Pages

Pages

Monday, September 19, 2016

HUSSEIN MSOPA: Sharifu majini aliyejikita kuwaombea wenye matatizo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
“IKIWA hujawahi kupata tatizo huwezi jua kama wapo binadamu wenzetu wanaotabika kusaka dawa au vitu vinavyoweza kuwaondoshea maswahibu yao yanayoendelea kuwapa wakati mgumu katika maisha yao bila kuangalia wanaishi kwa mtindo gani,”. Ndivyo alivyoanza kusema Sheikhe Hussein Msopa maarufu kama Sharifu Majini.
Chifu Hussein Msoma maarufu kama Sheikhe Sharifu Majini akiwa katika majukumu yake ya kawaida kama anavyoonekana pichani.
Ndio, sheikhe huyo mwenye maskani yake Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, unaweza kushangazwa na idadi kubwa ya watu wanaotembelea katika ofisi ya sheikhe hiyo, huku kila mmoja wake akiwa na shida yake inayohitaji utatuzi. Kwa wale ambao hawajui lolote kuhusu sheikhe Sharifu majini, pindi wanapopita katika mtaa huo, wanaweza kudhani labda kuna harusi, msiba ayu shughuli yoyote ya kijamii kutokana na ingia tokay a watu katika nyumba ya sheikhe huyo inayotoa huduma mbalimbali za kuombea watu, kuwapatia dawa zikiwamo zinazohusiana na mambo ya majini.
Sheikhe Sharifu Majini pichani.
Watu wanaweza kushangaa au kujiuliza. Je, ni kweli mtu mwenye tatizo anaweza kupata ufumbuzi wa shida yake atakapomuona sheikhe huyo? Katika mazungumzo na mtandao huu yaliyofanyika wiki iliyopita, sheikhe Sharifu anasema kwamba amedhamiria kuwakomboa wale wenye mahitaji na matatizo yanayohusu majini, ukosefu wa uzazi kwa njia za ushirikiana, kusumbuliwa na majini pamoja na kuzitafsiri ndoto mbalimbali zinazohusiana na mifumo ya maisha ya mwanadamu. Sheikhe huyo anasema kwamba uamuzi wake wa kuamua kujihusisha na masuala hayo umetokana na kufahamu adha kubwa inayowakumba binadamu, jambo linalowafanya waishi kwa mashaka katika kipindi chote cha maisha yao.
“Mtu anaweza kwenda hospitali kufanya uchunguzi wa afya ya matatizo ya uzazi na kukuta hana tatizo lolote. Lakini kila anavyojitahidi ili ashike mimba kwa ajili ya kufurahisha nafsi au ndoa yake anajikuta anashindwa kufanikiwa.

Hapo ndipo mtu anapotakiwa kuangalia njia nyingine ikiwamo dua kulingana na imani yake, maana tiba ya kwanza ya mtu ni imani yake, hivyo anapoamua kuja kwa Sharifu majini nafanya wajibu wangu kuangalia mhusika anatatizwa na jambo gani, yakiwamo majini ambayo mara kadhaa hufikia kuwazuia watu kushika mimba,” alisema Msopa.
Anasema mbali ya kushika mimba, baadhi ya wanawake wakati mwingine hujifungua na watoto wao kufariki au hata mimba zao kuharibika mara kwa mara zinazochagizwa na majini wabaya ambao huwasumbua wanawake wengi. Kwa mujibu wa Sheikhe huyo, baadhi ya majini pia huwafunga au kuwadhibiti wanawake wasipate watoto aidha wa kiumbe au wa kike, hivyo jambo kama hilo nahakikisha kwamba nayatoa majini hayo na kuwafungua akina mama hao ambao wengi wao hujikuta wakipoteza matumaini.

Mbali na mambo ya uzazi, shekhe Sharifu majini anasema kwamba wapo watu wanaoishi kwa wasiwasi na hawaoni faida katika maisha yao hususan katika shughuli zao za kijamii kutokana na kusumbuliwa na changamoto mbalimbali. “Haya mambo yapo na yanatuhusu sisi wanadamu, hivyo ni budi jamii kuelewa kwamba katika kitu kianchoitwa jinni si kigeni kwasababu tunaishi nacho ingawaje hatujapewa uwezo wa kukiona kiumbe hicho kwa macho yetu. “Hawa viumbe hutusumbua sana na hugawawanyika katika makundi mawili, yani wale wabaya na wazuri ambao mtu anapotaka kufahamu haya kwa kina au juu ya tatizo lake linalomsumbua namkaribisha ofisini kwangu Mabibo, nikiamini kuwa hatua hii inaweza kuwafanya watu waishi kwa amani na kufanikisha yale waliyokusudia,” alisema.
Sheikhe Majini anasema katika kutoa elimu ya majini na kuombea watu wenye shida, amedhamiria kutoa elimu hiyo haswa kwa wanawake Oktoba 30, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 za jioni.

Sheikhe huyo anasema kwamba katika dua hiyo kwa akina mama na kuwapa ushauri kwa wale watakaokuwa na matatizo hakutakuwa na kiingilio chochote kwenye ukumbi huo mkubwa na marufu hapa jijini Dar es Salaam. Msopa anasema ameamua kuandaa kongamano hilo la dua kwa akina mama baada ya kuona wenye uhitaji huo ni wengi na hawatoshi kufanyia katika eneo la ofisi yake baada ya kujaribu kufanya hivyo hivi karibuni na kujaza watu wengi. Mbali na kushindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati, pia aligundua si sahihi kuwajaza watu wengi katika eneo dogo hali inayoweza kuibua matatizo mengine, ndio maana akaona safari hiii, yani Oktoba 30 apeleke kongamano hilo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Anasema kwamba mambo hayo anayafahamu vizuri baada ya kujikita kwa muda mrefu, huku akiwa na kipaji cha aina yake cha kutambua namna ya kutatua tatizo la binadamu lililosababishwa kwa njia za ushirikina au majini ambayo ndio kesi nyingi zinazowatatiza  binadamu.
“Naomba akina mama wengi waje Diamond Jubilee Oktoba 30 katika kongamano langu ambalo naliandaa kwa mapenzi makubwa kwa watu wote nikiamini kuwa safari hii tutakuwa na wigo mpana wa kutoa huduma zangu kutokana na uzoefu wangu na kipaji nilichokuwa nacho.
“Watu wengi huhangaika sehemu mbalimbali kutafuta suluhu ya matatizo yao, lakini wakija kwangu Mabibo Mwisho ambapo kila mtu ukimuuliza kwa sheikhe Sharifu majini anakuelekeza au kukuleta wanajikuta wanapata tiba halisi,” alisema Msopa au Sharifu Majini kama anavyojulikana na wengi, huku ofisi yake ikipatikana Mabibo mwisho.

Sheikhe Sharifu Majini mwenye asili ya wilayani Handeni, mkoani Tanga, pia ajihusisha na elimu za nyota, tafsiri za ndoto, bahati, kuondoa mikosi pamoja na matatizo mbalimbali yanayowasumbua binadamu, hususan yale yanayoingia kwa njia za kienyeji.

No comments:

Post a Comment