https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, February 25, 2014

SIWEZI KUVUMILIA:Malinzi, zingatia vipaumbele


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

NI mapema mno kumlaumu Jamal Malinzi, kama Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), ukizingatia kuwa ndio kwanza ana kipindi cha miezi mitatu tangu alipoitwaa nafasi hiyo nyeti kwa soka la Tanzania.


Badala ya kumlaumu, ni vyema pia tukawa wawazi kumshauri ili katika mipango yake, basi mingi iwe na tija kwa soka la Tanzania, linalokwenda mbele na kurudi nyuma.


Tangu Malinzi aitwae nafasi hiyo, ameonyesha shauku kubwa ya kuongoza tofauti na aliyemtangulia, yani Leodgar Tenga, ambaye amemaliza muda wake.


Ingawa muhimu ni maendeleo, ila Napata hofu kuona Malinzi ametamani michakato mingi kwa haraka.


Binafsi naona suluhu ya maendeleo yetu ni kuhakikisha kuwa eneo la utawala, yani mfumo wa uongozi kwenye Shirikisho lake unakuwa na mashiko.


Utawala ambao utasimamia sheria 17 za soka na sio wale wanaochukua uamuzi kwa kuangalia faida zao binafsi, hasa hizi za Usimba na Uyanga.


Suluhu nyingine ni kuona kunakuwa na mashindano mengi ya vijana, maana ndio maeneo mazuri ya kukuza kiwango cha mpira wa miguu.


Ingawa kila mtu ana haki ya kusema kile anachojisikia, ila kwangu mimi nitaangalia zaidi vitendo vyake na mipango kabambe ya kuendeleza mpira wa miguu.

Monday, February 24, 2014

Yanga, Al Ahly haitafungwa kwa magazeti

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KIDOGO nimepata furaha kuona kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwassa, alielekea nchini Misri kwa ajili ya kusoma nyendo za wapinzani wao, timu ya Al Ahly, kabla ya kuvaana Jumamosi wiki hii.


Timu hiyo tishio katika ukanda wa Afrika Magharibi, inajiandaa kucheza na Yanga, timu kongwe hapa nchini, kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kipa wa Yanga, Juma Kaseja, ni moja ya walinda mlango makini wanaopaswa kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya mechi ya Al Ahly hap0 Machi Mosi mwaka huu.

Yanga inaingia uwanjani huku Watanzania tukiwa na kumbukumbu mbaya ya timu zetu kushindwa kutamba mbele ya timu za Misri.


Ni timu ya Simba tu, walau inaweza kuwa na historia japo kwa uchache juu ya timu za kutoka Misri, walipokutana na mara chache iliweza kujivunia.


Mwaka 2003, Simba iliweza kuwaondosha Mabingwa wa nchi hiyo, timu ya Zamalek, baada ya kushinda bao 1-0 jijini Dar es Salaam, kabla ya kushinda 3-2 kwa njia ya penati katika Uwanja wa ugenini.


Ukiacha historia hiyo kwa Simba dhidi ya Zamalek, bado timu hiyo ina chakujivunia kwa timu ya Mafulira Wandarers ya Zambia, mwaka 1979 baada ya kuchapwa bao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa, kabla ya kushinda bao 5-0 ugenini.

Sunday, February 23, 2014

Simba majanga, yapigwa 3-2 na Ruvu JKT, Azam nao watoka sare dhidi ya Prisons



MAJANGA. Timu ya Simba ilijikuta ikiangukia pua baada ya kukubali kipigo cha bao 3-2 kutoka kwa maafande wa JKT Ruvu, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, hivyo kuonekana kujitoa rasmi kwenye mbio za ubingwa.
 Wachezaji wa JKT Ruvu wakishangilia goli dhidi ya Simba.
Mabao ya JKT yalifungwa na Hussein Bunu dakika ya 13, Dakika ya 45 kupitia kwa Emmanuel Swita na dakika 52 kupitia kwa Swita tena, wakati mabao ya Simba yalifungwa na Amis Tambwe dakika ya 64 na 84, hivyo kulala bao 3-2.

Mechi nyingine iliyopigwa leo ni Azam FC na Tanzania Prisons ambazo zote zimefungana bao 2-2 katika mechi iliyokuwa na msisimko wa aina yake.

Moto wazuka baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso mkoani Morogoro

LEO asubuhi mkoani Morogoro kumetokea ajali iliyohusisha Lori lililokuwa limebeba mafuta ya diesel, ambalo limegongana na lori lililokuwa likifuata saruji tanga na kusababisha shoti iliyozusha moto mkubwa eneo la Lubungo, Mikese. Ajali hiyo ilisababisha magari mengine yashindwe kupita kwa zaidi ya saa tatu.
Moto ukitekeza magari yaliyogongana mkoani Morogoro leo.
Shuhuda wa ajali hiyo alisema kuna uwezekano mkubwa ajali hiyo ikagharimu uhai wa mtu, hasa kwa kuangalia mazingira yake, hasa kwa madereva. Taarifa kamili juu ya ajali hiyo tutaendelea kukupatia kadri zitakavyofika kwenye chumba chetu cha habari.

Mtu mmoja akiangalia moto ulivyokuwa unatekeza magari yaliyogongana uso kwa uso leo mkoani Morogoro....

Jay Msangi aipigia magoti serikali



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
PROMOTA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Jay Msangi, ameiomba serikali kuliangalia upya suala la kusimamishwa kwake kuandaa mapambano ya ngumi kwakuwa hali hiyo inaweza kuzorotesha mchezo huo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msangi alisema kuwa kusimamishwa kwake kuandaa mapambano ya masumbwi kumelenga kumkomoa na si kuleta chachu ya kuutangaza zaidi mchezo huo.

Alisema miongoni mwa tuhuma kuwa anadaiwa na bondia wa Marekani, Phil Williams zilishamalizika kwa kulitatua suala hilo kwa makubaliano ya bondia huyo na waandaaji wa pambano hilo lililomkutanisha na Mtanzania Francis Cheka.

“Kuna mambo mengi yanaweza kutokea nyuma ya pazia, hivyo ninachoitaka serikali ni kuangalia zaidi athari zinazoweza kutokea juu ya kusimamishwa kwangu.

“Mimi na Williams tulishamalizanaa na nipo tayari kupekeleka vielelezo juu ya bondia huyo, hivyo siamini kama harakati hizi zinaweza kuleta tija katika masumbwi,” alisema.

Mgogoro wa promota huyo umekuja wakati wadau hao wa masumbwi walishafanya mkutano wa kujadili jinsi ya kuutangaza na kuukuza mchezo wa masumbwi unaosua sua, hivyo kuonyesha kuwa bado juhudi madhubuti zinahitajika ili kukomboa ngumi.

Waziri Mukangara mgeni rasmi Kilimanjaro Marathon


Mhe. Dk. Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dk. Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi.
Aggrey Marealle, Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waratibu wa mbio hizo alisema jana kwamba Dr. Mukangara amekubali kuwa mgeni rasmi na atahuduria sherehe ya utoaji zawadi ambapo atatoa zawadi kwa washindi kumi wa mbio defu za kilomita 42 maarufu kama Full Marathon kwa wanaume na wanawake. 
Aggrey Marealle
“Uwepo wa waziri ni ishara ya uungaji mkono tukio hili na ameeleza kufurahishwa kwake na maandalizi ya hali ya juu ya Kilimanjaro Marathon. Dk. Mukangara ameeleza mara kadhaa kwamba serikali inaunga mkono Kilimanjaro Marathon kwa kutambua mchango wake michezo, utalii na uchumi,” alisema Marealle.
Marealle aliongeza kwamba baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe. Leonidas Gama, wawakilishi wa wadhamini na watu wengine mashuhuri kwenye mlo maalum  wa mchana uliodhaminiwa na Kibo Palace Hotel. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro binafsi na kupitia ofisi yake amekuwa muungaji mkono wa Kilimanjaro Marathon na amekuwa akifurahia kukaribisha maelfu ya watu wanaokuja Moshi kutoka mataifa mbalimbali.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema “mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za  nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.

Saturday, February 22, 2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani afunga mkutano wa jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro

Kutoka kushoto, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani, Mubarrak Abdulwakil, Kaimu IGP, Abdulrahman Kaniki, Mkuu wa Polisi Zanzibar, Ali Mussa Ali na DCI, Isaya Mngulu
Maafisa wakuu wa polisi wakishiriki kuimba wimbo wa maadili ya Jeshi hilo.

Kiongozi wa bendi ya MPA, Dogo Vena na kundi lake wakitumbuiza katika hafla ya kufunga mkutano wa makamishna na Maafisa wakuu wa Jeshi hilo.

Yanga yafanya mauaji ya mwaka Taifa baada ya kuwatandika bila huruma Ruvu Shooting bao 7-0



MASHABIKI wa timu ya Yanga, leo wameondoka uwanjani na furaha tele baada ya kuishuhudia timu yao ikivuna ushindi mnono wa bao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mabao hayo yalifungwa na Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Emmanuel Okwi na Didier Kavumbagu ambao kwa hakika walifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa wanaichabanga timu hiyo inayomilikiwa na jeshi kwa bao nyingi zaidi ili wafunge midomo yao.

 

Friday, February 21, 2014

Matokeo kidato cha nne yatangazwa, angalia majina ya shule zilizofaulisha vizuri

Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2013 yametangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi leo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Wizara hiyo, shule 10 bora zilizopata matokeo mazuri ni pamoja na 1. St.Francis Girls (Mbeya), 2. Marian Boys (Pwani), 3. Feza Girls (Dar-es-salaam), 4. Precious Blood (Arusha), 5. Canossa (Dar-es-salaam), 6. Marian Girls (Pwani), 7. Anwarite Girls (Kilimanjaro), 8. Abbey (Mtwara), 9. Rosmini (Tanga) na 10. DonBosco Seminary (Iringa).

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MAPYA HAYA HAPA 2013

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

ACSEE 2013 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES







































Uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TASWA kufanyika Machi 2 mwaka huu


Uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam. 


Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Tanga Raha blog kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo,Boniface Wambura zimeelewa kuwa fomu kwa ajili ya waombaji uongozi zinaanza kutolewa Jumatatu (Februari 24 mwaka huu) kwenye ofisi za Idara ya Habari. 

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.


Ada kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.

Kamati ya Uchaguzi inawahimiza wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kugombea, lakini vilevile waisome vizuri Katiba ya chama chao.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...