Pages

Pages

Monday, September 19, 2016

Wingi wa mahabusu magerezani wazua gumzo nchini Tanzania

Mkurugenzi  wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf.

Na  Humphrey   Shao, Dar es Salaam
WITO umetolewa kwa wadau wa sheria  kusaidia kupunguza mahabusu Magerezani kutokana na wingi wao ambao aikuwa lazima kuweka humo .

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF),Joaquine De Mello,  wakati wa Hafla ya miaka mitano ya shirika hilo na kukabidhi fedha kwa mashirika mapya ya wanaufaika.

“nimeweza kuzunguka magereza yote nchini na kujionea namna gani wafungwa walivyojazana kwa wingi lakini robo tatu ya wafungwa waliopo humo ni mahabusu ambao awaja hukumiwa” alisema Jaji Joaquine De Mello.
 Wajumbe wa Bodi wa Legal Services Facility katika picha ya pamoja.

 Mwenyekiti wa bodi ya Lsf , Joaquine De Mello akiakabidhi hundi kwa mmoja wa wanufaika.
 Mnufaika wa Ruzuku kutoka tasisi ya  TEWORECakinyoosha hundi yake juu yenye thamani ya shilingi bilioni moja.
 Wanufaika wa Ruzuku wakiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa bodi
Mkurugenzi  wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf
 Mkurugenzi  wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  LSf.


Aliongeza kuwa imefika wakati wa wasaidizi wa kisheria kuanza kuwasaidia watu kwa nagazi ya vituo vya Polisi ambapo huko wanaweza kupata dhamana kabla ya kufika magarezani.

Kwa upande wake, Scholastica Julu, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo alisema kuwa shirika hilo limeweza kutoa fedha zaidi ya Bilioni ishirini kwa mashirika mbalimbali nab ado litaendelea kutoa hili kuweza kusaidia wasaidzi wa kisheria na Mashirika yanayowasimamia .

Alisema kuwa wameweza kupokea changamoto ya usafiri kwenye baadhi ya mikoa na kama shirika wanalifanyia kazi hilo swala hili waweze kutatua tatizo hilo kwa wasaidizi wanaofanya kazi hiyo kwa mazingira hayo magumu. 

No comments:

Post a Comment