https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, December 22, 2013

Wilaya ya Handeni yafurahia utamaduni kuenziwa

Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

AFISA Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Godfray Munga, amesema kwamba kufanyika kwa Tamasha la Utamaduni wilayani humo kumechangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza wilaya yao.

Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Tanga, Frank Maduga, akiperuzi katika gazeti huku akiwa ni miongoni mwa wadau waliohudhuria tamasha la Handeni Kwetu lililofanyika Jumamosi ya wiki iliyopita, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Tamasha hilo lilifanyika Jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu, huku likishirikisha wadau mbalimbali sanjari na viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya Mkuu wa Wilaya Muhingo Rweyemamu.

Akizungumza mapema wiki hii, Munga alisema akiwa kama Afisa Utamaduni, amefurahi kuona eneo lake la kazi linakusanya watu wengi kwa ajili ya kuenzi jitihada za maendeleo kwa kupitia sekta ya utamaduni.

“Hili ni jambo ambalo limenifanya nione faraja sana katika kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania unaenziwa hususan kwa wakazi na wananchi wa Handeni.

“Naamini mambo yatazidi kuwa mazuri katika siku zijazo kulifanya tamasha lifike mbali zaidi kwa kushirikisha wasanii na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,” alisema.

Katika Tamasha hilo, mgeni rasmi alikuwa DC Rweyemamu, ambapo alishuhudia umati wa watu ukihudhuria kwa mara ya kwanza na kulifanya kwa mafanikio makubwa.

Asha Baraka ambana Mbizo sakata la Gurumo


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Kamati ya Gurumo (55) Asha Baraka, amembana mratibu wa tamasha hilo Juma Mbizo kwa kumtaka ampelekee ripoti ya matukio yalivyoandaliwa na kufanyika katika onyesho la kumuaga Muhdin Gurumo, lililofanyika Jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu.

Mwenyekiti wa iliyokuwa Kamati ya Gurumo, Asha Baraka kulia, katika matukio ya kufanikisha tamasha la mzee Gurumo.

Asha aliyasema hayo huku kukiwa na habari mbaya kutoka kwa baadhi ya wadau waliolalamikia maandalizi pamoja na mgawo wa fedha kwa wale walioalikwa, ukiachwa walioamua kujitolea.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Asha alisema kwamba wakati tamasha hilo la kumuaga Gurumo linafanyika alikuwa nje ya nchi, hivyo amemtaka Mbizo kama mratibu apelike ripoti.

Baada ya kupigwa bao 3-1 na Simba jana, Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ambeba mgongoni Juma Kaseja



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuph Manji, amesema kwamba klabu yao haijamsajili kipa Juma Kaseja ili aweze kuifunga timu ya Simba, badala yake wametaka kuboresha kikosi chao katika michuano ya Kimataifa, ikiwamo ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, pichani.
Jana katika mechi yao ya bonanza inayojulikana kama Nani Mtani Jembe, ilimalizika kwa Simba kuwafunga Yanga bao 3-1 na kuwasononesha mashabiki wa jangwani walioamini kuwa kikosi chao ni imara dhidi ya Simba.

Akizungumza leo asubuhi Makao Makuu ya Yanga, Manji alisema kuwa wanaoamini Yanga inastahili kuifunga Simba kwasababu yupo Kaseja langoni hao wanajidanganya, maana si lengo lao.

Alisema Yanga pamoja na benchi lote la ufundi linaamini kwa kuboresha kikosi chao kwa kuwa na wachezaji wazuri ni safari nzuri ya kutafuta heshima Barani Afrika.

Saturday, December 21, 2013

Zitto Kabwe afunguka mjini Kigoma, mapokezi yake hayajawahi kutokea

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, leo ameonyesha kukubalika kwake baada ya maelfu kumiminika kwa wingi kumshuhudia akitokea mjini Dodoma katika Bunge, ikiwa ni ishara ya wananchi hao kumuunga mkono.

Katika mapokezi hayo, Kabwe anayeparuana vikali na viongozi wenzake ndani ya Chadema, alitumia muda mwingi kuonyesha namna hali ya mnyukano inavyoendelea ndani ya Chadema, chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

Na haya ndiyo aliyosema Kabwe, katika mapokezi yake leo mjini Kigoma..........
 
Hotuba ya Zitto Kabwe - Kigoma: 21 Desemba 2013
HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DESEMBA 2013

Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji.

Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.

Hivi ndivyo wananchi walivyompokea Kabwe Zitto leo.

Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995. Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994.

Wakati Watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa Ujiji, watu wa Kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.

Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma.

Japhet Kaseba aapa kumtungua Alibaba kesho



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA Japhet Kaseba, amesema uwezo wake ni mkali hivyo anaamini Alibaba Ramadhan hawezi kumletea madhara katika pambano lao litakalofanyika leo katika ukumbi w Friends Corner, Manzese, jijini Dar es Salaam.
Japhet Kaseba, pichani.
Akizungumzia maandalizi yake, Kaseba alisema kuwa ana kiwango cha juu pamoja na pumzi za kucheza na Alibaba katika pambano lisilokuwa la ubingwa.
Alisema kuwa anaamini mashabiki wake watapata burudani kali kutoka kwake, hivyo aliwataka waingie kwa wingi kushuhudia makali yake katika ulimwengu wa masumbwi.
“Uwezo wangu ni mkali na siwezi kufanya makosa dhidi ya Alibaba, hivyo nimeapa lazima nishinde kwa kuhakikisha kuwa natoa kichapo kwa mpinzani wangu,” alisema.
Kaseba aliwahi kutamba pia katika ulimwengu wa mateke, huku akiwa ni Bingwa wa Ngumi za Mateke na kufanikiwa kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Pitia hutuba iliyong'oa vigogo wa Rais Kikwete Bungeni jana

1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likijadili hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013, iliyowasilishwa na Mhe. Said Nkumba, Mbunge wa Sikonge kuhusu Mgogoro kati ya Wafugaji na Wakulima, Hifadhi na Uwekezaji, Mheshimiwa Spika alitoa Uamuzi ‘Speakers Ruling’ kuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ishughulikie kazi ya kutathmini na kuangalia jinsi Mpango wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na kutekelezwa na Serikali kupitia ‘Operesheni Tokomeza’.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr Khamis Kagasheki, kabla ya kujiuzulu jana.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Taarifa Rasmi za Bunge za tarehe 1 Novemba 2013, wakati Bunge likihitimisha Hoja ya Kuairisha Shughuli za Bunge, Mhe. Spika alitoa uamuzi ufuatao:-
…Kamati ile ya kawaida ya Maliasili itaendelea na kazi yake ya kufanya tathmini ya kuangalia jinsi mpango ule wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na ndani yake itashughulikia kama kulikuwa na uzembe ama kuna watu wanahusika katika kuondoa maisha ya watu kwa sababu za uzembe …

1.1 Kuundwa kwa Kamati Ndogo ya Uchunguzi
Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi ulioutoa tarehe 01 Novemba, 2013 Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, ilikutana Dodoma tarehe 9 Novemba, 2013 kwa lengo la kujadili utaratibu wa kutekeleza jukumu hilo. Katika kikao hicho Kamati iliazimia kuunda Kamati Ndogo kwa mujibu wa Kanuni ya 117(18), ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Tole la 2013 ili iweze kushughulikia suala hilo kikamilifu.

1.2 Hadidu za Rejea, Wajumbe wa Kamati na muda wa kazi
Mheshimiwa Spika, Kamati Ndogo ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyoundwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwa agizo lako la tarehe 01 Novemba, 2013, ilipewa Hadidu za Rejea Nne (4) zifuatazo:-
1) Kutathmini na kuangalia jinsi Mipango ya Kupambana na Majangili ilivyopangwa;
2) Kuangalia kasoro zilizojitokeza katika kutekeleza mpango huo;
3) Kutathmini iwapo kulikuwa na uzembe katika kutekeleza Operesheni Tokomeza ambao ulisababisha watu wasio na hatia kupoteza maisha na mali zao; na
4) Kuchunguza migogoro ya Ardhi inayohusu Wakulima, Wafugaji na Wawekezaji kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi.

Friday, December 20, 2013

SIWEZI KUVUMILIA: Karibu Logarusic, ila jiandaye kwa mengi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KWA hali ilivyokuwa ndani ya klabu za Tanzania, hususan zile kongwe za Simba na Yanga, utaamini kuwa hata aje kocha wa aina gani, bado mabadiliko yanaweza kuwa ya kubangaiza.
Siku kocha mpya wa Simba, Zdravko Logarusic alipowasili Tanzania.
Hii ni kwasababu mara kadhaa utaona jinsi baadhi ya viongozi wa soka na wadau wao wanavyojifanya hawanazo katika kubuni mikakati yenye kuleta maendeleo ya klabu zao.
 
