Jamal Malinzi, akisaini baada ya kurudisha fomu leo TFF
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI
wa Chama cha Soka mkoani Kagera (KRFA), Jamal Malinzi amekuwa wa kwanza
kurudisha fomu za kuwania nafasi ya Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),
katika Uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.
Jamal Malinzi akishuka kwenye gari lake leo TFF
Mbali na
Malinzi, Makamu wa Rais, Athumani Nyamlani, naye alijitokeza katika uchukuaji
wa fomu wa nafasi hiyo nyeti, ikiwa ni baada ya rais anayemaliza muda wake,
Leodgar Tenga, kutangaza kujiweka kando kwenye uchaguzi huo.
Athumani Nyamlani kulia, akipokea fomu za kugombea nafasi ya Urais wa TFF
Akizungumza
muda mfupi baada ya kurudisha fomu hiyo, Malinzi alisema kwamba anaamini muda
wake wa kuwa rais wa TFF umefika kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika
michezo.
Alisema
mwaka 2008 alipogombea nafasi hiyo, kura zake hazikutosha, hivyo uvumilivu
wake, uwezo wake katika masuala ya michezo, ukiwamo mpira wa miguu, mambo
yatakuwa mazuri na kufanikiwa kuipata nafasi hiyo.
“Sitaki
kusema maneno mengi kwasababu muda wa kampeni bado, hivyo lakufanya navuta
subira huku nikiwataka wenye uwezo wa kuongoza wachukuwe fomu ili atafutwe mtu
mmoja katika nafasi ya Urais wa TFF.
“TFF
kumekuwa na utulivu wa aina yake hasa kutokana na sera nzuri za Tengaa, ambaye
ametangaza kutogombea tena nafasi hii, hivyo wa kuvaa kiatu chake atapatikana
baada ya uchaguzi huo kukamilika,” alisema.
Naye
Nyamlani alisema kuwa TFF sio taasisi ya kujaribu kujifunza kuongoza, hivyo
kwake yeye uwezo anao wa kuongoza kutokana na uzoefu aliokuwa nao baada ya kuwa
Makamu kwa miaka minne.
“Nimeiva
vizuri ili niwe rais wa TFF, hivyo baada ya kampeni kuanza nitatangaza sera na
mikakati yangu, maana naamini kwa sasa muda wake bado zaidi ya kusubiri watu
wengine wenye nia yao kugombea nafasi za uongozi wa TFF,” alisema.
Kinyang’anyiro
hicho kimeibua joto kali kutokana na wanamichezo wengi kuhamasika katika
uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za TFF.
No comments:
Post a Comment