https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, February 18, 2015

MGODI UNAOTEMBEA:CCM iwapime wabunge wake mizigo 2015

Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete pichani.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
JOTO la kisiasa limezidi kupamba moto. Hii ni kutokana na harakati za kuimarisha kambi za wagombea wa nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini kote.
Wameanza mchaka mchaka wa udiwani, ubunge bila kusahau urais. Kwa nafasi ya urais, tumeshuhudia watu wanaojiandaa kuvutana na kustawisha makundi yao ili iwe chachu yao ya kurithi kiatu cha Rais wa Awamu ya nne, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete.

Ingawa nafasi za ubunge na udiwani zinawaniwa pia na watu kutoka kwenye vyama vya upinzani, lakini ni wazi kuwa joto na mtifuano mkubwa upo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kila chama kina taratibu zake. Hata hivyo, kutokana na maridhiano yao waliyopa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vyama vinne vya upinzani vikiongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama Cha Wananchi CUF, NCCR Mageuzi na NLD vimetangaza kusimamisha mgombea mmoja kila jimbo la uchaguzi au kata.

Huo ndio msimamo wa wapinzani. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaamini kuwa vyama vya upinzani mwaka huu watafanya vizuri katika Uchaguzi Mkuu, endapo CCM haitajisahihisha na wafalme wake majimboni.

Ni kutokana na hilo, nadiriki kusema kwamba, uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu. Katu CCM isitarajie mteremko. Ili iweze kujua namna gani inafanya vizuri katika uchaguzi huo, ni lazima iwapime wabunge na wagombea wake hususan kwa nafasi za ubunge.

Tuesday, February 17, 2015

Radio za Jamii zapewa somo

DSC_0219
Mshehereshaji kwenye madhimisho ya siku ya redio duniani, Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.(Picha zote na Zainul Mzige.

Na Mwandishi wetu, Arusha
Vyombo vya habari hususan redio za jamii zimetakiwa kutanguliza uzalendo na kutetea maslahi ya taifa ili kuliepusha taifa katika migogoro na mitafaruku inayoweza kusababisha machafuko nchini hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa wakati wa kuadhimisha Siku ya Redio duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na watangazaji wa redio za jamii na wadau mbalimbali wa habari nchini katika ufunguzi wa maadhimisho hayo Munasa alisema redio ina nguvu kubwa kuchambua na kutengeneza mustakabali wa taifa na hasa vijana iwapo itatumika vizuri badala ya kuwa chanzo cha matatizo na uchochezi mambo ambayo yanaweza kulisambaratisha taifa.

Amewataka waandishi na watangazaji wa redio jamii kuzingatia maadili ya kazi zao kwa lengo la kuleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania na kujenga taifa endelevu .
DSC_0255
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, Nyerembe Munasa akizungumza katika ufunguzi wa kuadhimisha siku ya redio duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

“Mnatakiwa kutafiti, kutathmini na kupeleka taarifa zenye tija na kuhamasisha vijana kujituma kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa wimbi la umaskini kwa wananchi na hasa vijana, mkitekeleza wajibu wenu kwa kujua nini mnachofanya mtachochea mabadiliko kwa haraka katika jamii”.

Akizungumzia fursa zilizopo, Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru ametoa wito pia kwa vyombo vya habari hususani radio za jamii kuwawezesha vijana wa Kitanzania kutambua na kutumia fursa zilizopo za uchumi wa gesi na mafuta ili kujiondoa katika umaskini unaolalamikiwa kusababishwa na ukosefu wa kazi.

Mahundi, Bahanuzi wachezaji bora VPL

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KIUNGO wa timu ya Coastal Union, John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Disemba 2014 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Baraka Kizuguto, alisema kwamba Mahundi alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Coastal Union mwezi Disemba mwaka jana na kuchaguliwa na jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi.

Aidha mshambuliaji wa timu ya Polisi Morogoro, Said Bahanuzi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi mzunguko wa 15 kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Bahanuzi anayechezea timu ya Polisi Morogoro kwa mkopo akitokea timu ya Young Africans amekua na mchango mkubwa kwa timu yake tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini.

Kwa kuibuka wachezaji bora, Mahundi na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

Monday, February 16, 2015

Msanii TID amlilia baba yake Dully Sykes aliyefariki

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed maarufu kama (TID), pichani chini mwenye miwani, ameonyesha kuguswa na kifo cha baba wa msanii Dully Sykes, Abby Sykes, anatayetarajiwa kuzikwa leo mchana katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Msanii TID pichani...
Baba yake Dully Sykes, marehemu mzee Abby Sykes, pichani enzi za uhai wake.
Akizungumzia msiba huo, TID alisema kwamba marehemu alikuwa karibu naye, sambamba na kuwahi kuimba naye mara kadhaa.

“Mzee Abby Sykes alikuwa ni kama mzee wangu kwasababu nilikuwa karibu naye, hivyo nimepokea msiba huu kwa masikitiko makubwa,” alisema TID.

DRFA yaivuliaa kofia Azam na Yanga michuano ya Kimataifa

CHAMA cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya vilabu barani afrika klabu ya Azam FC na Yanga SC,kwa kuanza na ushindi katika mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.

Yanga walikuwa wa kwanza kuwapa raha watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa taifa jijini,baada ya kuifunga mabao 2-0 timu ya maafande wa Polisi toka Botswana BDF 11,mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe la shirikisho.

Kwa upande wa Azam FC,wao waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika mchezo wa kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam Cpmplex Chamazi.

Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo, amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo nzuri waliyoanza nayo,na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo kuelekea mashindano hayo ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na makocha,ni dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.

Kasongo,pia amesema DRFA imeridhishwa na muitikio wa mashabiki wa Dar es salaam na maeneo mengine nje ya jiji kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo mbili,na kuwapongeza pia viongozi wa vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya licha ya dosari ndogo ndogo zilizojitokeza.

Tanzania yaichapa Kenya 5-3 michuano ya beach soccer

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni (Beach Soccer) jana imeibuka na ushindi wa mabao 5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa fukwe za Hotel ya Big Tree Pirates jijini Mombasa.

Katika mchezo huo mabao ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne  na Mwalimu Akida bao moja .

Kipindi cha kwanza kilimazika kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili kilimalizika Tanzania 4 Kenya 3 na kipindi cha tatu na cha mwishokwa mchezo kimalizika kwa Tanzania kupata mabao 5 Kenya 3.

Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar es salaam, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa Kenya, itacheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.

Mchezo wa kwanza utafanyika kati ya tarehe 7,8 Machi 2015 jiji Dar es salaam na marudiano yatafanyika nchini Misri kati ya tarehe 13,14 Machi 2015.
Timu inarejea leo jijini Dar es salaam majira ya saa 11 jioni ikitokea jijini Mombasa nchini Kenya.

SIWEZI KUVUMILIA: NSSF safi, sasa tutasonga mbele

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKA la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), limejitokeza katika sekta nyeti ya michezo kwa kushirikiana na Klabu ya Real Madrid kuanzisha kituo cha michezo nchini Tanzania. 
Meneja Kiongozi na Uhusiano wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume, pichani.
Katika kituo hicho cha michezo, NSSF shirika kubwa Tanzania lenye uwezo mkubwa na kushirikiana na jamii yake, litashirikiana pia na klabu ya Real Madrid ya Uhispania, huku mradi huo ukigharimu Sh bilioni 16.

Ujenzi huo utajumuisha viwanja vitano vya mpira wa miguu, mabweni ya wachezaji na wageni, maduka na huduma nyingine muhimu, ambapo pia watajenga uwanja wa gofu wenye mashimo 18 utakaoambatana na ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo la ekari 400 lililopo katika mji uliopangwa kuwa wa kisasa wa Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Hongera sana NSSF, ila wengine wapo wapi? Shirika hilo limefanya kitu ambacho kitakuwa na mguso na uwezo wa kuibua vipaji vya vijana wetu. Hii ni kwa sababu kwa miaka mingi Tanzania imeshindwa kufanya vizuri katika michezo, hususan mpira wa miguu.

Kushindwa huko kunatokana na kukosa mipango yenye tija. Tunakuwa na wachezaji ambao umri wao ni mkubwa. Nguvu zao nyingi zinaishia kwenye ligi za mchangani na wanapoingia Ligi Kuu wamechuja.

Wednesday, February 11, 2015

Uzinduzi wa Tanzania Financial Services For Underserved jijini Dar es Salaam

Dr. Evans Rweikiza akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Giraffe Ocean View, katika uzinduzi wa Tanzania Financial services  for Undeserved Settlements(TAFSUS) jijini Dar es Salaam.

MGODI UNAOTEMBEA:Vita ya urais, inawatoa akili wapambe

NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM
JAMHURI ya Muungano wa Tanzania, inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu kwa nafasi mbalimbali. Ni katika Uchaguzi huo, Watanzania watapata fursa ya kuwachagua madiwani, wabunge na rais.
Bernard Membe, mmoja  wa makada wa CCM na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye anatajwa kuwa na ndoto ya kuwania urais baadaye mwaka huu.
Edward Lowassa, naye ni kada wa CCM ambaye pia Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, anayetajwa pia kuwa na ndoto ya kuwania urais baadaye mwaka huu.

Uchaguzi huo utafanyika Bara na Visiwani nao watachagua wawakilishi wao wanaoamini kuwa watakuwa na msaada nao kuhakikisha kwamba Zanzibar inapiga hatua.
Joto kali na msisimko wa aina yake umeshika kasi kutokana na uchaguzi huo. Mengi yanasemwa. Mengi yanasikika pia. Ieleweke kuwa, kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

Yoyote anaweza kuwa mbunge au diwani kama sheria inavyosema katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, wale wenye sifa zilizotajwa kwenye urais, nao wana haki hiyo.

Hata hivyo lazima tufahamu urais si jambo dogo. Ni Mungu pekee anayebariki jambo hilo, ukizingatia kwamba ni nafasi moja inayoshikwa na mtu mmoja, iwe Tanzania au kwingineko kwenye utaratibu huo.

Tatizo si kugombea nafasi hiyo nyeti ya urais. Tatizo hawa wapambe wa urais wanaojitoa akili kwa kushabikia mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu, hususan kwa wakati huu.

Vita ya urais ipo katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya wanachama wake wengi kutajwa au kuonyesha nia ya urais mwaka huu. Hadi sasa, wanachama zaidi ya nane wameonyesha nia ya kuwania urais badaye mwaka huu na kuibua joto na msigano wa hali ya juu.

Baadhi ya wanachama hao ni pamoja na Bernard Membe, Samuel Sitta, Dkt Asha-Rose Migiro, Steven Wassira, January Makamba, Khamis Kigwangwallah, Edward Lowassa, Lazaro Nyalandu na wengineo.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...