https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, March 23, 2014

Azam yashinda, Simba yalala mbele ya Coastal Union Wagosi wa kaya

TIMU ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam, imejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania ubingwa wa Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Oljoro bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodaco uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Bao la Azam lilifungwa katika dakika ya 71 na mshambuliaji wa timu hiyo, John Bocco kali.
Kwa matokeo hayo wanaendelea kukalia usukani wa ligi hiyo wakiwa na pointi 47,  kwa tofauti ya pointi nne na Yanga, wenye pointi 43.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu ya Simba ilijikuta ikifungwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Bao la Coastal Union katika mchezo huo lilifungwa katika dakika ya 45 na Hamadi Juma baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Simba na kumchambua kipa Ivo Mapunda.

TAZARA wafungua tawi la Simba SC, wapewa onyo la kutokuwa wachochezi ili waisaidie klabu yao



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAFANYAKAZI 176 wa Shirika la Reli la Zambia na Tanzania (TAZARA), wamejiunganisha kwa pamoja na kufungua tawi la klabu ya Simba, wakiwa na shauku ya kuisaidia timu yao kufanya vyema na wao kupata raha ya ushindi.
Baadhi ya wanachama wa Tawi la TAZARA wakisikiliza maneno ya meza ya mbele.
Uzinduzi wa tawi hilo ulikwenda sambamba na kugawa kadi 50 za uanachama kwa wafanyakazi hao, huku mgeni rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Swed Mkwabi.


Swed Mkwabi, mwenye fulana nyekundu, akipiga picha ya pamoja na wanachama wa tawi la Simba la TAZARA leo jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu wa Tawi hilo jipya la Simba lililokuwa na maskani yake TAZARA, Abdallah Sambizi, alisema kuwa kuanzishwa kwa tawi hilo ni hatua muhimu za kuisaidia klabu yao.



Mgeni Rasmi, aliyesimama meza ya mbele, Swed Mkwabi, akisikiliza baadhi ya hoja kutoka kwa wanachama wa Simba, Tawi la TAZARA, jijini Dar es Salaam leo.
Alisema kuwa wanaamini kwa pamoja watafanya mambo mema ya kusaidiana na viongozi wao Makao Makuu kwa ajili ya kuipaisha timu yao, ambayo kwa msimu huu imeonekana kusua sua.

Sisi mashabiki na wanachama tunachohitaji ni ushindi tu, hivyo naamini kwa pamoja tutashirikiana na wenzetu wa Makao Makuu ili kuipaisha klabu yetu ndani na nje ya nchi, huku tukiepuka kuwa wasumbufu au kutoa matamko yasiyokuwa na mashiko kwa timu yetu tunayoipenda,” alisema Sambizi.

Naye Mgeni rasmi wa uzinduzi wa tawi hilo, Mkwabi, aliwataka wanachama na viongozi wa tawi hilo kuwa na dhamira ya kweli ya kuisaidia Simba na sio wao kusaidiwa na klabu yao kwa kushiriki au kujitolea kwa mambo ya kimaendeleo.