Wakati nasema haya, nakumbuka jinsi kocha mpya wa Simba, Zdravko Logarusic alivyopokewa kwa mbwembwe na mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi.
 
Hata hivyo, utagundua kuwa aina ya mapokezi ya Logarusic si kitendo kigeni, maana tayari walishawahi kupokewa kwa vishindo kiasi cha wao wenyewe kujishangaa.
 
Hakika siwezi kuvumilia. Siwezi Kuvumilia, maana najua kocha huyo hatakuwa   na maisha mazuri ndani ya Simba. Anapita njia tu. Labda amekuja kutalii au kujionea viongozi wa soka wasiokuwa na dhamira ya kweli ya kuokoa soka letu.
 
Ama amekuja kuangalia mashabiki na wanachama wenye mihemko ya aina yake. Ukifiria sana unaweza kulia. Ni pale makocha hao wa kigeni, mfano wa Logarusic wasivyokuwa na heshima mbele ya jamii yao pale matokeo yanapokuwa magumu.

Monday, December 16, 2013

Ilikuwa ni raha na utamu Tamasha la Handeni Kwetu lililofanyika wilayani Handeni mkoani Tanga, juzi Desemba 14

MSIMU wa kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni, lililokuwa  likisubiriwa kwa hamu hatimaye lilifanyika Juzi, wilayani Handeni  Tanga  ambapo kama ilivyokuwa ikitarajiwa, Shirika la Taifa la mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilijitokeza na kubeba tamasha hilo.
Meneja wa NSSF mkoani Tanga, Frank Maduga
Shirika hilo, likiwa limejitokeza dakika za mwisho katoa udhamini wake katika tamasha hilo kubwa na la kwanza kuwahi kufanyika katika Ardhi  ya wilaya ya Handeni linalojumuisha vijiji zaidi ya kumi, lilichangia fedha taslimu shilingi milioni mbili, fedha ambazo kwa kiasi kikubwa ukiacha mchango wa wahisani wengine zilichangia  kufanikiwa kwa Tamasha hilo.
Akizungumza wakati wa kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la utamaduni Handeni 2013, Kambi Mbwana alisema kukiwa na dalili zote za tamasha kushindwa kufanyika kama ilivyotarajiwa, NSSF kupitia Ofisi ya kanda ya Tanga ilijitolea kunusuru Jahazi.
Mratibu wa Tamasha la Utamaduni Handeni-Kambi Mbwana akitambulisha Wadhamini wa Tamasha hilo lililofanyika Juzi katika uwanja wa Azimio, wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Ilikuwa balaa.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu akimkaribisha mmoja wa wahudhuriaji wa Tamasha hilo, Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Mohamed Mhita.
Mkurugenzi wa Grace Products akitoa neno la Shukrani kwa Waandaji wa Tamasha


“Awali ya yote napenda kutanguliza shukurani zangu zote kwa wahisani wa Tamasha hili, Vodacom, Grace products pamoja a wadhamini wengine kwa kufanikisha Tamasha hili la kwanza kuwahi kuwakutanisha watu wa kadhia mbalimbali,
JKT walikuwepo wakafanya yao jukwaani ilikuwa ni noma saaaana
Utamu wa Ngoma uingie uicheze
DC Muhingo Rweyemamu

Shukurani kubwa ziende kwa NSSF, kwa kweli hawa watu wanajali utu, tunaomba watusamehe kwa mapungufu yetu lakini kwa kweli wanastahili kuitwa mfuko wa Hifadhi,” alisema Kambi
Awali akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao pamoja na kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha kama hayo jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo wanayoyataka.

