https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, July 27, 2013

Happy Birthday bwana mkubwa Yusuphed Mhandeni, Taifa linahitaji mchango wako



Happh Birthday Yusuph Shaban Mhandeni, Yusuphed Mhandeni kama anavyojulikana. Siku kama ya leo alizaliwa. Aliyesimama mbele ya magari ya Phed Trans ni Karima ChiChi Mhandeni, mke wa Yusuphed Mhandeni ambaye ndio anayemuweka sawa kiongozi huyu ambaye pia ni Mchumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Makumbusho, jijini Dar es Salaam. Picha na Maktaba Yetu.



 Happy Birthday kaka Yusuphed Mhandeni. Hapa amesimama mbele ya magari yanayojulikana kama Phed Trans yanayofanya safari zake Dar es Salaam na Mkata, wilayani Handeni, mkoani Tanga.



Happy Birthday bwana mkubwa Yusuph Shaban Mhandeni. Kichwa chako kiendelee kufanya kazi kwa manufaa ya Taifa hili. Hapa Mhandeni kulia akizungumza na vijana wa tawi la Yanga la Green Stone, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam. Picha na Maktaba yetu.

Makamu wa Rais, Dkt Gharib Bilal apokea maandamano ya maonyesho ya vikundi vya wakulima mjini Morogoro

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro.

Msanii wa kizazi kipya, Mady Salu afunga mkanda kulilia ujiko



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva, Ahmad Salum, maarufu kama Mady Salu, amesema kwamba yupo kwenye mipango ya aina yake ya kumpatia mafanikio.
Msanii Mady Salu akijiachia kama hivyo.
Mady Salu ni kati ya vijana wanne waliotamba na kundi lao la Ngovita Clew lililokuwa na maskani yake Tandale jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kuachia wimbo wao wa ‘Maisha Miangaiko’.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mady Salu alisema kwamba kwa sasa amesharekodi wimbo wake wa Tatizo ni ‘Kama Unanipenda’, wimbo aliorekodi katika Studio za BM Records.

Wasanii wetu acheni vituko mitaani, tumechoka



Je, mzima?
NATUMIA muda huu kuwakumbusha wasanii wetu juu ya kuacha vituko vyao mitaani, maana wao ndio vinara wakati wanajua kuwa usanii ni kioo cha jamii.
Msanii Aunt Ezekiel akijiachia kama unavyomuona hapo.
Kwa kufanya hivyo, jamii itanufaika kutoka kwao, jambo ambalo kwa sasa ni gumu kulipata kutoka kwa wasanii wetu wanaoishi kwa vituko na kuandikwa vibaya magazetini.

Nasema hivi kwasababu mimi ni shabiki wa sanaa na wasanii, hivyo inapotokea mapungufu kama haya ya kutia hawanazo siwezi kubaki kimya nikililia maendeleo ya kazi yao.

Ni kwasababu hiyo, naomba wasanii wetu waone yale yenye kutia moyo na kuelimisha jamii, huku vitendo vya kufanya uhuni, uvutaji wa dawa za kulevya, uzinzi na uchafu mwingineo wauache.

Naamini kwa kufanya hayo, sisi wadau wao tutanufaika kwa kiasi kikubwa, ukizingatia kuwa msanii anapofanya lolote, kuna wanaopenda kuwaiga kwa sababu za aina mbalimbali.

Kwa mfano, leo msanii hata akivaa nusu uchi, akapita mtaani kwao, basi wale wanaowaona nao wanatamani kuwa kama hao, hivyo kuonyesha hasara kubwa katika jamii yao.

Jambo hili haliwezi kukubalika hata kidogo, ndio maana kwa mapenzi yangu kwao nikaona niandike barua hii nikiamini kuwa ujumbe utafika kwa hadhira.

Nitafurahi kama walengwa ambao ni wasanii pamoja na mashabiki wao watausoma ujumbe huu na kuamua kubadilika kwa ajili ya faida ya jamii inayowazunguuka.

Joseph Kirubo
Chalinze, mkoani Pwani.