UVCCM wapongeza hotuba ya Rais Kikwete juu ya Katiba Mpya



MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Utangulizi:
Ndugu waandishi wa habari, mabibi na mabwana. Leo tena nimewaita kwa ajili ya kuzungumza mambo machache muhimu yahusuyo taifa letu Tanzania. Yangu leo ni machache na muhimu ni kutoa salamu za pongezi za Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hotuba murua aliyoitoa Juzi 21/03/2014 wakati akizindua bunge maalum la katiba. Kama taasisi muhimu katika taifa hili, tumechukua hatua hii madhubuti kulieleza taifa umuhimu wa ile hotuba, mantiki iliyopo katika ile hotuba, na kwa kuwa sisi tunawakilisha sauti za vijana zaidi ya milioni 25 wa taifa hili, na kwa kuwa athari nyingi za katiba hii tunayotengeneza zitawaathiri sana vijana kuanzia sasa na mustakabali wao. Hatuwezi kukaa kimya ama tukaungana na wale wenye kulaumu pasipo kujua mantiki, maana mwisho wa siku vijana hawatawalaumu wale wanaowapotosha kwa sauti zao kali, bali watawalaumu wale walio na ufahamu na wakakaa kimya kama Martin Luther "King" alivyowahi kusema;
"In The End we will remember, Not the Voices of Our Enemies, but The Silence of Our Friends".
Sisi ni rafiki wa Taifa hili na watu wake, hatuwezi kukaa kimya huku tukiwaona wale wasitutakia mema wakiendelea kueneza sumu mbaya ya kutugawa katika makundi makundi.
Ndugu waandishi, Tanzania ina watu milioni 49 (kwa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 na makadirio yake ya mwaka 2013). Kwa kuwa bunge hili maalum limechukua mfumo wa uwakilishi wa watu wote kwa makundi yao (yaani fair representation), kwa bunge lenye wajumbe 619, maana yake ni kuwa, kwa wastani kila Mbunge anawakilisha Watanzania 79,000. Sasa hapa ndipo kwenye kazi na mantiki tunayoijenga; kwamba
i. Ikiwa Mbunge mmoja atasimama bungeni na kutekeleza wajibu wake ipasavyo, basi sauti za watanzania 79,000 zitakuwa zimewakilishwa vema, na akifanya tofauti yake halikadhalika haohao watanzania kwa hasara yao.
ii. Fikiria kwa mfano Mbunge akasimama dakika tano akatumia muda huo kutukana badala ya kujenga hoja kwa manufaa ya taifa, maana yake ni kuwa hawa watanzania elfu 79 wamepoteza dakika 79000x5=4,345,000 ambayo ni sawa masaa 72,461 ama siku 3,071 ambayo kimahesabu ni karibu miaka kumi. Hebu fikiria huyu ni Mbunge wako yaani kwa kitendo cha dakika tano amekufanya umepoteza miaka 10 kwa kutukana mfululizo.

Soka la vijana lapigiwa chapuo wilayani Handeni, mkoani Tanga



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
KATIBU wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 ya Lyons Sport ya kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Sadiki Mbwana, amesema kwa kuwekeza kwenye soka la vijana, mpira wa Tanzania unaweza kupiga hatua kubwa.
Sadiki Mbwana, pichani.
Akizungumza mjini humo, Mbwana alisema kuwa jambo hilo limewafanya waendelee kuweka mikakati ya kuiendeleza timu hiyo ya vijana, inayotokea katika mgongo wa timu kubwa ya Men Stone.

Alisema kuwa kwa kulifanyia kazi jambo hilo, wanaamini mchakato huo utakuwa na mashiko, hivyo wanaendelea na mikakati yao kuliboresha kwa kuiunda timu hiyo vizuri.

“Naamini huu ni mpango mzuri ambao kwetu sisi utakuwa na mafanikio makubwa, jambo linalotupa moyo zaidi.

Timu za vijana zianzishwe katika kila mahala, tukiwamo sisi tunaopatikana katika wilaya, ukizingatia kuwa ndio sera yenye tija kwa soka la Tanzania,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, wanaamini kwa kuiendeleza zaidi timu yao ya vijana, wanaweza kukuza soka la wilaya yao ya Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Serikali yatenga Sh Bilioni nne kulikabili tatizo la maji wilayani Handeni, mkoani Tanga

Kilichojiri mtandaoni wiki hii.
Hii ndio kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akielezea mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika ziara yake wilayani Handeni, Korogwe na maeneo mengine ya Mkoa wa Tanga. Pia DC Muhingo alielezea tatizo la maji na kusema kuwa litapatiwa ufumbuzi kwa kutengwa kiasi cha Sh Bilioni 4 kwa ajili ya maji wilayani Handeni.....

Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu pichani.
"Nashukuru Kambi, huwa nasoma sana mtandao huu sana. Tupo kwenye maandalizi, tumeaandaa mabasi manane ya kubeba watu; matatu toka Komsala kwenda Handeni na matatu toka Mkata kwenda Handeni. Tumepika chakula cha kutosha watu 2,000 ili kila anayefika asishinde njaa. Tutakuwa na vikundi kadhaa vya burudani bila kusahau ngoma ya selo pamoja a wapambanaji wa JKT. 

Tutakuwa na bendi tatu. Taarabu moja ya JKT itapiga leo usiku.Tumechelewa hamasa kwa sababu tumepata uthibitisho wa ziara siku ya Alhamisi lakini tunajitahidi watu wengi wafike. Hoja kama wengi mnavyosema ni maji na tungefurahi wananchi wakimuomba rais wao kuhusu maji. Hata hivyo, mwaka huu serikali imetenga shilingi bilioni nne kwa ajil ya wilaya ya Handeni tu. 

