Pages

Pages

Thursday, July 14, 2016

Mbunge wa Nzega Vijijini afanya ziara jimboni kwake

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla, pichani kushoto, amewataka wananchi wa Jimbo lake kuwa na Imani naye kwani yeye ni miongoni mwa “Majembe” ya Rais wa awamu ya tano, Mh. Dk. John Pombe Magufuli hivyo kwa Wananchi wa jimbo hilo kuchagua mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani wameramba dume na watapata fursa mbalimbali kama walivyoahidiwa kipindi cha kampeni.

Dk. Kigwangalla amebainisha hayo katika ziara yake ya kushukuru wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kwa kumuwezesha kumchagua kurudi Bungeni kwa kura nyingi na pia kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani

“Ndugu zangu wananchi wa Kata ya Milambo Itobo na wale wa Kata ya Magengati ...Leo narejea hapa kuwashukuru kwa kunichagua kwenu. Nashukuru sana kwani kula zenu zimeweza kuniwezesha mimi kwa mara nyingine tena kurejea Bungeni na kuweza kuwawakilisha nyie katika vikao vya maamuzi hasa vile vya kimaendeleo. Na kutokana na uchapaji wangu wa kazi hata Rais ameniona mimi ni jemba na amenipatia moja ya nafasi za Uwaziri.

ameniteua kwenye Baraza lake la Mawaziri. Napenda kuwapongeza sana na pia naomba niwafikishie salama za Rais kwa kuweza kumpatia kura nyingi sana za NDIO…” Alieleza Dk. Kigwangalla katika mkutano huo wa wazi ambao watu mbalimbali walipata wasaha wa kushuhudia mkutano huo wa kutoa shukrani ambapo pia alitoa misaada mbalimbali ambayo aliahidi yeye mwenyewe kwa moyo wake hasa kwa vijana.

Aidha, Dk. Kigwangalla aliwaomba wananchi wa Vijiji vya Kaloleni kuwa na subira kwani atahakikisha Umeme wa gridi ya Taifa inapita katika vijiji hivyo na kupata umeme wa uhakika ambapo kwa sasa tayari ameliombea hilo na litatekelezwa muda wowote kuanzia sasa.

Mbali na hilo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kuwa na subra kwa kipindi hiki kwani barabara inayoanzia kwenye barabara kuu ya lami ya Tabora kuingia Inagana mpaka Milambo Itobo ambayo hipo chini ya Tanroad, inatarajiwa kukarabatiwa na itakuwa msaada kwa wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao wanajishughulisha na shughuli za Kilimo ikiwemo ulimaji wa vitunguu kwa wingi, Tumbaku, Pamba na Mpunga.

Mbali na kutoa ahadi hizo kwa wananchi hao, Pia Dk. Kigwangalla aliahidi kutoa shilingi Laki tatu kwa vijiji vya Kaloleni, Usagali na Inagana kwa ajili ya kuchangia maswali ya dini

Dk. Kigwangalla pia mbali na kutoa shukrani kwa wapiga kula wake hao, pia alipata wasaha wa kusikiliza kero za wananchi huku akipokea kero zao hizo ambapo ameeleza kuwa atazifanyia kazi

Wananchi waliuliza maswali mbalimbali ikiwemo kupata matibabu licha ya kujiunga na mfumo, barabara mbovu, Umeme.

Na Andrew Chale, Nzega

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akkwaslli kwenye viwanjavya mikutano katika kijiji cha Magukula cha Kata ya Milambo Itobo. (Picha zote na Andrew Chale - MO Blog)
Diwani wa Kata ya Milambo Itobo Mh.Rafael Rwenge akitoa hotuba fupi katika mkutano huo
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akieleza katika mkutano huo.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasikiliza baadhi ya wazee wa Jimbo hilo baada ya kumaliza mkutano wa kuwashukuru kwa kumchagua
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akimjulia hali mmoja wa waananchi wa jimbo hilo waliofika kwenye mkutano
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Wazee Usagala (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog-Nzega).

No comments:

Post a Comment