Pages

Pages

Saturday, July 30, 2016

Sia Pius ndiye Miss Sinza mpya 2016


 Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd akisema chochote kwenye shindano hilo.
 Mtoa huduma wa kampuni hiyo akitoa huduma kwa wadau wa windhoek.

MGODI UNAOTEMBEA: Tuzipinge siasa za mtaji wa damu zinazohitajiwa na Chadema

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HATA vitabu vya dini vinatueleza binadamu tuzitii mamlaka halali tulizochagua wenyewe ili zituongoze. Ndio, inapotokea mtu anakwenda kinyume na maandiko hayo,  ni dhahiri hatufai, hastahili kuchekewa.
Kambi Mbwana, mwandishi wa makala haya.
Na kutii huko hakupo kwa mwananchi wa kawaida tu. Maadamu ni mamlaka halali, hapana shaka kila Mtanzania wa nchi yetu anapaswa kutii hilo bila kujali dini yake au itikadi yake ya kisiasa. Kwa bahati mbaya, tangu kuanzishwa kwa sheria ya vyama vingi, mwaka 1992, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya viongozi wa upinzani, kufanya mambo ambayo ni kinyume, wakiwa na malengo yao binafsi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli pichani.
Malengo ya kutafuta sifa ya kuungwa mkono na wafuasi wao bila kujali wanafanya kitu kizuri au cha kijinga. Bahati mbaya mfumo huo kadri unavyozidi kupewa nafasi na wapinzani hao, dalili za wazi za kutowesha amani ya nchi yetu inazidi kuonekana. Kwanini isionekane? Utawekeje tone moja la damu kwenye nguo nyeupe na bado ukajindanganya kwamba nguo hiyo itaendelea kuvutia? Pamoja na dalili ya machafuko inayozidi kuonekana, bado hakuna juhudi zinazochukuliwa na wanasiasa kutoka mlengo wa upinzani, wakiamini siasa za kumwaga damu za wananchi wao ndizo zinazoweza kuwaweka juu.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pichani.
Hili haliwezi kukubalika.  Watanzania tusikubali. Tumeshahudia mara kadhaa damu za Watanzania wenzetu zikimwagika bila soni wala haya. Machafuko ya kisiasa yanayoanzishwa na wanasiasa kama Arusha, Morogoro na katika maeneo mengine yameendelea kuonekana, huku chanzo chake kikiwa ni siasa chafu, nyepesi, zisizokuwa na tija kupewa nafasi hususan na chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kwa mfano, Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania (Chadema), kwa kupitia mwenyekiti wao Freeman Mbowe JUZI wametangaza kufanya maandamano na mikutano nchi nzima katika siku ya Novemba Mosi. Na mikutano hiyo itafanyika bila kuangalia imeruhusiwa na jeshi la Polisi au itazuiwa. Inawezekana kuandamana ni halali kwa mujibu wa Katiba, lakini pia busara na usalama lazima ziimarishwe kwa faida ya nchi yetu.

Kufanya maandamano yenye viashiria vya uvunjifu wa amani hakuwezi kuruhusiwa hata kama yamewekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii ni kwa sababu si Watanzania wote wanapendezwa na siasa za upinzani. Wapo ambao hawaungi mkono agizo lolote la upinzani. Na wengine si wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wala CUF. Isipokuwa wote ni Watanzania. Hivyo endapo hayo maandamano yatafanyika bila kufuata sheria, kanuni na taratibu tulizojiwekea, ni wazi kutakuwa ni kupoka haki ya kuishi na kulindwa kwa wengine watakaoathiliwa na maandamano hayo yasiyokuwa na kichwa wala miguu, kama wanavyotaka kufanya viongozi wa juu wa Chadema.
Ndio maana kunakuwa na taratibu. Nani asiyejua kuwa siasa za namna hiyo zimepelekea kifo cha Mtanzania mwenzetu, mwandishi wa habari Daud Mwangosi kule mkoani Iringa?