Muhingo alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima watu wa eneo Fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao kwa sauti kama waratibu wa Tamasha hilo walivyofanya.
Vyakula vya Asili hapa palikuwa ni mahala pakee

“Tunajivunia kuwa na vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa tamasha hili ni matokeo ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu, Hongereni sana,” alisema Rweyemamu.
Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank Maduga alisema shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na waaandaaji wa Tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa Mtanzania unatumika kulitangaza Taifa.
Mamia ya Waandamanaji wakielekea katika Viwanja vya Azimio.
Timu ya Tamasha la Utamaduni Handeni....chezea, aliyenyoosha vidole viwili ishara ya Chadema ni msanii wa kizazi kipya, aliyeimba mtindo wa Kitanga Tanga, Ahmad Salum, Mady Salu, akiwa katika picha ya pamoja kwenye Tamasha hilo.
Msanii kutoka katika kundi la Okalandima, akionesha uwezo wa kutafuna Moto, hii ni moja ya Vyakula vyetu huku Handeni hasa Kwamsisi, karibu Handeni Kwetu.....

Katika tamasha hilo,kulikuwa na vionjo mbalimbali vya Utamaduni wa Wanahandeni, ikiwa ni Pamoja na Ngoma za asili kutoka katika Vijiji vya wilaya ya Handeni kama vile, Kweingoma, Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni Mjini.

Burudani kali na ya kuvutia iliyoonesha asili kamili ya Mtanzania ilitoka kwa Kundi la Sanaa la Jeshi la JKT Mgambo, Azimio Jazz band bila kusahau msanii wa kundi la Fataki, Machenja ambaye alipiga onesho la kukata kiu akiwa na wana okalandima.

Tamasha la Utamaduni Handeni ambalo linafanyika kwa mara ya Kwanza lilidhaminiwa na NSSF, Clouds fm, Vodacom, Plan B, gazeti la Mwananchi, MICHUZI BlogKajunason Blog, Chichi Local Wear, Katomu Solar specialist, Dullah Tiles and Construction, Anesa Company Limited, Country Business directory, Jiachie Blog na TAIFA LETU.com.

Tamasha la Handeni lafana chini ya udhamini wa NSSF kwa kushuhudia burudani kali za Wazigua na chakula cha asili

Mamia ya wakazi wa wilaya ya Handeni, kutoka katika vijiji vya Kwamsisi,Kwachaga, Kwamkonga, Komsala na vijiji vinginevyo wakiandamana kuelekea katika Uwanja wa Azamio ilikofanyika Tamasha la Utamaduni Handeni Mwaka 2013 ilikuwa ni noumaa Sana

Baadhi ya wananchi kutoka katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Handeni wakiandamana kuelekea katika viwanja vya Azimio, kuhudhuria msimu wa Kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni Kwetu 2013, Tumethubutu na kufanikiwa tunasonga mbele...

Akizungumza wakati wa kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la utamaduni Handeni 2013, Kambi Mbwana alisema udhamini wa NSSF ulikuwa mkombozi mkubwa kwao.

“Awali ya yote napenda kutanguliza shukrani zangu zote kwa wahisani
wa tamasha hili, hasa ndugu zetu wa NSSF maana hakika wameonyesha moyo wa uungwana katika kuhakikisha kuwa Handeni Kwetu inazaliwa kwa mafanikio, ukizingatia kuwa tamasha hili limekusanya watu wa aina mbalimbali.

Awali akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao pamoja na kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha kama hayo jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo wanayoyataka.

Muhingo alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima watu wa eneo fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao kwa sauti kama waratibu wa tamasha hilo walivyofanya.


“Tunajivunia kuwa na vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa tamasha hili ni matokeo ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu, hongereni sana,” alisema Rweyemamu.


Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank Maduga alisema shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na waaandaaji wa tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa Mtanzania unatumika kulitangaza Taifa, pamoja na kutumia fursa hiyo kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa kutoa elimu ya huduma zao wilayani Handeni na Tanzania kwa ujumla.


"NSSF ni shirika la Watanzania na tumedhamiria kuwapatia huduma bora Watanzania wote, hivyo kila mtu ana haki ya kujiunga na mfuko huu kwa ajili ya kujiwekea mazingira mazuri katika wakati wote wa maisha yake," alisema Maduga.

Katika tamasha hilo,kulikuwa na vionjo mbalimbali vya Utamaduni wa Wanahandeni, ikiwa ni Pamoja na Ngoma za asili kutoka katika Vijiji vya wilaya ya Handeni kama vile, Kweingoma, Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni Mjini.