Na wewe unaweza kutoa unachokiona, usichopenda katika jamii yako, iwe siasa, uchumi, sanaa na mengineyo kwa kututumia barua fupi kwa emai kambimbwana@yahoo.com au meseji kwa namba +255 712 053949 kisha sisi tutaandika. Pia unaweza kutuma na picha yako kama utaona inafaa na kuwekwa kila Jumamosi.

MAMBO FULANI MUHIMU:Ndio tatizo la kujirahisi, jichunge mwanakwetu



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI siku nyingine tena tunapokutana katika safu hii inayokujia kila Jumamosi, huku nikiamini kuwa tutaendelea kuwa pamoja tukielezea mambo ya uhusiano na maisha.
Wawili wapendanao wakitafakari love yao.

Nitakuwa mchoyo wa fadhira kama nitashindwa kukushuru wewe unayeguswa na safu hii kiasi cha kutufanya tuwe wote kila wiki tukichambua mambo haya ya uhusiano.

Hakika ndio furaha yangu, maana bila wewe safu hii haiwezi kuwa na mashiko kwa namna yoyote ile. Baada ya kusema hayo, nirudi kwenye mada yangu ya wiki hii.

Friday, July 26, 2013

Taifa Stars hakuna kulala kesho mechi na wenyeji wao Uganda

Na Boniface Wambura, Uganda
MOJA ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
Kocha Kim Poulsen amesema maandalizi ya Taifa Stars jijini Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo ambayo Uganda inaongoza kwa bao 1-0 yalikuwa mazuri, lakini mabao ni muhimu hivyo watashambulia bila kusahau kulinda lango lao.

“Unapocheza mechi za aina hii za nyumbani na ugenini, huku mwenyeji akiwa anaongoza mabao yana maana kubwa katika mechi. Mabao yanabadili mchezo na pia wachezaji kifikra,” amesema Kim akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mt. Zion ambayo Stars imefikia.

DC Handeni aunga mkono juhudi za kuitangaza wilaya



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amewataka wadau na wananchi kuunga mkono juhudi za kuitangaza wilaya yao kwa kupitia watu mbalimbali, ikiwamo blog ya Handeni Kwetu.
Muhingo Rweyemamu, Mkuu wa wilaya Handeni.
Akizungumza hivi karibuni wilayani humo, Muhingo alisema kuwa juhudi zinazofanyika zinahitaji kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa, ili maendeleo yapatikane kwa vitendo.

Alisema hata kuanzishwa kwa blog ya Handeni Kwetu ni namna ya kuendeleza juhudi hizo kwa ajili ya kutafuta maendeleo kwa namna moja ama nyingine, jambo linalotia moyo.

Yanga wajivunia mazoezi ya kutetea ubingwa wao wa ligi ya Tanzania Bara

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema kuwa unaamini mazoezi wanayofanya wachezaji wao katika Uwanja wa Luyola, utawaweka katika nafasi nzuri katika michuano ijayo ya Ligi ya Tanzania Bara msimu ujao.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto
Ligi hiyo ambayo Yanga ndio mabingwa watetezi imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu 14 kuwania taji hilo.

Akizungumza mapema wiki hii, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema timu yao inafanya mazoezi kabambe kwa ajili ya kuwaweka sawa.

Alisema kwa kupitia uhodari wa kocha wao Ernest Brandit, wana amini mambo yatakuwa mazuri katika kuifanya timu yao itishe msimu ujao na kutetea vema taji lao.

“Timu yenye wachezaji wa ushindi wanafanya mazoezi yao katika Uwanja wa Luyola, huku tukiamini kuwa ubora wao utashangaza wengi.

“Lengo ni kutetea ubingwa wetu tuliyoutwaa msimu uliopita, hivyo kwa sasa majukumu yote yapo kwa benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla,” alisema.

Juzi katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki, Yanga walitoka sare dhidi ya timu ya URA ya nchini Uganda, ambayo walipocheza na Simba, waliibuka na ushindi wa bao 2-1.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...