Yusuf Manji kushoto, akipewa fomu na mmiliki wa timu ya African Lyon, Rahim Zamunda.
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI
wa klabu ya Yanga ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Yusuf
Manji, ameingia kwenye mbio za uongozi za Shirikisho la Soka nchini (TFF),
baada ya kuchukuliwa fomu na mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Zamunda leo katika ofisi za TFF.
Manji akizungumza na waandishi wa habari.
Zamunda
alimchukulia fomu za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu kwa nia
ya klabu za Ligi Kuu zilizompendekeza mwenyekiti huyo wa Yanga.
Uchaguzi
huo utafanyika Februari 24 huku ukizidi kuleta msisimko wa aina yake kutokana
na majina ya wanamichezo wanaojitokeza katika patashika hiyo.
Mbali na
Manji, wengineo waliochukua fomu leo ni pamoja na Jamal Malinzi, Athumani
Nyamlani na Omari Mussa Nkwarulo, ambao
wamechukua fomu za kugombea urais wa TFF.
Uchaguzi
wa TFF unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka hapa nchini, ikiwa ni hatua ya
kupatikana viongozi wapya, hasa baada ya kipindi cha rais anayemaliza muda
wake, Leodgar Tenga kumalizika na kutangaza kutogombea tena nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment