https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, September 27, 2013

Watanzania waaswa wathamini ibada kwa ajili ya kumpendeza Mungu



Na Kambi Mbwana, Handeni
WAUMINI wa dini ya kiislamu na Watanzania kwa ujumla wameombwa washiriki katika ibada ili wajiwekee mazingira mazuri ya kumrudia Mungu na kuacha vitendo viovu.
Sheikhe wa Kijiji cha Komsala, Ramadhan Mavyombo, akizungumza jambo na watu waliohudhuria kumbukumbu ya mzee Mbwana Hemed, kijijini hapo juzi, wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Shaikhe wa Kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Ramadhan Mavyombo katika shughuli ya kumbukumbu ya marehemu Mbwana Hemed, iliyofanyika kijijini hapo juzi Septemba 25 na kuhudhuriwa na watu wengi.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Mavyombo alisema kuwa mtu anayemjua Mungu kwa kushiriki katika ibada, kamwe hawezi kutenda vitendo viovu.

Tuesday, September 24, 2013

Handeni sasa kujipanga na maabara shule za sekondari


Na Kambi Mbwana, Handeni
MKURUGENZI Mtendaji wilaya Handeni, mkoani Tanga, Khalfany Haule, amesema wanakabiriwa na changamoto ya ukosefu wa maabara kwa shule za sekondari, hivyo wanajipanga kushirikiana na wadau ili kufanyia kazi na kuinusuru elimu wilayani humo.



Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani, akiwa ofisini kwake.

Akizungumza mjini hapa, Haule alisema maabara hizo ni kwa shule zote za sekondari zilizopo wilayani humo, jambo ambalo linaweza kuchangia kufanya vibaya kwa wanafunzi kwenye mitihani ya Taifa.

Tamasha la Utamaduni Handeni Kwetu kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga


Na Mwandishi Wetu, Handeni
TAMASHA la Utamaduni lililopewa jina la ‘Handeni Kwetu 2013’ linatarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga, likiwa na lengo la kutangaza sekta ya utalii na utamaduni wilayani humo.



 Mratibu wa Tamasha la Handeni Kwetu 2013, Kambi Mbwana, ambaye pia ni Mmiliki wa mtandao huu wa Handeni Kwetu Blog, pichani.



Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Handeni, Dr Khalfany Haule, akizungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake muda mchache baada ya kuruhusu Tamasha la Handeni Kwetu kufanyika wilayani humo, Desemba 14 mwaka huu.



Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akizungumza na Handeni Kwetu Blog, jana ofisini kwake wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Handeni Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa wilaya hiyo inayoongozwa kwa sasa na Mkuu wa wilaya Muhingo Rweyemamu.

Akizungumza jana wilayani Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema wameamua kuandaa tamasha hilo ili kushirikiana na wadau wote kutangza utamaduni nchini Tanzania.

Maandalizi ya kumbukumbu ya baba yetu mzee Mbwana Hemed Masudi, yakiendelea kwa watoto kutembelea kwenye kaburi na kumuombea dua njema

Mama mzazi, Fatuma Rashid, akiomba dua ya marehemu mume wake, ikiwa ni maandalizi ya kumbukumbu ya mzee Mbwana Hemed Masudi, katika makaburi yaliyopo kijijini Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Zaina Rajabu, akimuombea dua marehemu Mbwana Hemed Masudi katika kaburi lake, ikiwa ni maandalizi ya kumfanyia kumbukumbu ya mwaka mmoja baada ya kifo chake.
 Amina Rajabu, mjomba mtu akishiriki katika dua hiyo leo.
 Rashid Mbwana, akimuombea baba yake mzee Mbwana.
Kambi Mbwana kushoto na mchumba ake Grace Misango wakishiriki kwa pamoja katika dua hiyo ya kumuombea mema mzee Mbwana Hemed Masudi, leo kijijini kwao Komsala, wiilayani Handeni, mkoani Tanga.

Sunday, September 22, 2013

DK. SEIF KHATIB AKUTANA NA KATIBU WA MAMBO YA NJE WA CHAMA CHA ANC CHA AFRIKA KUSINI.

 KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib, akimkaribisha Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana, kwa ajili ya mazungumzo na kuwasilisha, Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini.
 KATIBU wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alikimkabidhi Katibu wa NEC ya CCM, Ogamaizesheni, Muhamed Seif Khatib, kabrasha la Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini, jana, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib, akizungumza na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo na kuwasilisha, Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini.
 KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo na kuwasilisha, Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini. Wengine kushoto ni Ofisa kutoka ANC Lebogang Matshaba na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
"KOTE KULEE NILIWAHI KUFIKA..." Katibu wa Mambo ya Nje Chama cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha akimwambia Dk. Khatib wakati akiaga nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, baada ya mazungumzo yao.

Kwa Hisani:Taifa letu.com

Saturday, September 21, 2013

Al Shabaab watingisha nchini Kenya leo na kuua kadhaa na kuzua taharuki ya aina yake



Na Mwandishi Wetu, Kenya
HALI ya hatari imezidi kutingisha viunga vya Kenya baada ya watu zaidi 22 kufariki Dunia baada ya watu kuvamia Westgate nchini humo na kuzua taharuki ya aina yake.
Hali ilivyokuwa nchini Kenya leo. Picha kwa hisani ya Reuters...
Wakati vifo hivyo vikitokea huku wengineo wakisema waliokufa ni zaidi ya watu 30, kundi la wanamgambo wa kiisilamu la Al shabaab nchini Somalia limedai kutekeleza mauaji hayo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari nchini Kenya, kikundi hicho kimekiri kuhusika na kadhia hiyo, ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa bado wana nguvu za kutingisha wanavyotaka.

Waziri Muhongo azindua hafla ya udhibiti wa vihatarishi katika usimamizi wa fedha

Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Barclay's Tanzania Kihara Maina akitoa hotuba ya kumkaribisha  Mgeni Rasmi Waziri wa Wizara ya Fedha na Uchumi  Dkt. William Mgimwa katika hafla ya uzinduzi wa udhibiti wa vihatarishi katika  usimamizi wa fedha (Risk Management Solutions).Uzinduzi huo uliyofanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Waziri wa Wizara ya Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiongea na viongozi, wawezeshaji na wateja wa  Benki ya Barclays Tanzania  wakati wa  hafla ya uzinduzi wa udhibiti wa vihatarishi katika  usimamizi wa fedha (Risk Management Solutions)  iliyofanyika leo kwenye  hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa bodi ya benki ya Barclays Tanzania Fatma Karume (kulia) akisisitiza na kufurahia jambo alipokuwa anaongea na Mgeni Rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa hafla ya uzinduzi wa udhibiti wa vihatarishi katika usimamizi wa fedha (Risk Management Solutions) iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mjumbe wa bodi ya benki hiyo Suleiman Mohamed.

Je, uliyekuwa naye ana mwingine ampendae?



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI wiki nyingine tena msomaji wangu tunapokutana katika safu hii inayokujia kila Jumamosi, ikiwa na lengo la kuelezea mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano na maisha.
Wawili wapendanao, pichani.
Nashukuru kama wewe ni mpenzi wa safu hii kiasi cha kuwa pamoja kila Jumamosi. Kwa wewe ambaye si shabiki zaidi, hivyo nakuombea ili tuwe wadau kwa ajili ya kujadili mambo haya.

Ndugu msomaji wangu, ni rahisi mno kujihusisha na mapenzi na waume au wake za watu bila wewe mwenyewe kujua. Hii ni kutokana na baadhi yao kufanya siri katika mambo haya.

Wapo baadhi ya wanaume au wanawake wakiulizwa juu ya uhusiano wao, hukanusha vikali. Mara kadhaa majibu yao ni kuwa wapo huru. Ati hawana uhusiano na mtu mwingine.

Ukiwachambua zaidi, wanakueleza walikuwa nao lakini wameachana naoa kwa sababu mbalimbali. Majibu haya mara kadhaa ni kurahisisha mamabo tu ili aingie kwa mtu mwingine.

Kuachiwa kwa Masogange kwavuta hisia za wengi, nguvu na harakati za Mwakyembe sasa zajadiliwa na kuzua maswali lukuki



Na Timu ya Handeni Kwetu Blog
TUKIO la kuachiwa huru kwa msanii Agness Gerald Masogange na Melisa Edward nchini Afrika Kusini, limepokelewa kwa shingo upande na Watanzania wengi wanaofuatilia kasi ya dawa za kulevya.
Dawa za kulevya
Katika hilo, wapo wanaochukizwa na uamuzi huo wakisema kuwa ni njia ya kumdhalilisha Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyemba, aliyepania pia kulivalia njuga suala hilo.

Masogange amepigwa faini ya shilingi za Tanzania Milioni tano, kwasababu ya madai kuwa walizokutwa nazo si dawa za kulevya.



Masogange akiwa katika pozi kama unavyomuona hapo. Chezea Masogange wewe.
Katika mitandao ya kijamii na mitaani, kila mmoja anasema lake, huku wengineo wakifika mbali zaidi kupekua na kuorodhesha vifungu vya maswali vya kuangalia sakata hilo.

Masogange ametiwa hatiani na kalipa faini. Melisa ameachiwa huru. Kesi yao imekuwa rahisi baada ya kubainika kwamba yale waliyobeba yalikuwa si madawa ya kulevya bali mali ghafi mojawapo ya kutengenezea madawa ya kulevya.

Waziri wa Uchukuzi, Harrison Makyembe, pichani.
Mtanzania mmoja, anayejulikana kwa jina la Ibrahim Mkamba, aliandika mambo mengi kwenye wall yake facebook. Na haya ndiyo aliyoandika na sisi tumeyachukua kama yalivyo kama ishara ya kupanua wigo wa kufikiri juu ya vita ya dawa za kulevya Tanzania kama tulivyoweka mengine hapo chini ili kupata la kujadili juu ya vita hii.
Melisa Edward pichani, aliyeachiwa sambamba na Masogange, nchini Afrika Kusini, baada ya kuonekana hana hatia.

"Tungekuwa serious na kama watu wanaokubalika na watu hawahusiki na sula hilo, tungefanya upelelezi wetu wa kina ili usaidie kuziba mianya yote ya suala hilo kwa kupata kutoka kwa Masogange na Mellisa fact:-
1. kwamba walisafirisha mali hiyo wakijua kwamba ni mali ghafi ya madawa ya kulevya?

2. kwamba waliitoa wapi mali ghafi hiyo na walikuwa wanampelekea nani au taasisi gani Afrika Kusini?

January Makamba apinga kuhusisha siasa na mgogoro wa kiwanda cha chai Bumbuli



Ray Said, Bumbuli
Naibu  Waziri  wa  Mawasiliano  Sayansi na  Teknolojia  January  Makamba  amewataka  baadhi  ya watu  kuondokana  na dhana  ya  kusema  mgogoro  wa  kiwanda cha  chai  cha  Mponde   ni siasa badala  yake amewataka  kuiacha  serikali  indelee na taratibu zake  za  kulitafutia  ufumbuzi  swala hilo. 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, pichani.
Makamba  ambaye pia ni Mbunge  wa  jimbo  la Bumbuli, alisema lazima ashirikiane na wananchi wake na si kikundi cha watu wachache licha ya kutukanwa kwa kwasababu ya kuwaunga mkono wananchi.

Naibu  waziri huyo alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya watu kuliingiza suala hilo kwenye kisiasa na kwamba lina maslahi binafsi  huku mambo hayo yakiachwa tangu mwaka 2010  baada ya kumalizika uchaguzi, hivyo kwa sasa ni wakati wa kuleta maendeleo.

“Siamini   kama  kuwaunga  mkono  wananchi  walionichagua yanatokana na tofauti za kisiasa kwani eneo hili linamilikiwa na Chama kimoja ambacho ni Chama cha Mapinduzi na wala sina  maslahi binafsi katika suala hilo,” alisema Makamba nakuongeza kuwa  yeye anawasimamia  wakulima wa zao la chai.

Friday, September 20, 2013

Mbeya City mdomoni mwa Simba mwenye uchu wa nyama kesho Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Simba mazoezini na kocha wao msaidizi Jamhuri Kihwelo Julio.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.

Jumuiya ya wazazi CCM mkoani Tanga yatema cheche



Wana CCM, pichani. Picha na maktaba yetu.
Na Ray Said, Lushoto
VIONGOZI wa  Jumuiya  ya  wazazi  wilayani  Lushoto,  mkoani  Tanga, wameshauriwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye juhudi kwasababu siasa  za wakati huu zimejaa ushindani na kunahitajika utekelezaji  wa  sera  zilizowekwa  ili kuweza  kukipatia Chama cha Mapinduzi (CCM) ushindi  wa  kishindo mwaka  2015.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti  wa  Wazazi  Mkoani  Tanga  Dkt Edmund Mndolwa, alisema hayo katika ziara ya  kuwashukuru kwa kumchagua kwa  kishindo katika  nafasi  hiyo ya  kuwa  mwenyekiti  wa Jumuiya hiyo na kutembelea wilaya zote 9 za Mkoa wa Tanga.

Alisema imekuwa ni jambo la kawaida kwa wenyeviti na Makatibu kufanya kazi kimazoea kwa kufanya kazi zisizo eleweka kwa kigezo cha kuwa Chama Cha Mapinduzi tayari ni chama kikubwa na kinapendwa na kuza hofu kwa mustakabali wa siasa za Tanzania.

Waziri Chizza aingilia kati mgogoro wa wakulima wa Chai wilayani Lushoto, mkoani Tanga



Na  Ray Said, Bumbuli
WAZIRI  wa  Chakula, Kilimo  na  Ushirika, Injinia Christopher  Chizza, amependekeza kuundwa kwa menejimenti ya muda katika kiwanda cha chai cha Mponde kama njia ya kusuluhisha mgogoro uliopo kati ya wakulima wa chai na mwekezaji wa kiwanda hicho, Kampuni ya Chai Lushoto.  
 Injinia Christopher  Chizza, katikati.
Akizungumza katika mkutano wa  hadhara  uliofanyika  katika  uwanja  wa  mazoezi katika kata ya Mponde, Chiza  pia aliahidi kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wakulima hao wa chai na mwekezaji wa kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Bumbuli, mkoani Tanga, ili kiendelee kutoa huduma bora.

 Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda kuhusu suala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo.

"Nitaishauri  serikali  kuchukua  kiwanda  hicho  na  baadaye   kuwakabidhi  wananchi  ambao  ndio  wamiliki  wa  kiwanda  hicho," alisema.

Karima ChiChi Mhandeni ashusha mzigo wa nguvu kutoka Dubai

Karima ChiChi Mhandeni, akionekana pichani. Sasa ameleta mali mpyaaaaa kabisa. 

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI na mdau wa muziki wa dansi nchini, Karima ChiChi Mhandeni, ameingiza mali mpya katika duka lake linalojulikana kama Chichi Yusuphed lilipo Kinondoni kwa Manyanya jijini Dar es Salaam.

                        
                                           Mzigo mpya huo uneonekana.
                                       Mzo mpyaa kabisa.
Akizungumza mara baada ya kutua katika ardhi ya Tanzania, akitokea Dubai, Chichi alisema amekuja na mali mpya na wateja watakaopata mzigo huo wataukubali.
“Kuna mzigo wa aina mbalimbali hivyo naomba wateja wetu waje kwa wingi kujionea namna tulivyoshusha vitu makini na vyenye uwezo wa kuwatoa bomba,” alisema.
                              Mzigo huu kama kawaida.
Karima ni miongoni mwa wadau makini wa kike wa muziki wa dansi hapa nchini, huku mchango wake ukiungwa mkono na watu wengi.

Tegua kitendawili, nani zaidi ya kati ya Diamond na Ommy Dimpozi kwa Bongo Fleva hawa?



KUNA wasanii makini na waofanya vyema mno katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva. Si wengine, ila ni Diamond Platinum na mwenzake Ommy Dimpozi. Hawa vijana wanazua maswali mengi mtaani.

Kila mmoja anasema lake. Wapo wanaosema Diamond ni zaidi na mwingine anamuweka juu Ommy. Jana mitaa ya Kinondoni tulikuta ubishani wa hali ya juu.

Diamond kwa ameachia wimbo wake My Number One, wakati mwenzake Dimpozi anatamba na kibao chake cha Tupogo. Aidha Dimpoz pia ameshatamba na nyimbo kadhaa, ukiwamo ule wa Nai Nai. 

Wakati Diamond yeye alishakuwa na vibao motomoto ukiwamo ule wa Nimpende Nani.

Je, wewe una0na nani ni mkali zaidi ya mwenzake? Najua una mtu unayemkubali sana. Nataka nifahamu nani zaidi kwa upande wako? Binafsi kichwa kinauma. Nikisema Diamond mkali, nikianza kumfuatilia Dimpoz du hataree.

Pia hawa jamaa wamekuwa na mashabiki kadhaa kutokana na life style zao kitaani kwetu. Unajua nini ehee? Ati jamaa hawa ni wazee wa Pamba. Kuna mmoja anajiita yeye ni Rais wa Wasafi.

Weeee. Tena mtindo huo unaacha watu kinywa wazi hataree. Unajua nini ehee? Baadhi yao wanataka sana kujigandisha kwao kutokana na kung’aa kwao. Na ndio maana mmoja wapo hapo anaonekana kiwembe ile mbayaa.
Nataka uniambie nani kwako zaidi?
Tutumie barua pepe au msg ikisema nani zaidi kati yao.
+255712053949

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...