Burudani kali na ya kuvutia iliyoonesha asili kamili ya Mtanzania ilitoka kwa Kundi la Sanaa la Jeshi la JKT Mgambo, Azimio Jazz band bila kusahau msanii wa kundi la Fataki, Machenja ambaye alipiga onesho la kukata kiu akiwa na wana okalandima.


Tamasha la Utamaduni Handeni ambalo linafanyika kwa mara ya Kwanza lilidhaminiwa na NSSF, Clouds FM, Vodacom, Plan B, gazeti la Mwananchi, Kajunason Blog, Chichi Local Wear, Katomu Solar specialist, Dullah Tiles and Construction, Anesa Company Limited, Country Business directory, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.
MC-Mtata, Mwani De Omar Nyangasa alifanya yake na kuhakikisha msimu wa kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni linaenda kama lilivyopangwa, Handeni Hoyeeee
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu "Bosi wangu" akiwasili katika Viwanja vya Azimio kuzindua msimu wa Kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni, ilikuwa ni raha sana ndani ya Uwanja, ambapo pia vyakula vya asili vilipatikana kwenye Tamasha hilo..
Dkt. Khalfani Haula, Mkurugenzi wa Handeni anawasalimu...Hamjambo Handeni!!
huyu ndiye Baba mwenye Nyumba, Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Thomas Mzinga

 OCD wa Handeni, Zuberi Chembela naye alikuwepo

Hawa ni wazee wa Kazi, Azimio Jazz Band....Chezea Mayenuu!!
huyu naye na Mashuka yake kama Maasai...mwanaokalandima, Machenje wa fataki alifanya yake kikwetu kwetu
Mtu Nyomi Sana
Nasema msimu wa kwanza Tamasha la utamaduni Handeni mtu Nyomi sana

Ohoo unashangaa nini sasa?? huu ndio utamaduni wenyeywe kutoka kwamsisi
Twende kazi ni ngoma za asili kwa kwenda mbele, hamna Bongo fleva wala Rhumba.....hatariiiiii
Mzee wa Kijiji...Madini iliyopbaki hapa Handeni kwetu
Funga kibwebwe tusakate sasa

Wednesday, December 11, 2013

Vyakula vya asili kupatikana ndani ya Tamasha la Handeni Kwetu



Na Mwandishi Wetu, Handeni
BAADHI ya vyakula vya asili ya Handeni, vinatarajiwa kuwapo katika Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu 2013 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani. DC ni miongoni mwa viongozi wa juu serikalini wanaoliunga mkono Tamasha hili linalofanyika kwa mara ya kwanza wilayani Handeni, huku likisubiriwa kwa hamu na wadau wa utamaduni na maendeleo hapa nchini.
Kambi Mbwana, Mratibu wa Tamasha la Utamaduni Handeni, maarufu kama Handeni Kwetu 2013, pichani. Maandalizi yamezidi kupamba moto na watu wote wanakaribishwa kujionea burudani za aina yake kwenye tukio hili la aina yake.

Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa tayari wametoa nafasi kwa wanaoweza kazi hiyo kwa umakini na usafi wa aina yake ili kuliweka tamasha hilo kwenye mguso wa aina yake.

Alisema taratibu zote zimeshafanyika ikiwamo kutembelea vikundi vitakavyotoa burudani, ambapo Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alitumia muda mwingi kuwahamasisha wadau kuhudhuria kwa wingi katika tamasha hilo, kupitia sherehe za Uhuru zilizofanyika wilayani humo Desemba 9 mwaka huu.

“Kila kitu kimekamilika, tukiamini kuwa wadau wote watakaohudhuria kwenye tamasha hilo watapata fursa ya kula vyaku7la vya asili, maana pia ni sehemu ya utamaduni wa Handeni.

“Sisi tunaamini hili ni tamasha la aina yake ambalo litashangaza watu wengi kutokana na kuandaliwa kwa kiwango cha juu, huku likianzia kwa maandamano katika Ofisi za Halmashauri ya mji Handeni kuanzia saa 2 asubuhi na kuelekea Uwanja wa Azimio,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na vyakula wala vinywaji ili kudhibiti suala la afya za watu kwa kupitia tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania wote, hususan wapenzi wa utamaduni hapa nchini.

 Wadhamini katika tamasha hilo ni gazeti la Mwananchi, Clouds Media Group, Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters, Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD), Michuzi Media Group, duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Partnership, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie
Blog na Taifa Letu.com.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...