wa tukio hilo katika wakati huu mgumu wa kukabiliana na athari zilizotokana na janga hilo.
Viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali, wabunge, madiwani na wanachama wote wa CHADEMA wataungana na kusaidiana kwa kila hali na wote walioguswa na tukio hilo katika wakati huu mgumu wa kupoteza ndugu, jamaa, marafiki, kusitiri miili ya marehemu, kuuguza majeruhi na kupata hifadhi mbalimbali kwa waliopoteza mali na makazi.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na tunawatakia uponaji wa pole na haraka majeruhi wote wa tukio hilo.
Imetolewa na
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Wakulima Kilimanjaro wapewa somo

Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akikagua magunia yaliyokutwa yakiwa yamejazwa Rumbesa.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Wakulima wa mazao mbalimbali likiwemo zao la vitunguu wametakiwa kutofanya biashara kwa kujaza rumbesa ili kuwanufaisha wafanya biashara ambao wanajitokeza vijijini kunua mazao kwani jambo hilo linawanyonya zaidi wakulima na kuwanufaisha wafanya biashara.

Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule mara baada ya kuitisha mkutano wa wananchi katika ziara yake ya kuwahimiza kwa pamoja kujitokeza kushiriki katika zoezi la upimaji ardhi linaloendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Same.

Hata hivyo lengo mahususi la kuamua kuwapo kwa zoezi la upimaji ardhi ni kutaka kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo mbalimbali Wilayani humo sambamba na kupinga kipimo cha Rumbesa kinachowanyonya wakulima wengi nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika Katika Kitongoji cha Jitengeni na Mvungwe uliwahusisha pia wataalamu wa kilimo na ardhi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo sambamba na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akizungumzia unyonyaji wanaokumbana nao wananchi kutoka kwa wafanyabiashara wanaotaka magunia yaliyojazwa Rumbesa.