Ni hela nyingi kutolewa kuliko wilaya yoyote nchini. hizi zinatosha kuchimba mabwawa 17, kati ya hayo mabwawa mawili yanaendelea kuchimbwa likiwamo la Mkata na Manga. Maji kutoka Wami yapo kijiji cha Kwasunga, yanakuja Manga. Serikali imekubali kutupatia fedha kwa lengo la kufufua mradi wa HTM. Mradi huo unahitaji jumla ya shilingi bilioni 136. 

Hata hivyo, serikali itatusaidia fedha hizo kwa awamu. Tumeagiza mashine kwa ajili ya Sindeni na fedha tumekwishalipa shilingi milioni 50 na inatarajiwa kufika mwishoni mwa mwisho wa mwezi ujuao. Hii itauhakikishia mji wa Handeni maji ya uhakika. Natamani mmoja wenu journalism aje ili tuandike program na matatizo ya maji Handeni"

Tuesday, March 18, 2014

SIWEZI KUVUMILIA: Yanga hii imevurugwa?

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam 
YANGA acheni masihara na serikali. Sio kila mnalolijadili nyie na kulihitaji, basi ni zuri na linastahili kuchukuliwa kama msimamo wa Watanzania wote. Wakati mwingine mambo yanayofikiwa kwenye klabu hii kongwe yanachekesha na kushangaza pia!
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, pichani.
Katika kuliangalia hili, naukumbuka wimbo wa dada mmoja wa kizazi kipya aliposema ‘Nimevurugwa’. Mwanzo sikumuelewa, lakini sasa namuelewa, hasa baada ya kutafakari kwa kina mashairi yake na jinsi jamii yetu tunavyoishi kwa kuvurugwa vurugwa.
Hili ‘Siwezi Kuvumilia’. Ni baada ya kikundi cha watu wachache, Yanga kuipa serikali siku tano iwape majibu, kabla ya kuamua kufanya maandamano makubwa jana Jumatatu kushinikiza wapewe eneo la heka 11 zilizopo Jangwani, jijini Dar es Salaam. Kauli hiyo tata ilitolewa na anayejiita ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali. 
Mbaya zaidi, kauli yake iliungwa mkono baada ya kuipata barua ya kubariki msimamo huo kutoka kwa Katibu Mkuu wao Benno Njovu. La kushangaza zaidi, Akilimali na wenzake walijigamba kuwa uamuzi huo umetoka juu, yani chini ya Mwenyekiti wao Yusuph Manji.
Ni kweli, maana kitendo cha Katibu Mkuu kulisapoti inamaanisha kuwa wameafiki jambo hilo. Hapa inashangaza kidogo! Yanga hii ina sauti gani kiasi cha kufikia kuipa amri nzito serikali? Naheshimu ukongwe wao katika nyanja ya soka, ila si kitendo cha kutaka kuvuruga amani ya Taifa letu. 

Sunday, March 16, 2014

TFF yalalalamikiwa mkoani Tanga

Na Mwandishi Wetu, Tanga
BAADHI ya Wakazi waliokuwa wamejenga katika eneo ambalo shirikisho la soka nchini kwa kushirikiana na shirikisho la soka duniani (FIFA) wanatarajiwa kujenga uwanja wa Kimataifa wamelalamika kuwa serikali bado haijawalipa fidia ili kuweza kupisha ujenzi wa uwanja huo.
 
Hatua ya wakazi hao inatokana na kuona Rais wa Shirisho la soka nchini (TFF)Jamali Malinzi akitembelea uwanja huo na kuanza mikakati ya ujenzi wa uwanja huo ambao unatarajiwa kugharimu mabilioni ya fedha za kitanzania.
 
Wakizungumza katika nyumba zao wanazoishi ndani ya eneo la shirikisho hilo lililopo Mnyanjani jijini Tanga baadhi ya waathirika hao ambao wengi wao ni akina mama Christina Lucas alisema wamekuwa wakihangaikia fidia kila kukicha kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ili waweze kupisha ujenzi wa uwanja wa kimataifa bila mafanikio yoyote.
 
Alieleza zaidi kuwa baadhi yao wameshapewa maeneo ya kwenda kujenga nyumba baada ya serikali skuridhia ombi lao lakini fidia ndio imeshindwa kutoka hadi wakati huu kitendo ambacho kinawaweka kwenye wakati mgumu.

Yanga wanusurika katika ajali mkoani Morogoro

BASI la Yanga lenye namba za usajili T916 CCS, limenusurika kupinduka maeneo ya Mikese, mkoani Morogoro, ikitokea huko kucheza mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mechi hiyo iliyopigwa jana, timu hizo zilichoshana nguvu, licha ya kutambiana kwa siku kadhaa katika kuelekea kwenye mechi hiyo ya aina yake na iliyohudhuriwa na watu wengi.

Katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi, wachezaji na wote waliokuwapo kwenye basi hilo walitokea madirishani, akiwamo kocha wao Mholanzi Hans van der Pluijm.

Ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo linajaribu kukwepa basi la abiria, hivyo kuingia mtaroni na kuzua hofu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile, alishindwa kuthibitisha kwa ajali hiyo baada ya simu yake kushindwa kupokewa licha ya kupigiwa simu mara kadhaa na mwandishi wa habari hizi.

Hata hivyo, hakuna aliyeumia na timu imeendelea na safari ya kurejea Dar es Salaam, licha ya kuzua hofu kadhaa kutoka kwa wadau wa soka.

Saturday, March 15, 2014

Ridhiwani aanza mbwembwe za kampeni Uchaguzi Mdogo Chalinzee

Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Steven Kazidi (kushoto) akimuinua mkono juu kwa ishara ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo jana Machi 14,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubi wananchi wa Kijiji cha Matipwili,Saadani Wilayani Bagamoyo,wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni zake ulioanza rasmi jana Machi 14,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubi wananchi wa Kijiji cha Saadani,Wilayani Bagamoyo.wakati wa kampeni zake zilizoanza rasmi jana Machi 14,2014.

Friday, March 14, 2014

Ridhwan kuwasaidia wasanii Chalinze



Na Mwandishi Wetu, Chalinze
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete amesema atahakikisha anaitumia sanaa kama bidhaa muhimu katika kuongeza ajira kwa wananchi wa jimbo hilo.

Ridhwani alitoa msimamo wake huo juzi ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuinua maisha ya wakazi wa Chalinze kwa njia ya sanaa na michezo.

Akizungumzia fursa za ajira katika sanaa na michezo, alisema anaamini Chalinze kuna vipaji vingi ambavyo vinatakiwa kuendelezwa.

Alisema akiwa kama mgombea wa Ubunge analitambua hilo na anaona kuwa linahitaji kuandaliwa mkakati endelevu.

"Mimi mwenyewe kwanza ni mdau wa mambo mengi, yaani mimi kwanza ni mtu wa mpira na pia masuala ya utamaduni, ninaamini kabisa katika mila zetu za kiafrika, sasa kwa nini nisipiganie kukuza sekta hizi," alihoji.

Rais Kikwete awaapisha viongozi wa Bunge la Katiba

Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw, Yahya Khamis Hamad akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Yahya Khamis Hamad akisaini Kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete Leo Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kiapo baada ya kumuapisha Katibu bunge Bw. Yahya Khamis Hamad (mbele aliyesimama).

Jeshi la Polisi laweka mikakati kabambe Uchaguzi wa Kalenga

Kamanda wa polisi mkoani Iringa Kamishina Msaidizi Ramadhan Mungi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari asubuhi hii mjini Iringa wakati alipozungumza nao katika ofisi zake zilizopo jengo la mkuu wa mkoa huo. IMG_4471 
……………………………………………………………………………
Ndugu waandishi wa habari, kwa niaba ya askari Polisi wa Mkoa wa Iringa, nitumie fursa hii kuwakaribisha hapa ofisini kwetu.
                Ndugu zangu tumeitana hapa asubuhi hii ili niweze kuwapa taarifa ya usalama katika Mkoa wetu wa Iringa hususani katika Jimbo la Kalenga katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kalenga na usalama wa siku ya uchaguzi wenyewe.Ili iwe rahisi kueleweka taarifa hii nitaitoa kwa kifupi sana kwa kuigawa katika maeneo matatu.
Eneo la kwanza ni juu ya wapi tunataka tupafikie  ( Where we want to go ), eneo la pili ni lile la wapi tulipo ( Where are we? ) na eneo la tatu ni jinsi gani tutafika huko ( How do we get there ). Tuanze    na  wapi   tunataka   tupafikie. Sisi  Polisi  Mkoa  wa  Iringa  tunataka  wananchi  wa  Kalenga  wapinge  kura  kwa  amani  na  utulivu  mkubwa   siku  ya   jumapili  tarehe  16/3/2014. Hii   ndio  dila  yetu  na  tutahakikisha  tunafika  hapo.

Thursday, March 13, 2014

Wakulima wa chai Bumbuli waiangukia serikali


Na Mwandishi Wetu, Bumbuli

SERIKALI imetakiwa kufikia uamuzi wa haraka juu ya kumtafuta mwekezaji mwingine wa kiwanda cha Chai, cha Mponde,  kilichopo Halmashauri ya Bumbuli,  Wilayani  Lushoto, ili kuinusuru chai ya wakulima inayoendelea kuharibikia shambani kwa miezi minane sasa, tangu kifungwe.