Ingawa Chadema wanasema mauaji hayo yamesababishwa na Jeshi la Polisi, lakini chanzo kikuu ni ghasia zilizoendeshwa na wao na wakiwa na nia waliyojua wenyewe, ikiwamo hii ya kujulikana kwa lazima bila kujali athari kutoka kwa baadhi ya Watanzania wasiokuwa na hatia. Licha ya kifo hicho au machafuko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, wapinzani wameendelea kutembea katika njia ile ile, wakiamini ndio mtaji wao wa kisiasa ulipo. Hii haikubaliki. Watanzania tusikubali siasa za kumwaga damu zinazofanywa na kuhubiriwa na wanasiasa wa upinzani kwa sababu hazina faida kwetu. Tunachafua tunu ya Taifa letu.

Thursday, July 28, 2016

Chadema wamlilia mpiga picha wa Tanzania Daima, marehemu Joseph Senga

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha mmoja wa waandishi wa habari za picha mwandamizi na mahiri nchini, Joseph Senga kilichotokea usiku wa jana akiwa kwenye matibabu nchini India.
Marehemu Joseph Senga enzi za uhai wake.
Kama taasisi na kisha mtu mmoja mmoja kuanzia kwa wanachama na viongozi wa chama kwa hatua ya sasa tumejikuta tumeishiwa maneno ya kusema kuhusu kifo cha mwandishi huyu mwandamizi, lakini katikati ya mshtuko na majonzi tuliyonayo, tunaweza kusema kuwa kifo cha Senga, hasa siku kiliyotokea, kimedhihirisha jambo moja kubwa kuwa alikuwa SHUJAA WA DEMOKRASIA NA HAKI.
Kifo cha Senga kimetokea siku ambayo kulikuwa na matukio makubwa mawili kuhusu demokrasia na haki nchini.
Kwanza, wakati Senga anafariki usiku wa Jumatano, Julai 27, mchana wa siku hiyo hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, ilikuwa imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 15 jela askari anayefahamika kwa jina la Pacificius Simon kwa hatia ya kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, mkoani Iringa.
Matukio hayo matatu; kuuwawa kwa Mwangosi, hukumu ya aliyemuua na kifo cha Senga, yana uhusiano mkubwa wa karibu huku Senga akiwa katikati yake, kwamba;

Mapambano ya homa Tanzania yazidi kushika kasi

 Baadhi ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kutokomeza homa ya ini wakielekea kwenye  maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo mchana.
 Bango likihimiza kuungana kutokomeza homa ya ini.

Miss Tanga kutimua vumbi jijini Tanga kesho

WAREMBO WANAOWANIA SHINDANO YA MISS TANGA 2016 USIPIME SASA KUFANYIKA IJUMAA MJINI TANGA
Warembo hao wakiwa kwenye picha ya pozi.


Mratibu wa Shindano ya Miss Tanga 2016,Mboni Muya akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusiana na maandalizi ya kuelekea shindano hilo.

Monday, July 18, 2016

Bayport yachangia Sh milioni mbili shule ya sekondari Lindi

Meneja  wa Bayport Financial Services, Tawi la Lindi, Lovin Mapunda, mwenye fulana juu ya jukwa, akitoa msaada wa Sh Milioni mbili katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua, ambapo harambee hiyo iliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Picha na Mpiga Picha wetu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, wa pili kutoka kushoto mstari wa mbele, akifuatilia jambo wakati Meneja wa Bayport Financial Services, taasisi inayojihusisha na mikopo, tawi la Lindi, Lovin Mapunda, hayupo pichani wakati anatoa jumla ya sh Milioni mbili kwa ajili ya mchango wa taasisi yake kwa shule ya Sekondari Lindi, iliyopata balaa la kuungua kwa baadhi ya majengo yake. Picha na Mpiga Picha Wetu, Lindi.


Saturday, July 16, 2016

Mwenyekiti UVCCM Mbeya atoa msaada wa kiti cha mlemavu

Mwenyekiti wa UVCCM  Mkoa Mbeya Amani Kajuna akiwa amebeba kiti maalumu(Wheelchair)  chenye  thamani ya laki tatu na nusu (350,000) kwa ajili kumpatia msaada kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja jijini Mbeya ,ambaye aligundulika akiwa amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka 11 mara baada ya kuzaliwa akiwa na tatizo la ulemavu wa akili na viungo.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya (katikati )akiwa na baadhi ya wadau wakielekea mahala anapoishi kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja jijini Mbeya ambaye aligundulika akiwa amefungiwa ndani na wazazi wake kutokana na ulemavu wake kwa zaidi ya miaka 11 ,ambapo mwenyekiti huyo alitoa msaada wa kiti maalumu (wheelchair)  pamoja  na godoro na mahitaji mengine.

