Pages

Pages

Sunday, July 03, 2016

Mbuzi namba tatu kutoka kwa Muhingo Rweyemamu

MBUZI NAMBA TATU
Na Muhingo Rweyemamu.
Jamani nimemiss sana kuandika. Sasa nimekumbuka wakati fulani niliwahi kuandika kolamu nikaiita acha niandike kama mwendawazimu. Lakini uandishi wangu huwa nalenga kumgusa kila mtu. Majuzi nemewapa mfano wa teabag.Nilisahau kuwaambia kuwa ufanisi wa teabag hautokani na position. Iwe juu ua kikombe, chini ya kikombe pembeni mwa kikombe teabag itafanya kazi. Ufanisi wa teabag hautokani na position. 
Kwa bahati mbaya huwa inachukuliwa kuwa mtu aliyepo juu kabisa kwenye sehemu ya kazi ama familia ndiyo muhimu. Hapana na nafsi yako katika hierarchy ya sehemu yako ya kazi isiathiri impact yako katika kazi yako. Nafasi yako siyo muhimu kwa kuwa nguvu hutoka ndani mwako siyo katika position yako.Leo nawapa mfano wa Mbuzi namba tatu. Mfano huu kwangu huwa ni somo kubwa kwa mahusiano ya kikazi na kimaisha.

Hebu nikueleze kidogo na wewe kwani linaweza pia kuwa darasa kwako. Je, umewahi kuhangaikia jambo ambalo huna na ukapuuza kile ulicho nacho? Katika shule moja ya sekondari Jumapili moja jioni, vijana wawili watukutu waliwazingira mbuzi watatu toka katika banda la jirani. Kisha wakawapaka rangi kwa kuwatia namba 1--2--4. Vijana hao wakawakimbizia mbuzi hao kati eneo la shule.

Kesho yake asubuhi wakati viongozi wa shule walipoingia shuleni walisikia harufu isiyo ya kawaida. Baadaye wakaona kinyesi cha mbuzi kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo lao na hivyo wakahisi kuna mbuzi kwenye jengo hilo. Search ikaanza na mara wakafanikiwa kuwakuta mbuzi watatu. Uongozi wa shule ukasema mbona mbuzi ni watatu badala ya wanne. Wakaulizana yuko wapi mbuzi namba tatu? Walitumia siku nzima wakimsaka mbuzi namba tatu.
Watu wote tangu walimu wanafunzi, wapishi, makarani na wote shuleni wakatoka kutafuta mbuzi namba tatu ambayo haikupatikana na kimsingi, hakuwepo. Hivi ndivyo tulivyo. Inawezekana tunayo malengo yetu ya kutimiza lakini tuko obsessively looking for the elusive missing, non-existing goat number three.
Badala ya kutumia vipawa au vitu tulivyo navyo tunabaki tukihangaikia vitu au sifa ambazo hatuna.
Kama wafanyakazi iwe katika shirika, taasisi binafsi, ya umma, au kwingineko ina frustrate mkiwa na kiongozi anayetafuta mbuzi namba tatu muda wote.

Kwa mawazo yangu mafanikio yanakuja pale tu tunapojitahidi kutumia vile tulivyo navyo na tukaacha kuhangaika na vile ambavyo hatuna na wala hatuwezi kuvipata.
Alamsiki.
©Muhingo Rweyemamu




No comments:

Post a Comment