Kiwanda hicho cha Mponde ambacho ni Umoja wa Wakulima wa Chai (UTEGA), wanamiliki asilimia hamsini, huku mwekezaji asilimia iliyobaki, kilifungwa baada ya wakulima kugoma kupeleka  majani  mabichi  kwa madai kuwa mwekezaji huyo anawalangua.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani Bumbuli, wakulima hao walisema tangu kiwanda hicho kimefungwa jana chai yao inaharibikia mashambani na kuwapa ugumu wa maisha.

Hamis Jabiri mkulima wa Chai katika halimashauri hiyo, aliiomba serikali kuwafungulia kiwanda chao ili kunusuru maisha yao, maana wamekuwa wakiishi maisha magumu na kuongeza makali ya maisha na kuyumbisha uchumi wao.

Naye Robart Tembe, alisema baada ya kufikia uamuzi wa kukifunga kiwanda hicho, serikali iliunda tume ili kupendekeza kuundwa kwa uongozi wa muda katika kiwanda hicho.

"Waandishi wa habari maamuzi ya kufungwa kwa kiwanda tuliyafanya sisi wakulima kwasababu hatumtaki mwekezaji, hivyo serikali ilete mwingine na kuanza kuendesha uzalishaji na sisi tuuze chai yetu kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Tembe.

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Beatreace Msomisi, alisema tangu kiwanda hicho kilivyoacha kufanya kazi halmashauri hiyo imeathirika kiuchumi, kwasababu ya kiwanda hicho kuwa tegemezi la wakulima.

Coastal Union waiwinda Azam fc



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TIMU ya Coastal Union, yenye maskani yake jijini Tanga, inajiandaa vizuri kukabiliana na joto katika mchezo wao dhidi ya Azam utakaopigwa Jumamosi ya Machi 15, katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mechi hiyo inachezwa huku kukiwa na marekebisho kadhaa, hasa kati ya Simba na Costal, waliopangwa kucheza Jumatano, kabla ya mechi hiyo kusogezwa mbele hadi Machi 23.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Costal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa wanajiandaa vyema ili kusaka ushindi dhidi ya Azam.

Alisema ingawa wamepata matokeo mabaya ya sare dhidi ya Ashanti United, ila bado hawajakata tamaa katika patashika ya Ligi ya Tanzania Bara.

“Coastal bado hatujakatishwa tamaa katika harakati za kuiweka juu zaidi timu yetu, hivyo kwa sasa tunajiandaa kuwakabiri Azam.

“Naamini utakuwa ni mchezo mgumu kupita kiasi, ukizingatia kuwa Azam wao wanasaka ubingwa, hivyo watataka mbeleko kutoka kwetu, jambo ambalo haliwezekani kirahisi,” alisema.

Simba inayonolewa na kocha wake Zdravko Logarusic, imeshindwa kuonyesha cheche za kuunyaka ubingwa wa Tanzania Bara, baada ya kuendelea kupata matokeo mabaya katika mechi zake.

Yanga waitisha maandamano makubwa kulazimisha kupewa eneo la Jangwani ili wajenge uwanja wao wa kisasa, Jerry Silaa, Meya wa Ilala lawamani



BARAZA la Wazee wa Klabu ya Yanga, limetangaza kufanya maandamano makubwa siku ya Jumatatu ya Machi 17, endapo Manispaa ya Ilala itashindwa kuwajibu ombi lao la kuongezewa heka 11 katika eneo la Jangwani ili wajenge Uwanja wa kisasa wa michezo, kwa madai kuwa wanazunguushwa na wanawekewa kauzibe na serikali hiyo waliyofanikisha maendeleo yao tangu kuasisiwa kwa klabu hiyo.




Maandamano hayo yatashirikisha wanachama na wapenzi wa Yanga, kwa madai kuwa serikali imeshindwa kuwathamini na kutotambua mchango wao, licha ya klabu hiyo kujihusisha na mambo mengi ya kimaendeleo, hivyo wanaona ni fursa yao sasa kuanza kuitisha maandamano hayo makubwa.

Endapo maandamano hayo yatafanikiwa, huenda ikawa timu ya kwanza kuandamana kwa kuishinikiza serikali, huku wakitambua kuwa nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria na sio kulazimishana.
 

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...