Friday, July 15, 2016

TFF yaupigia chapuo uongozi wa Stand United

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limesema linatambua uhalali wa uongozi wa sasa wa timu ya Stand United ambapo viongozi wake wamepatikana hivi karibuni baada ya kufanyika kwa uchaguzi ambao awali ulizua utata na kuleta sintofahamu kwa wanachama wake na kufikia hatua ya kusimamishwa kwa chaguzi hizo mbili kati ya Stand United wanaojiita wanachama halali na wa kampuni.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa uhalali wa uongozi huo umekubaliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF iliyokutana Julai 13 kwani kuwa uongozi huo unatambulika kihalali baada ya kujiridhisha na jina la usajili la klabu hiyo iliyosajiliwa kwa jina la Stand United Football Club.

"Uchaguzi uliofanyika ni wa haki na TFF tunatambua uhalali wa uongozi uliopo madarakani kwa sasa", amesema Alfred. Pia uongozi huo wa Stand unatambuliwa mara baada ya kufanya marekebisho ya daftari lake wa wanachama kama walivyoagizwa na TFF.

Amesema kwa wale ambao hawakushiriki uchaguzi huo (Stand kampuni) watabaki kuwa wanachama halali wa klabu hiyo hasa wale ambao walienda upande wa kampuni.
Maamuzi hayo yametolewa na Kamati ya uchaguzi wa TFF walipokutana na kuangalia kanuni na katiba na kufikia muafaka wa kuuhalalaisha uchaguzi huo pamoja na Stand United Fc Wakiwa chini ya Makamu mwenyekiti Domina Madeali

Mkuu wa Mkoa Mbeya akabidhi Power Tiller 102 alizopokea kutoka kwa mbunge wa Mbarali

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amepokea power Tiller 102 zenye thamani ya shilingi milioni 510 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Mbarali mhe Haroun Mulla kwa ajili ya shughuli za kilimo na kijamii kwa Vijiji na mitaa 102 ya jimbo la Mbarali.
Mkuu wa Mkoa Mbeya, Amos Makalla akizungumza jambo baada ya kukabidhi Power Tiller zenye thamani ya Sh milioni 510 kutoka kwa mbunge wa Mbarali.
Akikabidhi msaada huo mbunge wa jimbo hilo amesema kuwa wilaya ya mbarali ni wilaya ya kilimo na ufugaji hivyo msaada wake umelenga kusaidia Vijiji na mitaa ili kuchochea Vijiji na mtaa kuwa na chanzo cha mapato na pia kuchochea kilimo. Akipokea kabla ya kuzikabidhi power tiller hizo kwa viongozi wa Vijiji na mtaa amemshukuru na kumpongeza mbunge kwa msaada huo mkubwa na kwa kufanya hivyo ametekeleza vizuri ilani ya Chama tawala ya kuongeza ajira akiamini hizo power Tiller zitaendeshwa na madereva na wasaidizi na pia zitaongeza ukuaji wa uchumi.
Power Tiller pichani.
Aidha amewataka viongozi wa Vijiji kuzitunza na kueleza kwa wananchi mapato yatakayopatikana kutokana na hizo power tiller." Siyo hizi power tiller ziwe Mali zetu ni Mali za kijiji mzitumie vizuri na tuache fitna maana kuna wengine wangetamani badala ya powe tiller mngepewa Fedha hapa nasema Mbunge katupa nyavu tukavue siyo Samaki nawatakia kazi njema na Mipango mizuri"
Amewataka wananchi wote kufanya kazi na muda kwa vijana kucheza pool haupo na hivyo halmashauri zote zitenge asilimia 5 a mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya vijana na akina mama

Chipukizi wa Bongo Fleva kutoka Mwanza apania makubwa

Kutana na kijana Biela Alex kutoka Mtaa wa Mji Mwema Mkudi, Kata ya Isamilo Jijini Mwanza. Anasema yeye ni staa wa mtaa wao na ndoto yake kubwa kwa sasa ni kuwa staa mkubwa wa muziki na maigizo kimataifa zaidi.

