Pages

Pages

Sunday, September 11, 2016

Chadema yatoa pole kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kanda ya Ziwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHADEMA kinatoa salaam za pole kwa wananchi wote walioathirika na tetemeko la ardhi katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Tabora na kwingine, tukio ambalo limesababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali.
Kupitia taarifa hii, chama kinatoa wito kwa Watanzania wote katika maeneo yaliyopatwa na tetemeko hilo na wengine kutoka nje ya sehemu hizo, kuguswa na tukio hilo na kuwiwa kuwasaidia waathirika wa tukio hilo katika wakati huu mgumu wa kukabiliana na athari zilizotokana na janga hilo.
Viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali, wabunge, madiwani na wanachama wote wa CHADEMA wataungana na kusaidiana kwa kila hali na wote walioguswa na tukio hilo katika wakati huu mgumu wa kupoteza ndugu, jamaa, marafiki, kusitiri miili ya marehemu, kuuguza majeruhi na kupata hifadhi mbalimbali kwa waliopoteza mali na makazi.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na tunawatakia uponaji wa pole na haraka majeruhi wote wa tukio hilo.
Imetolewa na
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

No comments:

Post a Comment