Hadi sasa hajui namna ya kutimiza ndoto yake hiyo. Ni vyema pia ukampa ushauri namna ya kufanya ili awe staa katika sanaa kama ilivyo ndoto yake kubwa.

Mabondia Idd Mkwela kuzipachapa kesho Travertine, Magomeni Dar es Salaam


Bondia Idd Mkwela katikati akipima uzito kwa ajili ya mpasmbano wake wa kesho julai 16 na Hussein Gobosi mpambano utakaofantika Travertain Magomeni kushoto ni msimamizi wa upimaji uzito Pembe Ndava nadr donardMadono.
Na MWANDISHI WETU

MABONDIA Idd Mkwela pamoja na Hussein Gobosi wamepima uzito kwa leo kwa ajili ya mpambano wao kesho jumamosi ya julai 16 katika ukumbi wa Travetain Magomeni mpambano uho wa Kg 61 utakuwa wa raundi sita na umekuwa na changamoto kemkem baada ya kila bondia kutambiana kwa kambi zao katika sehemu mbalimbali ikiwemo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mbali na mpambano huo kesho kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi zitakazopigwa kesho ambapo bondia Hussein Itaba atapambana na Ibrahimu Tamba katika uzito wa kilo gram 76mpambano wa raundi nane.

katika upimaji uzito huo uliiofanyika soko la ndizi mabibo katika uwanja wa mpira wa  las vegas kulikua na shangwe na shamlashamla za mashabiki waliojitokeza kwa ajili ya kushudia shughuli nzima ya upimaji uzito

Mkutano wa kuombea Taifa amani kuanza Julai 19

 Mwenyekiti wa Good News for All Ministtry (Great Vition 2000), Askofu Dk.Charles Gadi (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkubwa wa kuombea Taifa kila Jumanne kwa siku 1001 utakaofanyika kuanzia Julai 19, 2016 viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mchungaji James Manyama, Palemo Massawe na Mchungaji Leonard Kajuna.


Na Dotto Mwaibale



Mwenyekiti wa Good News for All Ministtry (Great Vition 2000), Askofu Dk.Charles Gadi anatarajiwa kuongoza mkutano mkubwa wa kuliombea Taifa utakaofanyika kuanzia Julai 19 katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametajwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.


Makonda anatarajiwa kuzindua mkutano huo wa maombi hayo ya siku 1,001 ambayo  yataendelea kufanyika siku ya Jumanne ya kila wiki.


Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo 

Dar es Salaam leo, Askofu Dk. Charles Gadi alisema maandalizi ya  maombi hayo yamekwisha kamilika na kuwa yanakuja kufuatia mengine ya siku elfu moja na moja ya kuliombea taifa yaliyokwisha kufanyika  mwaka 2012 na kukamilika mwaka 2015.

Matokeo ya kidato cha sita, wilaya ya Handeni yaonyesha matumaini

Katika hali ya kufurahisha, wakazi na wananchi wa wilaya ya Handeni wamepata mwangaza wa elimu, baada ya shule yao ya Handeni Secondary School kujitahidi katika shule za sekondari za mkoa wa Tanga zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita.
Ingia hapa kuyaona matokeo yote na shule zote
www.necta.go.tz
YOTE UTAYAPATA KWA KUBONYEZA LINK

Thursday, July 14, 2016

Tigo waingia ubia na serikali kueneza mtandao kwenye shule za serikali


 Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Tigo, Shavkat Berdiev na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora(L) wakisaini makubaliano kwa ajili ya kuunganisha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika hafla iliyofanyika mapema jana katika shule ya sekondari Jangwani Jijini Dar es salaam.

KAMPUNI ya Tigo Tanzania leo imeingia ubia na Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha kufikiwa kwa intaneti katika shule za sekondari nchini  ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni  katika zoezi ambalo litachukua miaka miwili.

Kama sehemu ya makubaliano hayo, wizara itabainisha na kutoa orodha ya  shule zisizo na maabara za kompyuta ili ziunganishwe na hali kadhalika  kuongoza utekelezaji wa mradi  wakati Tigo itadhamini maendeleo ya miundombinu katika shule nchini ikiwa ni pamoja na kuunganisha nyaya ndani ya madarasa  na kufunga visivyotumia nyaya (LAN) na vituo vinavyofikia  mtandao wa intaneti.

Mbunge wa Nzega Vijijini afanya ziara jimboni kwake

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla, pichani kushoto, amewataka wananchi wa Jimbo lake kuwa na Imani naye kwani yeye ni miongoni mwa “Majembe” ya Rais wa awamu ya tano, Mh. Dk. John Pombe Magufuli hivyo kwa Wananchi wa jimbo hilo kuchagua mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani wameramba dume na watapata fursa mbalimbali kama walivyoahidiwa kipindi cha kampeni.

Dk. Kigwangalla amebainisha hayo katika ziara yake ya kushukuru wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kwa kumuwezesha kumchagua kurudi Bungeni kwa kura nyingi na pia kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani

“Ndugu zangu wananchi wa Kata ya Milambo Itobo na wale wa Kata ya Magengati ...Leo narejea hapa kuwashukuru kwa kunichagua kwenu. Nashukuru sana kwani kula zenu zimeweza kuniwezesha mimi kwa mara nyingine tena kurejea Bungeni na kuweza kuwawakilisha nyie katika vikao vya maamuzi hasa vile vya kimaendeleo. Na kutokana na uchapaji wangu wa kazi hata Rais ameniona mimi ni jemba na amenipatia moja ya nafasi za Uwaziri.

ameniteua kwenye Baraza lake la Mawaziri. Napenda kuwapongeza sana na pia naomba niwafikishie salama za Rais kwa kuweza kumpatia kura nyingi sana za NDIO…” Alieleza Dk. Kigwangalla katika mkutano huo wa wazi ambao watu mbalimbali walipata wasaha wa kushuhudia mkutano huo wa kutoa shukrani ambapo pia alitoa misaada mbalimbali ambayo aliahidi yeye mwenyewe kwa moyo wake hasa kwa vijana.

Mbunge Korogwe Vijijini atoa madawati jimboni kwake

 Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Robet Gabriel kushoto akipokea madawati 200 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu jana ambapo madawati hayo yalitolewa kupitia fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati kwa shule za msingi wilayani Korogwe.
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngony'ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu kulia kushoto ni Diwani wa Kata ya Kerenge wilayani Korogwe wakiwa wamebeba moja kati ya madawati 200 ambayo yalikabidhiwa leo na mbunge huyo kupitia Fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya shule za msingi wilayani Korogwe jana.

Saturday, July 09, 2016

Ninachokifahamu kuhusu ubunifu na wabunifu Tanzania

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWEZI January mwaka 2011 nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu, Ahmad Ally ‘Madee’. Madee ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, akipatikana katika kundi la Tip Top ‘Connection’. Madee hakunipigia kunipa habari za kisanaa, ila jinsi anavyomjua kijana mwenye kipaji cha ubunifu wa vitu mbalimbali. Kijana huyo anaitwa Ally Bundu. Wakati huo alikuwa amebuni kifaa kinachojulikana kama simu ya kifuu cha nazi.
 Kijana wa Kitanzania mwenye kipaji cha ubunifu, Ally Bundu, akionyesha moja ya vifaa anavyobuni kila siku kama sehemu ya kuonyesha kipaji chake. Bundu pia alibuni simu ya kifuu cha nazi.

Ni kweli ilikuwa simu ya kifuu cha nazi. Ilikuwa imebuniwa barabara, ikiunganishwa na waya zisizokuwa na idadi ndani yake na ikiingia na kutoka pindi inapopigwa simu hiyo. Baada ya mazungumzo yetu mimi na Madee, nikaafiki wazo la kijana huyo aliyebuni simu hiyo ya kifuu cha nazi kuonana na mimi. Nikiwa na hamu ya kujionea simu hiyo. Siku iliyofuata nikakutana na Bundu katika ofisi yetu ya New Habari 2006 Ltd, kampuni inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Rai, Dimba na The African.
Kambi Mbwana kushoto akiangalia simu ya kifuu cha nazi kutoka kwa mbunifu wake, Ally Bundu kulia.

Baada ya kumuona kijana huyo mwenye sura ya kisanaa ya ubunifu haswa, anayeonekana kujawa na vipawa hivyo vya kubuni, nikaiepeleka akili yangu kwenye kumpyuta  kwa ajili ya kuandika kile nilichoshuhudia kutoka kwa Bundu. Baada ya kumaliza kuandika makala yale, ikapata fursa ya kutumika kwenye gazeti la Mtanzania. Naweza kusema ni miongoni mwa makala au maandiko yangu kadha wa kadha yaliyokuwa na mwendelezo ulionisisimua sana. Siku siku chache baadaye, nakumbuka nilikuwa kwenye mgahawa wa Best Bite, Morocco, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, nikipunguza mawazo na kuzungumza na jamaa zangu kadha wa kadha, ghafla nikaona simu yangu inaita. Namba ilikuwa ngeni

Sunday, July 03, 2016

Mbuzi namba tatu kutoka kwa Muhingo Rweyemamu

MBUZI NAMBA TATU
Na Muhingo Rweyemamu.
Jamani nimemiss sana kuandika. Sasa nimekumbuka wakati fulani niliwahi kuandika kolamu nikaiita acha niandike kama mwendawazimu. Lakini uandishi wangu huwa nalenga kumgusa kila mtu. Majuzi nemewapa mfano wa teabag.Nilisahau kuwaambia kuwa ufanisi wa teabag hautokani na position. Iwe juu ua kikombe, chini ya kikombe pembeni mwa kikombe teabag itafanya kazi. Ufanisi wa teabag hautokani na position. 
Kwa bahati mbaya huwa inachukuliwa kuwa mtu aliyepo juu kabisa kwenye sehemu ya kazi ama familia ndiyo muhimu. Hapana na nafsi yako katika hierarchy ya sehemu yako ya kazi isiathiri impact yako katika kazi yako. Nafasi yako siyo muhimu kwa kuwa nguvu hutoka ndani mwako siyo katika position yako.Leo nawapa mfano wa Mbuzi namba tatu. Mfano huu kwangu huwa ni somo kubwa kwa mahusiano ya kikazi na kimaisha.

Hebu nikueleze kidogo na wewe kwani linaweza pia kuwa darasa kwako. Je, umewahi kuhangaikia jambo ambalo huna na ukapuuza kile ulicho nacho? Katika shule moja ya sekondari Jumapili moja jioni, vijana wawili watukutu waliwazingira mbuzi watatu toka katika banda la jirani. Kisha wakawapaka rangi kwa kuwatia namba 1--2--4. Vijana hao wakawakimbizia mbuzi hao kati eneo la shule.

Kesho yake asubuhi wakati viongozi wa shule walipoingia shuleni walisikia harufu isiyo ya kawaida. Baadaye wakaona kinyesi cha mbuzi kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo lao na hivyo wakahisi kuna mbuzi kwenye jengo hilo. Search ikaanza na mara wakafanikiwa kuwakuta mbuzi watatu. Uongozi wa shule ukasema mbona mbuzi ni watatu badala ya wanne. Wakaulizana yuko wapi mbuzi namba tatu? Walitumia siku nzima wakimsaka mbuzi namba tatu.

Taarifa za mipango ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa zamani wa Kilindi, Beatrice Shelukindo



Familia ya Bwana William H. Shelukindo, Inasikitika kutangaza kifo cha Bibi Beatrice Matumbo Shelukindo kilichotokea siku ya Jumamosi 2/7/2016 huko Arusha.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu 8 Galu Street, Ada Estate, Dar es salaam na huko Arusha.

Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano Tarehe 6/07/2016 alasiri Mjini Arusha.

Bwana ametoa Bwana, ametoa Jina la Bwana lihimidiwe.

Ma DC wapya Mkoa wa Tanga, akiwamo Gondwe wa wilaya ya Handeni waapishwa


Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza kwenye halfa ya kuapishwa wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Othumani Shijja.

Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.